
Utoaji Mimba Nchini Kenya
Jifunze kuhusu utoaji mimba Kenya: hali ya kisheria, njia salama (vidonge na upasuaji), gharama, na changamoto za upatikanaji.
Kutoa mimba kwa njia ya kifamasia hujulikana sana kama kutoa mimba kwa tembe. Watu wengine pia huiita njia hii kuwa ni utoaji mimba wa kujisimamia, kujifanyia au kujitegemea.
Ukichagua kutumia tembe za kutoa mimba,utapitia hali ya kutokwa na damu na maumivu ya tumbo. Dalili hizi hufanana sana na zile za hedhi ya kawaida au kuharibika kwa mimba kwa njia ya asili (mimba kutoka yenyewe).
Neno "tembe za kutoa mimba" kwa kawaida humaanisha matumizi ya mifepristone na misoprostol kwa pamoja, au misoprostol pekee.
DAWA ZA KUTOA MIMBA
Mifepristone ni dawa inayozuia mtiririko wa progesterone – homoni inayosaidia mimba kukua. Bila progesterone, mimba haiwezi kukua.
Mifepristone pia hulegeza kizazi (sehemu ya chini ya mfuko wa mimba), ambayo huongeza athari za misoprostol.
Mifepristone peke yake haitoshi kusababisha utoaji mimba; ili kukamilisha utoaji mimba, dawa ya misoprostol huhitajika pia.
Mifepristone hutumika hasa kwa shughuli ya utoaji mimba, hivyo kulingana na sheria na vikwazo, ni vigumu kupatikana katika kila nchi.
Misoprostol ni dawa ambayo husababisha mfuko wa uzazi kusogea au kushindwa kwa misuli yake (kujikunja), jambo ambalo husaidia kutoa mimba kwa kusababisha maumivu ya tumbo na kuvuja damu.
Utoaji mimba kwa kutumia njia ya kifamasia unaweza kufanyika kwa kutumia misoprostol bila mifepristone, lakini njia bora zaidi na yenye ufanisi ni kutumia dawa zote mbili pamoja.
Misoprostol pia hutumika kwa madhumuni mengine ya kitabibu kama kuchochea uchungu wakati wa kujifungua, kuzuia damu nyingi baada ya kujifungua, vidonda vya tumbo, n.k.), hivyo kwa kawaida hupatikana kwa urahisi zaidi.
Kutumia mifepristone na misoprostol kukomesha ujauzito hakuathiri ujauzito wa siku zijazo au kusababisha kuzaliwa kwa mtoto mwenye kasoro hapo baadaye. Dawa hizi zinaondolewa haraka kutoka kwa mwili na hazina madhara ya kudumu juu ya uwezo wa kuzaa au afya ya uzazi, na mimba ya siku za usoni itakua kwa kawaida. Ikiwa unapanga kuwa mjamzito tena, ni salama kufanya hivyo wakati wowote unapohisi kuwa tayari.
Habari za hivi punde na makala za blogu
Pata taarifa za hivi punde, habari, na maarifa ukiwa na safe2choose. Yaani taarifa kuhusu maendeleo ya afya ya uzazi, matangazo muhimu na hadithi kutoka kwa jamii yetu, Ukurasa wetu wa Makala unakuhabarisha na kufanya uendelee kushiriki katika taarifa mpya.
MAWASILIANO NA MSAADA
Tunatoa taarifa zenye ushahidi kuhusu utoaji salama wa mimba. Huduma yetu ya ushauri ni salama, ya siri, rahisi, na isiyo na hukumu yoyote. Tunangojea ujumbe wako!

Na timu ya safe2choose na wataalamu wanaosaidia kutoka carafem, kwa kuzingatia Mwongozo wa Huduma Salama za Utoaji Mimba wa mwaka 2022 wa WHO, Sasisho za Kliniki za Afya ya Uzazi za mwaka 2023 kutoka Ipas, na Mwongozo wa Sera za Kliniki za Huduma za Utoaji Mimba wa mwaka 2024 wa NAF.
safe2choose inasaidiwa na Bodi ya Ushauri wa Kitiba iliyoundwa na wataalamu wakuu katika sekta ya afya ya ngono na uzazi pamoja na haki.
carafem hutoa huduma za utoaji mimba salama na za kitaalamu pamoja na mipango ya uzazi ili watu waweze kudhibiti idadi na muda wa kuzaliwa kwa watoto wao.
Ipas ni shirika la kimataifa linalolenga kupanua upatikanaji wa huduma salama za utoaji mimba na huduma za uzazi wa mpango.
WHO – Shirika la Afya Duniani – ni taasisi maalum ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia afya ya umma duniani kote.
NAF – Shirika la Kitaifa la Utoaji Mimba – ni chama cha wataalamu nchini Marekani kinachounga mkono huduma salama, zinazotegemea ushahidi za utoaji mimba na haki za uzazi.