Ukubwa wa maandishi
safe2choose

Bodi ya Afya

Karibu kwenye ukurasa wa Bodi ya Ushauri wa Kimatibabu ya safe2choose iliyoundwa na wataalamu waliobobea katika nyanja za Afya na Haki ya Ujinsia na Uzazi (SRHR) ambao husaidia timu ya safe2choose katika kukagua na kuidhinisha miongozo ya kimataifa inayohusiana na utoaji mimba kwa njia salama inayoshirikiwa kwenye tovuti na kupitia jopo linalotoa ushauri. Bodi ya Ushauri wa Kimatibabu hushirikiana na timu ya safe2choose katika kutoa maarifa muhimu inayochangia mapendekezo ya ushauri nasaha inayozingatia viwango vya juu zaidi vya ubora na huduma salama.

Portrait showing Dr. Matt Reeves' face, smiling in a suit and blue shirt, Executive Director of the DuPont Clinic

Dk. Matt Reeves

Daktari wa Binadamu(MD), mwenye Shahada ya Uzamili ya Afya ya Umma(MPH), Mshirika wa FACOG, ni Mkurugenzi Mtendaji wa DuPont Clinic | Marekani

Matthew Reeves, Daktari wa Binadamu(MD), mwenye Shahada ya Uzamili ya Afya ya Umma(MPH), Mshirika wa FACOG, ni Mkurugenzi Mtendaji wa DuPont Clinic, kituo kinachojikita katika kutoa huduma ya utoaji mimba kwa mgonjwa katika miezi mitatu yote ya mwanzo ya ujauzito. Akiwa mwenye nyadhifa za ngazi za juu katika Chuo Kikuu cha Afya cha George Washington, Chuo Kikuu cha Afya cha Stanford na Chuo cha Afya ya Umma cha Johns Hopkins Bloomberg, Dk. Reeves ni mtaalamu bingwa.

Dk. Reeves ni mhitimu wa Chuo kikuu cha Afya cha Harvard na amemaliza mafunzo ya juu katika masuala ya uzazi na magonjwa ya wanawake katika Chuo Kikuu cha California, San Francisco (UCSF). Alijiendeleza utaalam wake akijikita katika Vipimo ya Ultrasound katika kituo cha UCSF. Baada ya hapo akawa mshirika katika kituo kinachojikita katika masuala ya Uzazi wa Mpango katika Chuo Kikuu cha Pittsburgh.

Akiwa Mshiriki katika American College of Obstetricians & Gynecologist na Society of Family Planning, Dk. Reeves ametoa mchango mkubwa katika nyanja hiyo. Majukumu yake ya awali ni pamoja na kuhudumu kama Afisa Mkuu wa Matibabu wa WomanCare Global na kama Mkurugenzi wa Matibabu wa National Abortion Federation. Hivi sasa, ana jukumu kubwa katika Kamati ya Masuala ya Kitabibu ya Society of Family Planning na Kamati ya American College of Obstetricians & Gynecologist. Dk. Reeves anaendelea kutoa mchango muhimu kama Mshirika anayeheshimika katika American College of Obstetricians & Gynecologist na Society of Family Planning.

Portrait of Dr. A. Kaaria, safe2choose medical board member, MBChB, MMed Obs/Gyn, Fellow of the College of Obstetricians and Gynecologists

Dk. Alice Kaaria

Shahada ya Tiba ya Binadamu na Upasuaji(MBChB), Mtaalamu wa Tiba katika Magonjwa ya Wanawake na Uzazi, Mshiriki wa COG (ECSA) | Kenya

Dk. Alice Kaaria, daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi na mtaalamu wa masuala ya kliniki kwa miongo miwili, mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 12 kwenye masuala ya Afya ya Uzazi katika mashirika yasiyo ya faida. Mbali na kuwa mhadhiri wa chuo kikuu na mkufunzi katika magonjwa ya wanawake na uzazi, Dk. Kaaria anatoa mchango mkubwa katika kuhamasisha afya ya ujinsia na uzazi katika jamii zenye kipato cha chini, zilizotengwa na ambazo hazipatiwi huduma, lakini pia kwa wanawake na wasichana wenye ulemavu.

Dk Kaaria amejipatia umaarufu kutokana na mchango wake mkubwa katika kutoa elimu zinazolenga haki ya Afya na Uzazi. Juhudi zake zinalenga kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora ya afya ya uzazi kwa mama, watoto wachanga, watoto pamoja na vijana. Ni mmojawapo wa wanachama wa Bodi ya Reproductive and Maternal Health Consortium - Kenya, anayetoa usaidizi wa kiufundi na kifedha kwa vitengo kama vile Idara ya Afya ya Uzazi, Youth Health Organization na Women Spaces Africa. Mashirika haya yanalenga kuelimisha kuhusu afya ya uzazi na upatikanaji wa huduma za afya kwa wanawake na wasichana wenye ulemavu.

Akiwa kama mshauri wa Idara ya Afya ya Uzazi na Uzazi wa Mama ya Wizara ya Afya ya Kenya, Dk. Kaaria ana mchango mkubwa katika uundaji wa sera ya kitaifa ya afya ya umma, viwango na itifaki za kimatibabu. Pia ni mkufunzi mkuu anayetoa maarifa na uzoefu wake kwa wengine waliopo katika nyanja hiyo.

Portrait of Dr. Tesfaye Tufa, safe2choose medical board member and associate professor specializing in obstetrics and gynecology

Dk. Tesfaye Tufa

Profesa Mshiriki katika Masuala ya Uzazi na Magonjwa ya Wanawake | Canada

Tesfaye Tufa ni profesa msaidizi katika masuala ya Afya ya Uzazi na magonjwa ya wanawake aliyebobea katika Uzazi wa mpango na afya ya uzazi. Mwaka 2019, alishiriki katika utafiti wa Shirika la Afya Duniani(WHO) akitoa mchango muhimu katika timu ya usanisi wa ushahidi katika kuboresha Mwongozo wa Shirika la Afya Duniani(WHO) wa 2022 wa huduma ya utoaji wa mimba. Akiwa na zaidi ya miaka 12 ya uzoefu kama daktari katika afya ya uzazi kimataifa, Tesfaye anabobea katika utafiti, sera na programu za uhamasishaji. Hivi sasa, ni profesa msaidizi katika Chuo Kikuu cha Ottawa na anafanya kazi kama mshauri wa utafiti katika Shirika la Afya Duniani(WHO).

Portrait of Dr. Laura Gil, gynecologist from Colombia and safe2choose medical board member, specializing in reproductive health

Dk. Laura Gil

Daktari wa Magonjwa ya Wanawake | Colombia

Dk Laura ni daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake kutoka Chuo Kikuu Cha Columbia, mwenye stashahada ya Utafiti kwenye Afya ya Uzazi na Ujinsia katika Nchi Zinazoendelea inayotolewa na Shirika la Afya Duniani(WHO). Ni mwanzilishi mwenza na mkurugenzi wa jopo la Madaktari la Right to Decide cha nchini Columbia, ni msemaji wa Causa Justa, mwanachama wa Kamati ya Utoaji Mimba Salama ya FIGO (International Federation of Gynecology and Obstetrics), mshauri wa Kamati ya Haki za Afya ya Kijinsia na Uzazi ya FLASOG (Latin American Federation of Obstetrics and Gynecology Societies) na mwanachama wa kamati ya kisayansi ya FECOLSOG (Colombian Federation of Obstetrics and Gynecology Societies).