Tembe za kutoa mimba ni nini? Zina nini?

Kuna tembe mbili ambazo hutumika sana kwa utoaji mimba [1], Mifepristone na Misoprostol. Mifepristone huzuia homoni ya uja uzito inayohitajika kwa ukuaji wa mimba, na Misoprostol husaidia mlango wa uzazi kutulia na tumbo la uzazi kijikunja ili kutoa uja uzito

Ni muhimu kujua kuwa tembe za kutoa mimba ni tofauti na tembe ya asubuhi baadaye au dawa za kupanga uzazi za dharura (levonorgestrel, ulipristal). Kwa taarifa zaidi kuhusu dawa za kupanga uzazi za dharura, bonyeza hapa

[1] WHO. Safe abortion: technical and policy guidance for health systems. Second edition. 2012. Retrieved from: https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/70914/?sequence=1

TAZAMA MASWALI ZAIDI

*Hakuna kinachotolewa hapa kinapaswa kudhaniwa kuwa ushauri wa kitaalam na hakuna dawa / tembe zinazopaswa kutumiwa bila agizo kutoka kwa mtaalamu aliye na leseni / aliye sajiliwa anayestahili kuagiza dawa hiyo katika mamlaka yako ya karibu.