Mbona tovuti zingine zina taarifa tofauti kuhusu tembe za kutoa mimba?

Kuna taarifa kinzani nyingi kuhusu utoaji mimba sio tu katika mtandao, lakini pia miongoni mwa wauzaji wa tembe za kutoa mimba wasioruhusiwa na hata wahudumu wa afya. Kwa sababu utoaji mimba umebanwa katika nchi nyingi na watu wengi wanapinga utoaji mimba, ni rahisi kupata taarifa za kimapendeleo ambazo hazijajikita katika ushahidi wowote wa kisayansi. Tunaamini kuwa ni muhimu kufuata taarifa zinazojikita kwenye mapendekezo ya mashirika ya kimataifa ya utabibu na wataalamu katika utoaji mimba.

Taarifa zote ambazo hutolewa na safe2choose katika tovuti yake hujikita kwa tafiti za kisayansi zilizofanywa na mashirika ya kimataifa ya utabibu. Washauri wetu na madaktari wa utabibu wamepewa mafunzo ili kukupa taarifa za kina zaidi na ushauri unaofaa kwa utoaji mimba wa utabibu. Bonyeza hapa ili kusoma habari za kuaminika kuhusu utoaji mimba au wasiliana nasi ikiwa una maswali.

Ikiwa unataka kusoma taarifa zingine za kutegemewa, tunapendekeza utembelee mitandao ifuatayo:

TAZAMA MASWALI ZAIDI

*Hakuna kinachotolewa hapa kinapaswa kudhaniwa kuwa ushauri wa kitaalam na hakuna dawa / tembe zinazopaswa kutumiwa bila agizo kutoka kwa mtaalamu aliye na leseni / aliye sajiliwa anayestahili kuagiza dawa hiyo katika mamlaka yako ya karibu.