Je utoaji mimba ni hatari?

Utoaji mimba kwa utabibu au upasuaji unapofanywa vyema, ni utaratibu salama zaidi. Hatari ya kuwa na utata ni chini ya 1% kwa utoaji mimba wa utabibu na takriban 1% kwa utoaji mimba wa upasuaji [1] Ikiwa utakuwa na utata baada ya utoaji mimba wa utabibu au upasuaji, inashauriwa utafute matibabu katika muda unaofaa. Kujua unapohitaji kutafuta msaada itakusaidia kulinda afya na uwezo wako wa kuwa na uja uzito, na kuzuia hali hatari.

Kuna njia mbili za kuwa na utoaji mimba katika wiki 11 za kwanza za uja uzito: Utabibu na upasuaji. Utoaji mimba wa utabibu unaweza kufanywa kwa Mifepristone na Misoprostol au Misoprostol pekee. Uavyaji mimba kwa upasuaji katika kiwango hiki hufanywa na mbinu inayojulikana kama u ufyonzaji wa kijusi kwa mrija [2]


Sources

[1] Ipas. (2019). Clinical Updates in Reproductive Health. L. Castleman & N. Kapp (Eds.). Chapel Hill, NC: Ipas. Retrieved from: https://ipas.azureedge.net/files/CURHE19-april-ClinicalUpdatesInReproductiveHealth.pdfh

[2] Ipas. Steps for performing manual vacuum aspiration using the Ipas MVA Plus® and EasyGrip® cannulae. Retrieved from: https://ipas.azureedge.net/files/PERFMVA-E19.pdf

*Hakuna kinachotolewa hapa kinapaswa kudhaniwa kuwa ushauri wa kitaalam na hakuna dawa / tembe zinazopaswa kutumiwa bila agizo kutoka kwa mtaalamu aliye na leseni / aliye sajiliwa anayestahili kuagiza dawa hiyo katika mamlaka yako ya karibu.

Tuko hapa kukuunga mkono Kwa chaguo lako la kuavya mimba wakati wa COVID-19

Tunafuatilia Kwa makini ueneaji wa virusi vya Corona kimataifa na tutaendelea kusasisha habari na huduma zetu.

Tunawashauri wasomaji wetu:

  1. Kusoma chapisho letu la hivi karibuni la blogi juu ya uavyaji wa mimba na COVID-19
  2. Kufuata miongozo ya usalama wa Shirika la Afya Duniani kuhusu COVID-19
  3. Kuwasiliana na washauri wetu