Utoaji mimba ni mojawapi ya huduma muhimu kwa wanawake hasa walio na hitaji la kuavya mimba kwa sababu ya afya ama kwa chaguzi. Hata hivyo, idadi kubwa ya wanawake wanaotoa mimba chini Kenya hafariki kila Mwaka kutokana na utoaji mimba kwa njia zisizo salama. Njia mwafaka na salama zinapatikana kuwasaidia wanawake kuavya mimba lakini tatizo kubwa ni upatikanaji kwa kila anayehitaji na gharama kubwa ya huduma. Kadhalika, kwa miaka mingi utoaji mimba nchini Kenya ulikuwa haramu, hali iliyoleta woga wa kuavya mimba na wataalamu kutoa huduma hii kwa vituo kwa afya kuhofia kukamatwa kwa mujibu wa sheria.
Katiba ya Mwaka 2010 ilipopitishwa, kipengele cha utoaji mimba kiliruhusiwa katika hali ambapo maisha au afya ya mama yako hatarini. Hata hivo, huduma hizi haziajatolewa kwa vituo vya afya kutokana na mada ya woga, kimya na unyanyapaa. Hali hii imesababisha pengo kubwa kati ya sheria na uhalisia wa maisha ya wanawake wengi, hususan wale wa vijijini na wa kipato cha chini. Kulingana ripoti ya Center for Reproductive zinaonyesha kila wiki wanawake 23 hufariki kutokana na utoaji mimba usio wa kitaalamu na matatizo yanayotokana na utoaji mimba usio salama na idadi hii ina uwezekano wa kuwa juu kulingana na wanaharakati.
Kutokana na vikwazo vilivyowekwa na sheria na hali iliyopo kuhusu utoaji wa mimba, wanawake na wasichana wengi hupendelea kutumia njia za usiri na za kiasili ambazo mwishowe ni salama. Makala haya yanaangazia njia salama za utoaji mimba zinazopatikana nchini Kenya, bei na gharama yake na changamoto za kupata huduma ya kutoa mimba.
Mbinu za Utoaji Mimba Nchini Kenya: Mwongozo wa Kuelewa Chaguzi Zako
Huduma ya utoaji mimba inaweza kufanyika kwa njia mbalimbali kilingana na mud awa ujauzito na hali ya afya ya mwanamke. Mbinu kuu zinazotumika ni matibabu ya kutumia dawa na upasuaji. Mbinu hizi ingawaje zinahitaji kufanyika kwa usalama katika vituo na wauguzi wa huduma za kitaalamu.
Utoaji Mimba kwa Matibabu (Medical Abortion)
Mbinu ya matibabu ni maarufu na faafu kwa ujauzito wa hadi wiki 10-12. Huduma hii inajumuisha matumizi ya dawa mbili za mifepristone na misoprostol. Mifepristone inafanya kazi kwa kuzuia uzalishaji wa homoni ya progesterone kwa mwili wa mwanamke ambayo ni muhimu kwa kuendelea kwa mimba. Misoprostol nayo husababisha uterasi kunyoosha na kutoa mimba.
Idadi kubwa ya mimba inayotolewa katika kliniki na wahudumu wa afya hutumia njia ya dawa. Hasa mbinu hii inatumika kwa sababu ya ufanisi wake ikiripotiwa kwamba asilimia 95 ya utoaji mimba hufanikishwa kwa usahihi. Vile vile, mbinu hii inawezesha wanawake kufhadili utoaji mimba kwa bei nafuu ikilinganishwa na mbinu zingine kwa mfano ya upasuaji.
Wanawake wanaweza kutumia dawa hizi kibinafsi wakifuata maelekezo sahihi, lakini ni muhimu kuwa na msaada wa mtaalamu kwa ajili ya ushauri na ufuatiliaji wa afya ili kuepuka matatizo kama maambukizi au damu kuvuja kupita kiasi. safe2choose hutoa mwongozo na usaidizi kwa wanawake wanaohitaji kutoa mimba kuptia wafahili walio na tajriba katika maswala haya. Pata wafadhili kwa kutembelea safe2choose ili kupata usaidizi.
