Ukubwa wa maandishi
safe2choose

Aina za Utoaji Mimba wa Kliniki

Utoaji mimba wa kliniki ni taratibu za kitabibu zinazotumika kukatiza mimba au kushughulikia mimba iliyoharibika. Wakati mwingine huitwa utoaji mimba wa upasuaji au utoaji mimba wa kitaratibu, na pia huweza kuitwa kwa jina la mbinu maalum inayotumika, kama vile utoaji mimba kwa kunyonya. Kuna aina mbalimbali za njia za utoaji mimba wa kliniki, kulingana na hatua ya ujauzito. Ukurasa huu unaeleza kila aina ya taratibu hizi na unachoweza kutarajia.

YOTE UNAYOPASWA KUJUA

Je! Kutoa mimba Katika kliniki ni nini?

Utoaji mimba wa kliniki ni taratibu ya kitabibu inayotumia vifaa au njia ya kuvuta kukatiza mimba au kushughulikia mimba iliyoharibika. Hufanywa na watoa huduma ya afya waliobobea katika kliniki au hospitali.

Medical setup with suction instruments and electric devices representing in-clinic abortion by trained healthcare providers.

Utoaji mimba wa kliniki ni taratibu ya kitabibu inayofanywa na watoa huduma ya afya waliobobea katika mazingira ya kliniki au hospitali. Taratibu hizi kwa kawaida ni salama na zina ufanisi wa takriban asilimia 99, ingawa usalama na uzoefu vinaweza kutofautiana kulingana na mbinu inayotumika na hatua ambayo ujauzito umefikia.

Njia za utoaji mimba wa kliniki hufanya kazi kwa kutumia dawa au mbinu za kitabibu kufungua mlango wa kizazi taratibu (inayojulikana kama upanuaji). Baada ya mlango wa kizazi kufunguka, mimba hutolewa kutoka kwenye mfuko wa uzazi kwa kutumia njia ya kunyonya, vifaa vya upasuaji, au kwa kusababisha misuli ya uzazi kujikaza ili kufanikisha utoaji.

Baadhi ya taratibu ni za haraka na hufanywa kwa mfumo wa mgonjwa wa nje, ilhali nyingine huenda zikahitaji mtu kubaki kliniki au hospitali kwa ajili ya uangalizi na kupona, hasa katika hatua za mwisho za ujauzito.

Kuna njia gani tofauti za utoaji mimba katika kliniki?

View and Download

Kuna mbinu kadhaa salama za utoaji mimba wa kliniki ambazo unaweza kuchagua, na mara nyingi hutegemea umri wa ujauzito. Kwa sababu kuna kufanana kwa kiasi fulani katika umri wa ujauzito kwa mbinu tofauti za utoaji mimba, uamuzi pia unaweza kutegemea eneo la kijiografia, upatikanaji wa vifaa, pamoja na mapendeleo ya mtoa huduma na ya binafsi.

Njia ya kunyonya au kufyonza ni aina ya utoaji mimba kwa njia ya kuvuta mfuko wa uzazi kwa mikono, na kwa kawaida hutumika hadi ujauzito wa wiki 14

Njia ya Upanuaji na ukwanguaji kwa njia ya electoniki ni aina ya utoaji mimba kwa njia ya kuvuta kwa kutumia umeme, na mara nyingi hutumika hadi ujauzito wa wiki 16

Njia ya upanuaji na ukwanguaji ni mbinu zinazotumika mara kwa mara baada ya ujauzito wa wiki 14

Njia ya kutishia/Uchocheaji wa mimba inapochaguliwa, kwa kawaida hufanyika kwa ujauzito uliozidi wiki 16

Njia ya Usafishaji wa kizazi ni mbinu ya zamani ya utoaji mimba na kwa kiasi kikubwa imebadilishwa na mbinu za utoaji mimba kwa njia ya kuvuta mfuko wa uzazi na Njia ya upanuaji na ukwanguaji.

Tazama na Upakue mchoro wetu wa taarifa kuhusu mbinu za utoaji mimba kwa kila hatua ya ujauzito.

Stylized blue suction medical instrument representing Manual Vacuum Aspiration (MVA), a safe abortion method for pregnancies up to 14 weeks.

Je! kutoa mimba kwa njia ya kunyonya au kufyonza ni nini?

