Huduma Salama ya Utoaji Mimba: Tembe na Chaguzi za Kliniki
Tunatambua kuwa kufanya chaguzi za utoaji mimba kunaweza kukufanya uhisi kuchanganyikiwa na kushindwa, lakini hauko peke yako. Sisi safe2choose, tuko hapa kwa ajili yako. Kwenye tovuti yetu, utapata taarifa sahihi na za kuaminika kuhusu njia salama za utoaji mimba, kama vile kutumia tembe za utoaji mimba au chaguzi za kliniki. Timu yetu yenye uzoefu wa ushauri nasaha iko tayari kukusikiliza, kujibu maswali yako, na kusaidia kupata huduma salama na za kuaminika zilizo karibu nawe. Unastahili msaada, na tuko hapa kukusaidia ili uweze kufanya uamuzi unaokufaa, kwa ujasiri na uangalifu.
NINI CHA KUJUA KWANZA
Je, Utoaji Mimba Ni Salama Kwangu?
Utoaji mimba ni salama sana unapofanywa kwa kutumia njia sahihi, katika mazingira sahihi, na ukiwa na maarifa sahihi.
Kabla ya kuanza mchakato wa utoaji mimba, unapaswa kujua umri wa mimba ili uweze kuchagua njia inayokufaa zaidi. Unaweza kutumia Kikokotoo chetu cha Ujauzito ili kujua hilo. Kuna vizuizi vya kiafya unavyopaswa kuvifahamu ambavyo vinaweza kuathiri chaguo lako. Washauri wetu wako tayari kukupa mwongozo na taarifa kulingana na hali yako binafsi.
Kikokotoo cha mimba
Ikiwa unahitaji msaada wa kuhesabu wiki za ujauzito, tumia kikokotoo chetu cha ujauzito. Chagua siku ya kwanza ya hedhi yako ya mwisho, kisha anza.
Jinsi ya kutumia kikokotoo cha mimba
UTOAJI MIMBA KWA NJIA YA TEMBE
Utoaji Mimba kwa Tembe: Chaguo Salama na Binafsi
Utoaji mimba kwa tembe ni njia rahisi sana ya utoaji mimba inayotumia aina mbili za tembe (mifepristone na misoprostol) au aina moja tu ya tembe (misoprostol). Tembe hizi husababisha kizazi kujikunja na kutoa mimba kwa namna inayofanana na mchakato wa hedhi. Mchakato huu unaweza kuchukua siku chache hadi wiki kadhaa na unaweza kufanyika nyumbani.
Hapa safe2choose, tunawaunga mkono watu wanaotaka kufanya utoaji mimba kwa kutumia vidonge wakiwa nyumbani kwa kuwapa taarifa sahihi na rasilimali kuhusu mchakato huu.
Chaguzi za utoaji mimba salama kwa tembe
Utoaji mimba kwa mifepristone na misoprostol
Utoaji mimba kwa misoprostol pekee
Aina za tembe za utoaji mimba na chapa za tembe za utoaji mimba wa kitabibu
Taarifa za utoaji mimba kwa kila nchi
Maswali yanayouliwa mara kwa mara
Tembe ya utoaji mimba dhidi ya utoaji mimba kwa njia ya kunyonya
KUTOA MIMBA KATIKA KLINIKI
Taratibu za Utoaji Mimba Kliniki
Utoaji mimba kliniki unajumuisha utoaji mimba wa kitabibu na wa upasuaji unaosimamiwa na mtaalamu, pamoja na njia ya kunyonya na usimamizi wa mimba iliyoharibika. Kawaida hufanyika kwa mtoa huduma, kliniki au hospitali kulingana na sheria za nchi husika. Kwa kawaida,haina maumivu kwani hufanyika kwa kutumia ganzi sehemu ya mwili au ya mwili mzima, na huduma huchukua dakika chache tu.
Iwapo hii ndiyo njia inayokufaa zaidi kulingana na hali yako, wasiliana na washauri wetu ili tuweze kukuunganisha moja kwa moja na watoa huduma wa kuaminika waliopo karibu nawe.
Habari za hivi punde na makala za blogu
Endelea kupata taarifa toka safe2choose
Pata taarifa za hivi punde, habari, na maarifa ukiwa na safe2choose. Yaani taarifa kuhusu maendeleo ya afya ya uzazi, matangazo muhimu na hadithi kutoka kwa jamii yetu, Ukurasa wetu wa Makala unakuhabarisha na kufanya uendelee kushiriki katika taarifa mpya.
WASILIANA NASI
Wasiliana na Washauri Wetu wa Utoaji Mimba kwa Msaada wa Bure
Kama hukupata unachotafuta au unahitaji msaada zaidi, tafadhali wasiliana nasi kupitia ukurasa wa ushauri na njia nyingine zilizopo. Tunaweza kukusaidia kujibu maswali yako kuhusu ujauzito, chaguzi za utoaji mimba, au huduma za baada ya utoaji mimba – wasiliana nasi!
imeandaliwa na timu ya safe2choose pamoja na msaada wa wataalamu toka carafem, kulingana na Miongozo ya Huduma ya Utoaji Mimba ya WHO ya mwaka 2022; Sasisho za Kliniki za Afya ya Uzazi za mwaka 2023 kutoka Ipas na Miongozo ya Sera za Kliniki kwa Huduma ya Utoaji Mimba ya NAF ya mwaka 2024.
safe2choose inaungwa mkono na Bodi ya Ushauri ya Matibabu, inayoundwa na wataalamu wakuu wa Afya ya Uzazi na Haki za Uzazi (SRHR).
carafem inatoa huduma za utoaji mimba na uzazi wa mpango kwa njia rahisi na za kitaalamu ili watu waweze kudhibiti idadi na muda wa kupata watoto.
Ipas ni shirika la kimataifa linalolenga kuongeza upatikanaji wa huduma salama za utoaji mimba na kinga ya uzazi.
WHO ni shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na Afya ya umma duniani.
NAF ni shirika la kitaalamu nchini Marekani linalounga mkono huduma salama za utoaji mimba zinazozingatia ushahidi na haki za uzazi.
[1] "Abortion care guideline." World Health Organization, 2022, SRHR Abortion Care. Accessed November 2024.
[2] Jackson, E. "Clinical Updates in Reproductive Health." Ipas, 2023, Ipas Clinical Updates in Reproductive Health CURHE23b. Accessed November 2024.
[3]"Clinical Policy Guidelines." National Abortion Federation, 2024, Prochoice Providers Quality Standards. Accessed November 2024.
