Tembe ya kutoa mimba dhidi ya utoaji mimba kwa kufyonza: Ni ipi sahihi kwangu?

MA dhidi ya MVA

Katika jedwali hili, tunalinganisha tofauti kati ya utoaji wa mimba kwa kutumia tembe na utoaji mimba kwa njia ya kunyonya au kufyonza (mwongozo au electroniki) njia ya kutoa mimba.

Ni juu ya wanawake kuamua ni ipi bora kwao kulingana na bajeti yao, upatikanaji, eneo la jiografia, umri wa gestational, na chaguo la kibinafsi.

Kuchagua njia bora ya utoaji mimba

Utoaji wa Mimba wa kimatibabu (MA) au Utoaji mimba na tembe Utoaji wa mimba katika kiliniki au kwa njia ya kunyonya au kufyonza
Je! kutoa mimba kwa kutumia tembe ni nini? ( utoaji wa mimba wa kimatibabu) Je! njia ya kufyonza ni nini? (kutoa mimba katika kiliniki)
Ufafanuzi Utoaji wa mimba kwa matibabu (wakati mwingine huitwa utoaji wa mimba kwa tembe) ni njia salama sana ya kutoa mimba ambayo mwanamke hutumia tembe nyumbani kumaliza ujauzito usiohitajika.
Kuna aina mbili salama za kutoa mimba kwa matibabu: kutumia Mifepristone pamoja na Misoprostol, au kutumia Misoprostol peke yako. safe2choose inakubali njia zote hizi za utoaji mimba kwa kimatibabu kwa ujauzito wenye wiki kumi na tatu [1], na maelezo yanaweza kupatikana hapa.
Njia ya kunyonya au kufyonza (MVA) ni njia salama sana ya kutoa mimba kwa ujauzito katika trimester ya kwanza, na / au mapema trimester ya pili hadi wiki kumi na nne ya ujauzito*. (*Kikomo cha umri wa mimba kwa MVA mara nyingi hutegemea kliniki, na vile vile mtoaji wa huduma wa afya anayefanya utaratibu). [3]Upanuaji na Ukwanguaji kwa njia ya Elektroniki (EVA) ni njia salama na sawa na njia ya kunyonya au Kufyonza (MVA). EVA inaweza kutumika kwa ujauzito katika trimester ya kwanza, na / au mapema trimester ya pili. Tofauti ya msingi kati ya utoaji mimba kwa njia ya Upanuaji na Ukwanguaji kwa njia ya Elektroniki (EVA) na njia ya kunyonya au Kufyonza (MVA) ni kwamba umeme hutumiwa kuunda mumunyo la kuondoa ujauzito. Kwa sababu EVA inahitaji umeme, inaweza kuwa haipatikani kwa mipangilio ya rasilimali duni.

MVA na EVA inafanywa kwenye kliniki na mhudumu wa afya aliyefundishwa. Unaweza kupata maelezo zaidi juu ya utaratibu hapa.