Njia ya kunyonya au kufyonza ni njia salama sana ya utoaji mimba kwa ujauzito wa kipindi cha kwanza cha mimba, na/au sehemu ya awali ya kipindi cha pili cha mimba hadi kufikia wiki 14 za ujauzito. Kikomo cha umri wa ujauzito kwa Njia ya kunyonya au kufyonza mara nyingi hutegemea kliniki pamoja na mtoa huduma ya afya anayefanya taratibu hiyo.
Chunguza maelezo

Njia ya kunyonya au kufyonza hufanywa na mtoa huduma aliyehitimu katika kliniki.

Wakati wa taratibu, mtoa huduma hutumia vifaa, ikiwa ni pamoja na kifaa cha kunyonya kisichotoa kelele, ili kuondoa mimba kutoka kwenye mfuko wa uzazi. Mara nyingi, taratibu hii hufanywa kwa kutumia ganzi ya sehemu tu ya mwili huku mtu akiwa macho, na kawaida huchukua kati ya dakika 5 hadi 10. Mtu anaweza kuhisi maumivu ya tumbo wakati wa taratibu, na kuna uwezekano wa kutokwa na damu kwa vipindi vya hapa na pale kwa siku au wiki kadhaa baada ya taratibu.

Teal electric device on light blue background, symbolizing Electric Vacuum Aspiration (EVA) abortion method.

Je! Njia ya Upanuaji na ukwanguaji kwa njia ya electoniki ni nini?

Njia ya Upanuaji na ukwanguaji kwa njia ya electoniki ni njia salama na inayofanana sana na Njia ya kunyonya au kufyonza. Njia ya Upanuaji na ukwanguaji kwa njia ya electoniki inaweza kutumika kwa ujauzito wa kipindi cha kwanza cha mimba, na/au sehemu ya awali ya kipindi cha pili cha mimba hadi kufikia wiki 16 za ujauzito.Njia ya Upanuaji na ukwanguaji kwa njia ya electoniki hufanywa na mtoa huduma aliyehitimu katika kliniki.
Chunguza maelezo

Wakati wa taratibu, mtoa huduma hutumia vifaa, ikiwa ni pamoja na kifaa cha kunyonya kwa kutumia umeme ili kuondoa mimba kutoka kwenye mfuko wa uzazi.

Tofauti kuu kati ya Njia ya Upanuaji na ukwanguaji kwa njia ya electoniki na Njia ya kunyonya au kufyonza ni kwamba kwa Njia ya Upanuaji na ukwanguaji kwa njia ya electoniki , umeme hutumika kuunda nguvu ya kunyonya ili kuondoa mimba. Kwa sababu Njia ya Upanuaji na ukwanguaji kwa njia ya electoniki inahitaji umeme, huenda isipatikane katika maeneo yenye rasilimali haba. Katika maeneo ambapo inapatikana, watoa huduma huenda wakapendelea kutumia Njia ya Upanuaji na ukwanguaji kwa njia ya electoniki badala ya Njia ya kunyonya au kufyonza kwa sababu inaweza kufanywa kwa haraka zaidi, hivyo kupunguza muda wa taratibu. Tofauti nyingine muhimu ni kwamba mashine ya Njia ya Upanuaji na ukwanguaji kwa njia ya electoniki hutoa kelele kwa sababu inatumia umeme.

Medical instruments on a light blue background, representing the Dilation and Evacuation (D&E) second-trimester abortion method.

Je! kutoa mimba kwa Njia ya upanuaji na ukwanguaji ni nini?

Njia ya upanuaji na ukwanguaji ni mojawapo ya mbinu zinazotumika sana kwa ajili ya utoaji mimba katika kipindi cha pili cha ujauzito (kati ya wiki ya 13 hadi 24 za ujauzito). Taratibu hii kwa kawaida hufanyika katika kliniki au hospitali na hufanywa na mtoa huduma ya afya aliyehitimu, na mara nyingi huchukua kati ya dakika 10 hadi 30. Watu wengi huruhusiwa kurudi nyumbani siku hiyohiyo na kupona haraka. Inapofanywa na watoa huduma wenye uzoefu, Njia ya upanuaji na ukwanguaji ni chaguo salama kiafya la utoaji mimba wa kliniki.
Chunguza maelezo

Upanuaji: Mlango wa kizazi (sehemu ya chini ya mfuko wa uzazi) hufunguliwa taratibu, au kupanuliwa. Hili hufanyika kwa kutumia dawa au vifaa vya kitabibu ili kuufungua mlango wa kizazi. Mchakato wa upanuaji unaweza kuchukua saa kadhaa au hata siku, kutegemea na umri wa ujauzito.