Utoaji Mimba kwa Upasuaji (Surgical Abortion)
Mbinu ya upasuaji hutumika zaidi kwa kutoa ujauzito uliozidi wiki 12 na wakati ambapo mibnu ya kutumia dawa haijafanya kazi. Upasuaji unajumuisha mbinu kadhaa:
Manual vacuum Aspiration (MVA)-Ili kufanikisha mbinu hii, mfumo wa kwanza na maarufu manual vacuum Aspiration ambao hutumika sana wakati mimba iliyofika wiki 14. Mhudumu hutumia kifaa kinachonyonya mimba kutoka kwa uterasi na linawezwa kufanikishwa kwa muda wa dakika 5-10. Kulingana na
Shirika la Afya duniani(WHO), MVA imedhimishwa kama mbinu salama na ya gharama nafuu. Ni mbinu inayotumika nchini Kenya katika kiliniki nyingi za afya za umma vile vile kwa mashirika yasiyo ya kiserikali.
Kunyonya kwa Umeme/ Electric Vacuum Aspiration (EVA) – Mbinu hii hutumia machine ya umeme kunyonya yaliyomo kwa uterasi hasa kwa mimba ya mapema hadi wiki 12-14. Mbinu hii inatumika katika vituo vya afya kwa kuwa inahitaji vifaa kamili. Tofauti kubwa kati ya mbinu hizi ni Manual Vacuum Aspiration (MVA) hutumia kifaa cha mkono ilhali EVA hutegemea mashine ya umeme kutoa nguvu ya kuvuta. Vilievile, EVA ni salama na mbinu ya haraka inapofanywa na mtaalamu wa afya.
Upanuzi na Uondoaji- Dilation and Evacuation (D&E)- Ili kutoa mimba iiyozidi wiki 13, ya D&E hutumika kwa kuwa ni salama kwa mimba iliyokomaa. Ili kufanikishwa, huduma hii inahitaji maandalizi na matayarisho ya awali yanayofanywa na mtaalamu. Utaratibu wake huanza na mdomo wa mji wa mimba kisha kuondoa mimba kwa umakini kutumia vifaa vya matibabu. D&E ni moja ya mbinu salama zaidi kwa utoaji wa mimba iliyofika wiki 13, lakini inapatikana kwa kiwango kidogo nchini Kenya kutokana na ukosefu wa wataalamu na vifaa.
Upanuzi na Usafishaji- Dilation and Curettage (D&C)- mbinu hii inaangazia utaratibu uliotumika zamani ingawaje inatumika katika maeneo tofauti. Vilevile D&C hutumika kusafisha uterasi baada ya mimba iliyoharibika yenyewe au utoaji wa mimba usiokamilika. Utaratinu wake huanza ha kupanua mlango wa mji wa mimba kisha kifaa maalum maarufu kama curette hutumika kukwangua kuta za uterasi na kuchuja mabaki ya mimba. Mbinu hii haijathibitishwa kuwa salama bali imeidhimishwa kufanywa na mtaalamu pale ambapo mbinu zilizotajwa hazipatikani.
Mbinu zisizo salama
Ingawa mbinu tofauti za utoaji mimba zinapatikana nchini Kenya, ni dhahiri kwamba hazipatikani kwa kila mmoja kutokana na bei, sehemu na sababu ya usiri kwa wanawake. Vilevile hali ya unyanyapaa uliopo katika kutoa mimba, wanawake wengine huchagua mbinu za kiasili ama wanazoweza kutumia ili kutoa mimba. Kulingana na ripoti ya Shirika la Afya Duniani ya mwaka 2022, utoaji mimba usio salama husababisha vifo takriban 39,000 kila mwaka na kusababisha mamilioni zaidi ya wanawake kulazwa hospitalini wakiwa na matatizo.
Mbinu zinazotumika uhusizisha kutumia dawa zisizo rasmi, miti ya kienyeji, au kuingiza vitu hatari mwilini. Utaratibu huu usipofanyika kwa usahihi hupelekea mwanamke kupata matatizo yanayoweza leta madhara na kwa kiwango kikubwa kifo kama hayatahudumiwa na mtaalamu wa afya. Mbinu zisizo salama huwa na hatari hasa kwa kuwa mgonjwa hatapata utunzaji na mawaidha baada ya kutoa mimba.
Gharama ya Utoaji Mimba – Kenya
Huduma salama ya kutoa mimba Kenya bad oni changamoto hasa kwa wanawake na wasichana kutoka jamii na familia za mapato ya chini hasa kwa sababu ya gharama. Ingawa njia salama kama utoaji mimba kwa dawa (medical abortion) zinapatikana, huduma hizi si rahisi kumudu kwa kila mtu.
Kwa ujauzito wa mapema, kutumia dawa kama mifepristone na misoprostol katika vituo vya umma au mashirika yasiyo ya kiserikali hugharimu kati ya KES 1,500 hadi 3,000. Hata hivyo, katika kliniki binafsi au maduka ya dawa, bei hii inaweza kupanda hadi KES 7,000 au zaidi, na wakati mwingine hufikia KES 15,000 ikiwa huduma inajumuisha ushauri na ufuatiliaji.