Utoaji wa Mimba wa kimatibabu (MA) au Utoaji mimba na tembe Utoaji wa mimba katika kiliniki au kwa njia ya kunyonya au kufyonza
Ubaya na uzuri wa utoaji wa mimba na tembe (utoaji mimba wa kimatibabu) [1], [2] Ubaya na uzuri wa utoaji mimba kwa njia ya kunyonya au kufyoza (utaratibu wa utoaji mimba) [3], [4]
Ufanisi Asilimia 95 yenye ufanisi Asilimia 99 yenye ufanisi
Usalama Salama sana Salama sana
Kupima ujauzito Jaribio la mawimbi sauti haihitajiki Uchunguzi wa mwili unahitajika, na Jaribio la mawimbi sauti inaweza kuhitajika kulingana na kliniki.
Kikomo cha umri wa mimba Inaweza kutumika hadi wiki kumi na tatu ya ujauzito
Ili kujua juu ya umri wako wa mimba yako, tembelea ukurasa wetu ambao una Uthibitisho wa Mimba na kikokotoo.
Inaweza kutumika hadi wiki 14 ya ujauzito kwa MVA na ujauzito ya wiki 15 kwa EVA *.
( Kikomo cha umri wa ujauzito kwa kufyonza mara nyingi hutegemea kliniki, na vile vile mhuduma wa afya anayefanya utaratibu)
Ili kujua juu ya umri wako wa mimba yako, tembelea ukurasa wetu ambao una Uthibitisho wa Mimba na kikokotoo.
Mahali Inafanyika katika faragha ya nyumba au mahali popote mwanamke anahisi ako salama Inafanyika katika ofisi ya daktari, katika kliniki au hospitali.
Imetekelezwa na Inaweza kufanywa na mwanamke mwenyewe. Inaweza kutolewa kwa usalama na daktari, watendaji wa wauguzi, wakunga wa wauguzi, wasaidizi wa daktari (PA), na wengine ambao wamefunzwa vya kutosha.
Muda Wakati wa kukamilisha mimba na tembe unaweza kuwa siku chache hadi wiki chache. Wakati wa kukamilisha Kufyonza ni madakika.
Madhara Damu yaweza kuwa yatoka na kupotea wakati wa kutokwa na damu kwa wiki mbili au zaidi.
Kukandamizwa kwa tumbo la uzazi kunaweza kuja na kupotea kwa mda wa wiki mbili
Kuvujadamu kunaweza kudumu kutoka kwa wiki ya kwanza hadi ya pili.
Kukandamiza kwa tumbo kunaweza kuja na kupotea kwa mda wa wiki moja hadi mbili.
Shida/hatari Uwezekano wa hatari ni pamoja na: kutokwa na damu nyingi, maambukizi, kuendelea kwa ujauzito, na utoaji mimba usio kamili. Uwezekano wa hatari ni pamoja na: kutokwa na damu nyingi, maambukizi, kujeruhiwa kwa mfuko wa uzazi na miundo iliyo karibu, utoaji mimba usio kamilika, kuendelea kwa ujauzito.
Gharama Kwa ujumla, utoaji mimba na tembe sio bei ghali kuliko utoaji wa mimba kwa kunyonya au kufyonza kwa sababu inajumuisha ununuzi wa tembe tu.Jaribio la mawimbi sauti, ambalo linaweza kuwa na gharama kubwa, halihitajiki. Gharama halisi ya MA itatofautiana sana kulingana na eneo la jiografia na ikiwa tembe zinapatikana au karibu na duka la dawa, au kwa maagizo tu. Kawaida, njia za kufyonza (utoaji wa mimba kliniki) zinakuwa ghali zaidi kuliko utoaji mimba kwa matibabu kwa sababu wakati mwingine inahitaji uchunguzi wa ziada (yaani Jaribio la mawimbi sauti) na mtaalamu mwenye ujuzi wa kufanya utaratibu. Gharama halisi ya njia ya kufyonza itatofautiana sana kulingana na eneo la jiografia na sheria husika zinazohusiana na utoaji mimba.
Huduma ya baada ya utoaji wa mimba Kufuatilia katika kliniki wakati mwingine kunapendekezwa kuthibitisha mafanikio ya utoaji mimba wa kimatibabu.
Wanawake wanapaswa kuwasiliana na kliniki yao ikiwa wanapata: kutokwa na damu nyingi, homa, maumivu makali, dalili za kuambukizwa au kuendelea kwa ujauzito.
Matokeo ya upimaji wa mimba kwa mkojo yatakuwa hasi wiki nne hadi wiki sita-6 baada ya mafanikio ya MA.
Kwa ujumla, wanawake wanaweza kurudi kwenye shughuli zao za kawaida kama inavyostahimiliwa baada ya MA.
Unaweza kupata maelezo zaidi juu huduma ya baada ya utoaji wa mimba hapa.
Kufuatilia wakati mwingine hutolewa baada ya utoaji mimba katika kliniki, lakini hauhitajiki.
Wanawake wanapaswa kuwasiliana na kliniki yao ikiwa wanapata: kutokwa na damu nyingi, homa, maumivu makali, dalili za kuambukizwa au kuendelea kwa ujauzito.
Matokeo ya upimaji wa mimba kwa mkojo yatakuwa hasi baada ya wiki mbili au tatu baada ya utaratibu.
Kwa ujumla, wanawake wanaweza kurudi kwenye shughuli zao za kawaida kama inavyostahimiliwa baada ya utoaji mimba katika kliniki
Unaweza kupata maelezo zaidi juu ya huduma ya baada ya utoaji wa mimba baada ya njia ya kunyonya au kufyonza hapa.
Utunzaji wa uzazi Njia nyingi za upangaji uzazi zinaweza kuanza mara moja baada ya utoaji wa mimba wa kimatibabu, isipokuwa machache ya kuwa pete ya uke na IUD.
Kupata njia sahihi za upangaji uzazi kwa changuo lako, tembelea www.findmymethod.org
Njia zote za upangaji uzazi zinaweza kuanza mara baada ya utaratibu wa kutoa mimba kwa njia ya kunyonya au kufyonza.
Kupata njia sahihi za upangaji uzazi kwa changuo lako, tembelea www.findmymethod.org

Waandishi:

timu ya safe2choose na wataalam wanaounga mkono carafem, kwa kuzingatia mapendekezo ya 2020 na shirika la Kitaifa aa Utoaji wa Mimba (NAF), mapendekezo ya mwaka wa 2019 na Ipas, na mapendekezo ya mwaka wa 2012 yaliyotolewa na shirika la Afya Ulimwenguni.

Shirikisho la Kuavya mimba ni chama cha wataalamu wa wahudumu wa afya ndani ya Amerika Kaskazini.

carafem hutoa huduma bora na ya kitaalam ya utoaji wa mimba na upangaji wa uzazi ili watu waweze kudhibiti idadi na nafasi za watoto wao.

Ipas ndio shirika la pekee la kimataifa ambalo limedhamiria tu katika kupanua ufikiaji wa kutoa mimba kwa njia salama na utunzaji wa uzazi.

Shirika la Afya Ulimwengini ni chombo maalum cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na afya ya umma ya kimataifa.

[1] National Abortion Federation (NAF). Clinical Policy Guidelines for Abortion Care. 2020. Retrieved from: https://5aa1b2xfmfh2e2mk03kk8rsx-wpengine.netdna-ssl.com/wp-content/uploads/2020_cpgs_final.pdf

[2] Gynuity. Providing medical abortion in low-resource settings An Introductory Guidebook. Second Edition. 2009. Retrieved from: https://gynuity.org/assets/resources/clinguide_maguide2nd_edition_en.pdf

[3] World Health Organization (WHO). Safe abortion: technical and policy guidance for health systems, second edition. 2012. Retrieved from: https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/70914/9789241548434_eng.pdf;jsessionid=F77B761669FC579124C1E9CA2CC3CFDB?sequence=1

[4] Ipas. Clinical Updates in Reproductive Health. 2019. Retrieved from: https://www.ipas.org/wp-content/uploads/2023/09/Ipas-Clinical-Updates-in-Reproductive-Health-CURHE23b.pdf

Chaguzi za Utoaji Mimba Salama kwa kutumia Tembe