Uondoaji/ukwanguaji: Baada ya mlango wa kizazi kufunguliwa vya kutosha, mtoa huduma aliyehitimu huondoa mimba kutoka kwenye mfuko wa uzazi kwa kutumia njia ya kuvuta na vifaa maalum kama vile forceps. Mara nyingi, kifaa cha ultrasound hutumika kuhakikisha kuwa taratibu inafanywa kwa usalama. Usimamizi wa maumivu, kama vile ganzi ya sehemu au usingizi mwepesi, huweza kutolewa ili kupunguza maumivu au usumbufu.

Hata hivyo, upatikanaji wa taratibu za Njia ya upanuaji na ukwanguaji unaweza kutofautiana kulingana na eneo, sheria za nchi, na kanuni za kitabibu. Katika baadhi ya maeneo, huduma hii hupatikana kwa maombi; katika maeneo mengine, inaruhusiwa tu chini ya masharti fulani, kama vile sababu za kiafya. Ikiwa unafikiria kuhusu Njia ya upanuaji na ukwanguaji , ni muhimu kuzungumza na mtoa huduma ya afya au shirika la kuaminika la afya ya uzazi ili kuelewa chaguo lako.

Syringe and medicine vial icon on light blue background, representing induction abortion used in second and third trimester pregnancies.

Utoaji Mimba kwa Njia ya Uchocheaji ni Nini?

Utoaji mimba kwa njia ya uchocheaji ni mbinu inayotumika katika kipindi cha pili au cha tatu cha ujauzito (kwa kawaida baada ya wiki 16 au zaidi). Wakati mwingine, njia hii hutumika kwa utoaji mimba wa hiari, lakini mara nyingi zaidi hutumika pale ambapo kuna sababu za kiafya kwa mtu mjamzito au kwa fetasi, hali inayofanya kukatiza mimba kuwa hatua salama zaidi. Sababu za kutumia njia hii hutofautiana sana kulingana na eneo la kijiografia na sheria au vikwazo vinavyohusika.
Chunguza maelezo

Mbinu hii huiga uchungu wa kujifungua kwa kutumia dawa zinazochochea upanuaji wa mlango wa kizazi na mikazo ya mfuko wa uzazi ili kuondoa mimba. Kwa kuwa njia hii ya utoaji mimba hufanyika katika hatua za baadaye za ujauzito, hufanyika daima katika kliniki au hospitali ambapo mtu anaweza kufuatiliwa kwa karibu wakati wote wa taratibu.

A hidden instrument behind a warning sign in gray, portraying an outdated surgical abortion method, no longer recommended.

Je! Njia ya Usafishaji wa kizazi ni nini?

Ya zamani
Njia ya Usafishaji wa kizazi ni mbinu ya zamani ya utoaji mimba kwa upasuaji ambayo kwa kiasi kikubwa imebadilishwa na mbinu za utoaji mimba kwa njia ya kunyonya. Mbinu hii haipendekezwi tena.
Chunguza maelezo

Wakati wa Njia ya Usafishaji wa kizazi, mlango wa kizazi hufunguliwa, kisha vifaa vyenye ncha kali vinavyoitwa curettes hutumika kukwangua kuta za mfuko wa uzazi ili kuondoa mimba. Kuna hatari kubwa zaidi ya kupata matatizo pamoja na maumivu ikilinganishwa na utoaji mimba kwa njia ya kuvuta. Kwa sababu hii, Shirika la Afya Duniani linapendekeza kwamba Njia ya Usafishaji wa kizazi ibadilishwe na mbinu ya utoaji mimba kwa njia ya kuvuta,Njia ya upanuaji na ukwanguaji, au utoaji mimba kwa vidonge inapowezekana.

SALAMA NA YENYE UFANISI

Je! Mimba katika kliniki ni salama?

Utoaji mimba wa kliniki ni taratibu salama zinapofanywa na watoa huduma ya afya waliobobea.

Kliniki zinazotoa huduma za utoaji mimba kwa njia ya kuvuta au kwa upasuaji zinapaswa kufuata viwango vya kitabibu vinavyotegemea kanuni za kitaifa na miongozo ya kimataifa, kama vile Mwongozo wa Shirika la Afya Duniani wa Huduma za Utoaji Mimba na Taarifa za Kliniki za Ipas.