Kwa wanawake wanaohitaji utoaji mimba wa upasuaji—kama vile Manual Vacuum Aspiration (MVA) au Dilation and Evacuation (D&E)—gharama huwa juu zaidi. MVA, inayofanyika hadi wiki ya 15 ya ujauzito, hugharimu kati ya KES 3,000 hadi 10,000. D&E, inayotumika kwa ujauzito wa zaidi ya wiki 12, inaweza kugharimu hadi KES 30,000.
Changamoto za Kupata Huduma Salama ya Utoaji Mimba Nchini Kenya
Ingawa Katiba ya Kenya 2010, kadhalika na maamuzi ya koti(2022), iliruhusu utoaji mimba katika hali Fulani; kama maisha au afya ya mama yako hatarini, wanawake wengi bado hukumbana na vizingiti wanapotafuta huduma salama. Changamoto hizi ni za kisheria, kijamii, kiuchumi, na kiutawala ifiatavyo:
Kutokueleweka kwa Sheria
Sheria ya utoaji mimba nchini si wazi kwa wengi. Ingawa inaruhusu katika baadhi ya hali, ukosefu wa mwongozo wa mwafaka huwafanya wahudumu wa afya kuwa na wasiwasi wa kushitakiwa au kupoteza kazi zao. Hili hupelekea wengi wao kuamua kutojihusisha kabisa na huduma hizo. Ni jambo linalihitaji kubainishwa na kutiliwa maanani ili kuondoa woga kwa kuwasaidia wanawake.
Unyanyapaa na Shinikizo la Jamii
Katika jamii nyingi za Kenya na vile vile barani Africa, utoaji mimba ni jambo lililowekewa unayanyapaa katika jamii. Mwanamke anayejaribu kupata huduma hizi anaweza kuhukumiwa, kubezwa au hata kufukuzwa nyumbani. Hali hii huwafanya wengi kutafuta huduma kwa siri na kwa mara nyingi hizi huwa njia hatari. Uhamazishaji unahimizwa na kusisitizwa ili kuondoa shinikizo zilizowekwa katika jamii hasa kwa kizazi
Gharama ya Juu ya mbinu salama
Huduma salama za utoaji mimba, hasa katika kliniki binafsi, ni ghali. Wanawake wa kipato cha chini au wanaoishi maeneo ya vijijini mara nyingi hawawezi kumudu gharama za dawa, ushauri, na usafiri. Hii huwapelekea kuchagua njia zisizo salama.
Upungufu wa Huduma Vijijini
Vituo vinavyotoa huduma salama vingi viko mijini. Wanawake wa mashinani hulazimika kusafiri mbali au kukosa huduma kabisa, jambo linalochelewesha matibabu na kuongeza hatari za kiafya.
Kukosekana kwa Taarifa Sahihi
Wengi hawajui haki zao wala njia salama zilizopo. Upotoshaji kuhusu dawa za kutoa mimba, athari zake au hatari za kisheria huwafanya wanawake waogope kutafuta msaada au kutumia njia zisizo salama.
Kwa kiwango kikubwa, utoaji mimba nchini Kenya kwa njia zilizo salama unazuiwa na kutokuwa na sheria iliyo wazi kwa kueleza vidokezo muhimu vya kukubali utoaji mimba hali kadhalika unyanyapaa na woga wa utoaji mimba katika jamii. Hili hupelekea wanawake wengi kutotafuta njia salama na utoaji mimba na pia wahudumu kuogopa kupeana huduma.
Jambo la muhimu ni kwamba huduma hii ikifanywa inavyofaa, utoaji mimba hufanikishwa kwa ufaafu na kwa haraka. Changamoto ni kuwasilisha huduma hii kwa wanaohitaji kwa gharama wanayoweza kufadhili. Vile vile, shirika la safe2choose linasisitiza jambo la kumaliza unyanyapaa na woga katika jamii ni muhimu ili kumaliza dhana ya kuavya mimba kwa njia zisizo salama.
Unahitaji ujumbe sahihi na usaidizi kuhusu utaoji mimba?
safe2choose inakusaidia kupata ujumbe sahihi kuhusu njia na jinsi ya kuavya mimba kwa njia salama. Washauri wetu wana tajriba kubwa na watakusaidia katika maswala mbali mbali ya kutoa mimba. Wasiliana nasi na washauri wetu kwa tovuti safe2choose.