
Utoaji Mimba Nchini Kenya
Jifunze kuhusu utoaji mimba Kenya: hali ya kisheria, njia salama (vidonge na upasuaji), gharama, na changamoto za upatikanaji.
Baada ya kuthibitisha uwepo wa mimba na kabla ya kufanya uamuzi wa kuitoa, ni muhimu kujua umri wa mimba – muda wa ujauzito kwa wiki.
Tuko hapa kukusaidia katika mchakato huu.
safe2choose, tunatoa taarifa kamili na msaada ili kukusaidia kupitia safari yako ya kutoa mimba. Rasilimali zetu zimeundwa kukuwezesha kupata maarifa na kujiamini ili kufanya uchaguzi bora kutegemeana na hali yako.
Uthibitisho
Iwe umeamua kuendelea kubeba mimba au kuitoa, kuthibitisha umri wa mimba yako ni muhimu kwa sababu zifuatazo:
Kuthibitisha ujauzito wako na kujua umri wake husaidia kufanya maamuzi sahihi na kujipanga vyema.
Njia za utoaji mimba hupendekezwa kutegemeana na hatua ya ujauzito. Kufahamu idadi ya wiki za ujauzito kutasaidia kubaini njia salama na bora zaidi ya kutumia.
Upatikanaji wa huduma za utoaji mimba hauna usawa duniani kote. Katika baadhi ya nchi na maeneo, utoaji mimba unaruhusiwa lakini unakabiliwa na vikwazo vya umri wa ujauzito, kwani baadhi ya mbinu za utoaji mimba zinapatikana tu katika wiki fulani za ujauzito.
Kuwa na taarifa sahihi husaidia kupunguza wasiwasi na kukuandaa kihisia kwa hatua zinazo fuata.
Upimaji mimba wa kuaminika
Ingawa kukosa hedhi mara nyingi huashiria ujauzito, sababu nyingine mbali na ujauzito zinaweza kuchelewesha hedhi au kupoteza kabisa. Ndiyo maana unapaswa kuthibitisha ujauzito kwa kutumia kipimo cha kuaminika cha ujauzito kabla ya kutumia kikokotoo cha ujauzito. Kipimo cha ujauzito nyumbani au kumwona mtoa huduma wa afya kunaweza kukupa taarifa sahihi unazohitaji.
Hupaswi kutumia vidonge vya kutoa mimba ikiwa hujathibitisha ujauzito kwa kipimo cha kuaminika na hujui ujauzito umefikisha wiki ngapi.
Ni muda gani?
Ili kupata idadi ya wiki za ujauzito, hesabu idadi ya wiki na siku ukianzia siku ya kwanza ya hedhi yako ya mwisho (LMP). Ni muhimu kuanza kuhesabu kuanzia siku hiyo kwa sababu inasaidia kutathmini wakati yai lilipotolewa na kurutubishwa.
Jua tarehe kamili ya mwanzo wa hedhi yako ya mwisho;
Kadiria tarehe inayokaribia ikiwa hukumbuki siku kamili ya LMP yako;
Tumia njia nyingine ikiwa hukumbuki mwezi au kama ilikuwa mwanzoni au mwishoni mwa mwezi.
kuanzia ulipokosa hedhi yako;
kuanzia siku ya tendo la ndoa;
kuanzia siku unayodhani ulishika mimba.
Ikiwa unahitaji msaada wa kuhesabu wiki za ujauzito, tumia kikokotoo chetu cha ujauzito. Chagua siku ya kwanza ya hedhi yako ya mwisho, kisha anza.
Jinsi ya kutumia kikokotoo cha mimba
Njia za utoaji mimba
Zipo njia kadhaa salama za utoaji mimba, njia utakayo chagua mara nyingi hutegemeana na umri wa ujauzito. Wakati mwingine, njia zaidi ya moja zaweza tumika kwa mara moja. Pia chaguo lako linaweza kuathiriwa na mahali unapoishi, vifaa au rasilimali zinazopatikana, na kile unachopendelea au kile daktari wako alicho pendekeza.
Utoaji mimba kwa vidonge au utoaji mimba wa kitabibu (MA) unaweza kufanyika salama nyumbani kwa mimba zenye chini ya wiki 13. Kwa mimba yenye zaidi ya wiki 13, tahadhari kubwa inahitajika na inashauriwa utoaji mimba ufanyike katika kituo cha matibabu.
Njia ya Kunyonya au Kufyonza (MVA) ni njia ya kutoa maudhui ya mfuko wa uzazi inayotumika kwa mimba zenye umri wa hadi wiki 14 na hufanywa na mtaalamu wa huduma za afya katika kliniki au kituo cha matibabu.
Upanuaji na ukwanguaji kwa njia ya electoniki (EVA) ni njia nyingine ya kutoa maudhui ya mfuko wa uzazi, inayotumika kwa mimba zenye umri wa hadi wiki 15, pia hufanywa na mtaalamu wa huduma za afya katika mazingira ya kliniki.
Njia ya upanuaji na ukwanguaji (D&E) kwa kawaida, hutumika kwa mimba zenye zaidi ya wiki 14. Huendeshwa na mtaalamu kwenye kliniki au kituo cha afya.
Kutishia mimba, kwa kawaida njia hii hutumika kwa ujauzito wenye zaidi ya wiki 16 na hufanywa na mtaalamu wa huduma za afya kwenye kliniki au hospitali.
Usafishaji wa kizazi (D&C) ni njia ya kizamani ya utoaji mimba ambayo kwa sasa imepitwa na wakati baada ya kugundulika kwa njia salama zaidi kama vile MVA, EVA, na D&E (1)(5). Ingawa bado inatumika katika baadhi ya maeneo, mbinu salama zinapendekezwa zaidi.
Kikokotoo cha ujauzito kinaweza kutoa makadirio muhimu ya umri wa ujauzito wako, lakini si kila mara huwa sahihi kabisa. Hufanya kazi vyema unapoweka taarifa sahihi, kama vile tarehe ya kwanza ya hedhi yako ya mwisho. Ikiwa hedhi zako si za kawaida au huna uhakika na tarehe, matokeo yanaweza yasiwe ya kuaminika sana. Bado, inaweza kukupa wazo la jumla la umri wa ujauzito wako, ambalo linaweza kusaidia kukuongoza kuelekea chaguo zinazofaa za utoaji mimba. Ikiwa huna uhakika, ni wazo nzuri kuchunguza njia nyingine za kubaini umri wako wa ujauzito. Wasiliana nasi ikiwa unahitaji usaidizi.
Habari za hivi punde na makala za blogu
Pata taarifa za hivi punde, habari, na maarifa ukiwa na safe2choose. Yaani taarifa kuhusu maendeleo ya afya ya uzazi, matangazo muhimu na hadithi kutoka kwa jamii yetu, Ukurasa wetu wa Makala unakuhabarisha na kufanya uendelee kushiriki katika taarifa mpya.
Wasiliana nasi
Ikiwa haupati kile unachotafuta au unahitaji msaada zaidi, tafadhali wasiliana nasi kupitia ukurasa wa ushauri au kwa kutumia njia nyingine zinazopatikana. Tunaweza kujibu maswali yako kuhusu ujauzito, njia za kutoa mimba, au huduma baada ya kutoa mimba – wasiliana nasi!