Miongozo hii husaidia kuhakikisha usalama na ubora wa huduma kwa kushughulikia mambo yafuatayo:

  • Ni nani aliyehitimu kutoa huduma za utoaji mimba
  • Jinsi dawa za utoaji mimba zinapaswa kuhifadhiwa na kutumika
  • Usafishaji na utunzaji sahihi wa vifaa
  • Utupaji salama wa taka za kitabibu
  • Mafunzo, usimamizi, na tathmini ya wafanyakazi wa afya

Watu wanaotafuta utoaji mimba wa kliniki wanapaswa kuchagua kliniki inayotumia mbinu salama zilizothibitishwa na inayozingatia miongozo ya kisasa ya kitabibu ili kulinda afya na ustawi wao.

HATARI NA ISHARA ZA ONYO

Kuna hatari na shida gani za utoaji mimba katika kliniki?

Wakati utoaji mimba wa kliniki unafanywa na wataalamu wa afya waliopata mafunzo katika kituo kilichoidhinishwa na kuna upatikanaji wa vifaa sahihi, ni salama sana na una hatari ndogo sana ya matatizo. Kwa mfano, utoaji mimba kwa njia ya kunyonya ni salama na wa ufanisi mkubwa, ukiwa na viwango vya mafanikio vya zaidi ya asilimia 98 hadi 99 na viwango vya matatizo makubwa chini ya asilimia 1.

Hata hivyo, bado kuna baadhi ya hatari zinazoweza kutokea kutokana na taratibu hizi, kama ilivyo katika huduma nyingine za kimatibabu. Hizi ni pamoja na: kutokwa na damu nyingi, maambukizi, kuumia kwa mfuko wa uzazi au viungo vya karibu, utoaji mimba kutokukamilika au mabaki ya mimba kubaki ndani ya mfuko wa uzazi, mimba kuendelea, na hata kifo.

Matatizo mengi si ya kutishia maisha na yanaweza kutibiwa. Hii ndiyo sababu ya umuhimu wa kufuatilia dalili za onyo baada ya utoaji mimba.

Ikiwa utapata mojawapo ya dalili au ishara zifuatazo, unapaswa kutafuta huduma ya matibabu mara moja:

  • Kutokwa na damu nyingi (kulowesha kabisa pedi mbili kila saa, kwa saa mbili mfululizo au zaidi);

  • Homa (zaidi ya 38°C au 100.4°F) kwa zaidi ya saa 24 baada ya utaratibu;

  • Maumivu makali ya nyonga yanayozidi kuongezeka; na

  • Dalili zinazoendelea za ujauzito (kama vile kichefuchefu kinachoongezeka, matiti kuwa laini, n.k.).

ATHARI ZA KAWAIDA

Ni Nini Madhara ya Utoaji Mimba wa Kliniki?

Watu wengi huhisi maumivu makali ya tumbo na kupata damu wakati wa utoaji mimba wa kliniki, hasa wakati mlango wa kizazi unafunguliwa na wakati wa taratibu zenyewe. Maumivu haya kawaida hupungua muda mfupi baada ya utoaji mimba kumalizika, lakini pia ni kawaida kuwa na maumivu ya tumbo na damu kwa siku chache au hata wiki kadhaa. Ikiwa misoprostol inatumiwa kusaidia kufungua mlango wa kizazi, inaweza kusababisha madhara kama kichefuchefu, kutapika, kuhara, homa, au baridi kali.

Ganzi ya eneo mara nyingi hutumiwa kufisha sehemu ya karibu na mlango wa kizazi. Hii husaidia kufanya taratibu kuwa za kustarehesha zaidi na kupunguza baadhi ya maumivu.

Pia ni kawaida kabisa kuhisi hisia tofauti baada ya utoaji mimba. Watu wengine huhisi ahueni, wengine huzuni, au mchanganyiko wa zote mbili. Ikiwa unahitaji msaada au mtu wa kuzungumza naye, ni sawa kabisa kuomba msaada.

NJIA ZA KUDHIBITI MAUMIVU

Je, Utoaji Mimba wa Kliniki ni Uchungu?

Doctor in white coat explains inhaler to patient in floral dress, symbolizing pain and cramping during abortion procedures.

