Naweza kunyonyesha ninapotumia tembe za kutoa mimba?

Unaweza kunyonyesha unapoavya mimba kwa kutumia tembe [1]. Mifepristone na Misoprostol zinaweza kuingia katika maziwa ya mama lakini viwango ni vidogo na husagwa haraka. Kwa sababu ya viwango vidogo vinavyoweza kuwepo, unaweza kuangazia kumnyonyesha mtoto wako, ukitumia Misoprostol, kisha kusubiri saa 3 kumnyonyesha tena. Ikiwa unatumia vipimo vya ziada vya Misoprostol, unaweza kunyonyesha, kisha utumie kipimo kingine. Ingawa hii ni njia, si lazima na ni hiari yako.

[1] National Abortion Federarion (NAF). Clinical Policy Guidelinesfor Abortion Care. 2018. Retrieved from: https://5aa1b2xfmfh2e2mk03kk8rsx-wpengine.netdna-ssl.com/wp-content/uploads/2018_CPGs.pdf

Kabla ya kumeza tembe ya kutoa mimba FAQs

TAZAMA MASWALI ZAIDI

*Hakuna kinachotolewa hapa kinapaswa kudhaniwa kuwa ushauri wa kitaalam na hakuna dawa / tembe zinazopaswa kutumiwa bila agizo kutoka kwa mtaalamu aliye na leseni / aliye sajiliwa anayestahili kuagiza dawa hiyo katika mamlaka yako ya karibu.