Tunaunganisha wanawake kila mahali kwa habari sahihi na iliyoundwa juu ya chaguzi salama za utoaji mimba, ili waweze kutoa mimba salama wapi, lini, na nani wanahisi kuwa wako salama zaidi nao.
Habari ya Utoaji Mimba Salama – Pata Kujua Zaidi
Asilimia Arubaini (40%) ya ujauzito ulimwenguni haujapangwa [1]. Wanawake kote ulimwenguni wana ujauzito usiohitajika na kwa sababu tofauti, wanaweza kuamua kutoa mimba. Wanawake wote, bila kujali rangi, tabaka, dini au jiografia wanastahili kupata kufikia njia za kutoa mimba kwa njia salama.
Tunatoa habari sahihi juu ya chaguzi salama za utoaji mimba.
Pata Huduma ya Kutoa Mimba
Jifunze zaidi juu ya jinsi ya kutoa mimba na tembe au utoaji-mimba wa kliniki. washauri wa safe2choose wanaweza kukuongoza kupitia chaguzi hizi zote na kukuunganisha kwa wasaidizi ndani ya nchi yako na rasilimali za karibu
Jifunze na Shiriki Habari salama za utoaji mimba
Unapojua zaidi juu ya utoaji mimba, ndivyo utakavyojiandaa zaidi. Pata maelezo zaidi kuhusu sheria ya utoaji mimba katika nchi yako, ushuhuda juu ya uzoefu wa utoaji mimba kutoka ulimwenguni kote, na pakua rasilimali za matibabu ili kutoa mimba salama.
Hapa kuna maswali masita ya juu zaidi yanayoulizwa juu ya utoaji mimba.
Ikiwa una maswali juu ya tembe za kutoa mimba, utoaji mimba kwa kufyonza, utoaji mimba wa upasuaji, au utunzaji wa baada ya kutoa mimba, unaweza kuangalia sehemu yetu ya Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara (FAQs). Ikiwa hautapata kile unachotafuta au unahitaji habari zaidi, tafadhali wasiliana na mmoja wa washauri wetu waliofundishwa kwa lugha nyingi kupitia ukurasa wa ushauri. Tuko hapa kukusaidia kwa kutoa habari salama ya utoaji mimba inayokidhi mahitaji yako.
Je! Utoaji mimba ni salama?
Utoaji mimba ni moja wapo ya taratibu salama za matibabu wakati itifaki sahihi zinafuatwa katika mazingira salama. Kuna hatari chini ya asilimia moja (1%) ya kuwa na shida ya matibabu, na shida zinasimamiwa kwa urahisi na msaada sahihi. [2]
Je! Chaguo gani la kutoa mimba ni sawa kwangu?
Chaguzi za utoaji mimba zinazopatikana zitategemea umri wako wa umri wa ujauzito wako. Hesabu umri wa ujauzito wako ukitumia kikokotozi cha Mimba, na kisha unaweza kuamua njia inayofaa zaidi. Utahitaji pia kuzingatia sheria ya nchi yako na upatikanaji wa njia hii, bajeti yako na upendeleo wako wa kibinafsi. Tembelea ukurasa wetu wa utoaji mimba na tembe dhidi ya utoaji mimba kwa Njia ya Kunyonya au Kufyonza au ukurasa wetu wa utoaji mimba ya upasuaji ili ujifunze zaidi kuhusu njia hizi.
Je! Utoaji mimba hugharimu pesa gani?
Bei ya utoaji mimba hutofautiana sana katika maeneo na inategemea ni njia gani unayoamua kufuata. Tuna habari za kina kwa nchi nyingi. Angalia ukurasa wetu wa Habari ya Utoaji Mimba kwa Kila Nchi na ukurasa wetu wa Chapa za Tembe za Kutoa Mimba ya Kimatibabu ili ujifunze zaidi juu ya kile kinachopatikana kwako.
Je! Kutoa Mimba Kunaumiza?
Inategemea njia ya kutoa mimba unayochagua. Utoaji mimba na tembe unafanya hedhi kuwa nzito ambayo inaweza kusimamiwa na Ibuprofen. Utoaji mimba kwa njia ya Kunyonya au Kufyonza kwa ujumla hufanywa chini ya dawa ya kukufisha nganzi ya ndani. Soma zaidi juu ya tofauti kwenye ukurasa wetu Utoaji wa mimba na tembe dhidi ya utoaji mimba kwa njia ya Kunyonya au Kufyonza ili kuongoza chaguo lako.
Je! Ninaweza Kupata Mimba tena Baada ya Kutoa Mimba?
Bila kujali njia hiyo, utoaji mimba salama hautaathiri uzazi wako wa baadaye, na unaweza kupata ujazito tena. Mzunguko wakowa hedhi unaweza kuanza mara tu baada ya siku Nane baada ya kutoa mimba. Ni muhimu kuanza njia ya upangaji uzazi ikiwa hautaki kuwa mjamzito tena. Sikiza mwili wako, na uamue kinachokufaa. [3]
Njia ipi ni bora kwangu?
Kwa kuelewa tofauti ya kiufundi kati ya njia tofauti za utoaji mimba salama, ni wewe tu unaweza kufanya uamuzi bora kwako mwenyewe. Unaweza kusoma juu ya njia kuu mbili za utoaji mimba chini ya wiki 13 kwenye Kutoa Mimba na tembe dhidi ya ukurasa wa Utoaji kwa ya Kunyonya au Kufyonza, na unaweza kuwasiliana na washauri wetu ambao watasaidia uamuzi wako bila kukuhukumu. [3]
[1] Guttmacher Institute. (2020) Unintended Pregnancy and Abortion Worldwide. Imechukuliwa kutoka: https://www.guttmacher.org/fact-sheet/induced-abortion-worldwide
[2] World Health Organization. (2012) Safe abortion: technical and policy guidance for health systems. Imechukuliwa kutoka: https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/70914/;jsessionid=AB2B02D2E41FB4F6CF95B5F59B0A9AF4?sequence=1
[3] Ipas. (2020). Clinical Updates in Reproductive Health. L. Castleman & N. Kapp (Eds.). Chapel Hill, NC: Ipas. Imechukuliwa kutoka: https://www.ipas.org/wp-content/uploads/2020/08/ClinicalUpdatesInReproductiveHealthCURHE20-English-digital.pdf