Watu wengi huhisi maumivu ya tumbo wakati wa taratibu za utoaji mimba kwa kutumia vacuum au upasuaji. Aina ya kawaida ya maumivu ni maumivu makali ya tumbo wakati wa taratibu. Kwa wengi, maumivu hayo hupungua haraka baadaye, lakini baadhi ya watu wanaweza kupata maumivu ya tumbo mara kwa mara kwa siku chache au hata wiki kadhaa. Maumivu haya kwa kawaida husababishwa na kufunguliwa kwa mlango wa kizazi na mji wa mimba kujikunja.

Kiwango cha maumivu mtu anachohisi kinaweza kutegemea hatua ya ujauzito, uvumilivu wa maumivu wa mtu binafsi, kama tayari amewahi kujifungua, kama huwa ana maumivu makali wakati wa hedhi, na kiwango cha wasiwasi alichonacho. Kila mtu huhisi maumivu kwa namna tofauti.

Chaguo za kudhibiti maumivu zinapaswa kutolewa kila wakati. Unaweza kupewa dawa kabla au wakati wa taratibu, na pia kuchukua dawa nyumbani kwa matumizi ya baadaye ikiwa itahitajika.

Ni Aina Gani ya Ganzi Inayotumika Katika Utoaji Mimba wa Kliniki?

Kuna aina mbalimbali za ganzi zinazoweza kutumika wakati wa utoaji mimba wa kliniki, na aina gani itatumika mara nyingi hutegemea umri wa ujauzito pamoja na upatikanaji wa dawa za ganzi katika kliniki.

Njia zinazowezekana za ganzi ni pamoja na:

Ganzi ya eneo :

Hii ndiyo aina ya kawaida ya ganzi inayotumika kwa utoaji mimba wa kliniki. Ni dawa ya kufisha inayodungwa karibu na mlango wa kizazi ili kusaidia kupunguza maumivu wakati wa taratibu. Mtu hubaki akiwa macho na anajitambua kikamilifu.

Usinyaa wa wastani/Uchovu wa fahamu wa kiasi:

Hii ni ganzi inayowekwa moja kwa moja kwenye mshipa, na inapunguza- kwa kiasi kiwango cha fahamu. Mtu bado anaweza kuitikia amri kwa maneno.

Usinyaa wa kina:

Hii ni ganzi inayowekwa kwenye mshipa na hupunguza sana kiwango cha fahamu. Mtu ataweza kuitikia tu amri zinazorudiwa au msisimko wa kuguswa.

Ganzi ya jumla:

Hii inaweza kuwa mchanganyiko wa dawa za ganzi zinazovutwa au kudungwa, na humfanya mtu kupoteza fahamu kabisa. Hatakuwa anaitikia amri yoyote.

HUDUMA BAADA YA UTOAJI MIMBA

Huduma Baada ya Utoaji Mimba wa Kliniki na Mpango wa Uzazi

Baada ya utoaji mimba wa kliniki, mara nyingi mtu hutolewa nafasi ya kurudi kwa uchunguzi wa kufuatilia, ingawa si lazima, kila mtu anapaswa kufuata ushauri wa mtoa huduma wa afya.

Hakuna muda maalum uliothibitishwa kitabibu ambao mtu analazimika kusubiri kabla ya kufanya shughuli fulani kama kuoga, kufanya mazoezi, kufanya ngono, au kutumia tamponi. Kwa ujumla, inapendekezwa kwamba angalau hadi damu ipungue baada ya taratibu, mtu anapaswa: kuepuka kuingiza vitu kwenye uke ikiwa ni pamoja na tamponi na vikombe vya hedhi, na kuepuka shughuli za mwili zenye nguvu. Kila mtu anaweza kurejea kwenye shughuli zake za kawaida kulingana na jinsi mwili wake unavyoweza kustahimili, na kila mtu ni tofauti.

Kabla ya kuondoka kliniki, unapaswa kupewa taarifa kuhusu mbinu za upangaji uzazi. Aina nyingi za upangaji wa uzazi zinaweza kuanza kutumika mara moja, hata hivyo, mjadala unapaswa kufanyika kuhusu kila mtu na uchaguzi wake wa njia. Kliniki zinapaswa kuwapa watu mawasiliano kwa ajili ya maswali au wasiwasi wowote baada ya utoaji mimba.

Ili kupata mbinu za upangaji wa uzazi zinazokufaa, tembelea findmymethod.org

User questioning herself, face resting on hand, question mark above her head

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara Kuhusu Utaratibu wa Utoaji Mimba kwa Kunyonya au kufyonza.

Linapokuja suala la kutoa ujauzito, usalama ni muhimu sana. Mbinu zisizo salama za utoaji mimba ni pamoja na chochote kinachofanywa bila usaidizi ufaao wa kimatibabu, dawa zilizoidhinishwa au wataalamu waliopokea mafunzo. Mbinu hizi zinaweza kuathiri afya yako na hata kuhatarisha maisha yako.
Mbinu zisizo salama zinaweza kujumuisha:
kutumia dawa au kemikali ambazo hazijaidhinishwa kwa ajili ya utoaji mimba;
kutumia vidonge sahihi lakini bila kufuata maagizo sahihi;
kuingiza vitu ukeni au kwenye mfuko wa uzazi;
kutumia watu ambao hawajapokea mafunzo au vituo ambavyo havina leseni kwa ajili ya utoaji mimba kwa njia ya upasuaji; na
kufanyiwa upasuaji mahali ambapo si safi au hapana vifaa vya matibabu.
Mbinu salama za utoaji mimba ni pamoja na:
kutumia tembe za kutoa mimba zilizoidhinishwa kwa kufuata mwongozo sahihi, unaotegemea ushahidi; na
kufanyiwa utoaji mimba unaofanywa kwenye kliniki na mtaalamu aliyehitimu katika mazingira safi na salama.
Afya na usalama wako ni jambo muhimu, daima chagua njia na vyanzo vya kuaminika vya kutoa huduma.
Vyanzo:
1) "Abortion." WHO, 2024, www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/abortion. Accessed July 2025.

MSAADA WA USHAURI WA UTOAJI MIMBA SALAMA

Ni sahihi kuomba msaada. for Support

Taarifa tunazotoa zinazingatia ushahidi kuhusu utoaji mimba salama. Huduma yetu ya ushauri ya bure ni salama, ya faragha, rahisi, na haina unyanyapaa. Tunangojea ujumbe wako!

Reach out to safe2choose for more info via our counseling and support channels

imeandaliwa na timu ya safe2choose pamoja na msaada wa wataalamu toka carafem, kulingana na Miongozo ya Huduma ya Utoaji Mimba ya WHO ya mwaka 2022; Sasisho za Kliniki za Afya ya Uzazi za mwaka 2023 kutoka Ipas na Miongozo ya Sera za Kliniki kwa Huduma ya Utoaji Mimba ya NAF ya mwaka 2024.

safe2choose inasaidiwa na Bodi ya Ushauri wa Kitiba iliyoundwa na wataalamu wakuu katika sekta ya afya ya ngono na uzazi pamoja na haki.

carafem hutoa huduma rahisi na za kitaalamu za utoaji mimba na upangaji wa familia ili watu waweze kudhibiti idadi na mpangilio wa watoto wao.

Ipas ni shirika la kimataifa linalolenga kupanua upatikanaji wa utoaji mimba salama na huduma za uzazi wa mpango.

WHO – Shirika la Afya Duniani – ni taasisi maalum ya Umoja wa Mataifa inayohusika na afya ya umma duniani kote.

NAF – Shirika la Kitaifa la Utoaji Mimba – ni chama cha kitaalamu nchini Marekani kinachounga mkono huduma salama za utoaji mimba zinazotegemea ushahidi na haki za uzazi.

[1] "Abortion care guideline." World Health Organization, 2022, Retrieved from: srhr.org/abortioncare/.

[2] Jackson, E. "Clinical Updates in Reproductive Health." Ipas, 2023, www.ipas.org/wp-content/uploads/2023/09/Ipas-Clinical-Updates-in-Reproductive-Health-CURHE23b.pdf Accessed November 2024. Accessed November 2024.

[3] "Clinical Policy Guidelines." National Abortion Federation, 2024, Retrieved from: prochoice.org/providers/quality-standards/.

[4] "Clinical practice handbook for quality abortion care". Geneva: World Health

Organization; 2023. Licence: CC BY-NC-SA 3.0 IGO. Retrieved from: https://iris.who.int/bitstream/handle/10665/369488/9789240075207-eng.pdf?sequence=1

[5] Weitz, T. A., Taylor, D., Desai, S., Upadhyay, U. D., Waldman, J., Battistelli, M. F., & Drey, E. A. (2013). Safety of aspiration abortion performed by nurse practitioners, certified nurse midwives, and physician assistants under a California legal waiver. American Journal of Public Health, 103(3), 454-461. Retrieved from: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3673521/