Ukubwa wa maandishi
safe2choose

Taarifa za utoaji mimba kulingana na nchi

Sheria za utoaji mimba na upatikanaji wa huduma hiyo zinatofautiana duniani kote kutokana na sababu za kitamaduni, kidini, na kisiasa. Baadhi ya nchi zimepiga marufuku kabisa utoaji mimba, wakati nyingine zikiruhusu, mara nyingi zinazoruhusu hufanya hivyo kupitia sheria fulani kutegemeana na umri wa ujauzito.

Infographic displaying abortion access categories: Permitted per Request, Socioeconomics Grounds, Preserve Health, Save the Life, and Prohibited Altogether.

Sheria za Utoaji Mimba Duniani

Katika kipindi cha miaka 30 iliyopita, nchi 60 zimerahisisha suala la utoaji mimba kwa kuruhusu kutoa mimba zenye umri fulani, kwa mfano wiki 12 au 14 na si zaidi. Hata hivyo, wanawake 4 kati ya 10 wenye umri wa kuzaa bado wanaishi katika maeneo yenye sheria kali za utoaji mimba. Katika maeneo haya, utoaji mimba unaweza kuruhusiwa tu kwa masharti fulani kama vile ikiwa maisha ya mwanamke yako hatarini au ikiwa alipata mimba baada ya kubakwa, sehemu nyingine utoaji mimba hauruhusiwi kabisa katika mazingira yoyote yale [1,2,3].

Jitihada kubwa zinahitajika ili kuhakikisha kila mtu anapata haki ya kufanya maamuzi kuhusiana na mwili wake.

Upatikanaji wa huduma ya Utoaji Mimba Duniani

Mambo kadhaa yanaweza kuathiri upatikanaji wa huduma ya utoaji mimba salama na kwa wakati. safe2choose inasaidia kutoa taarifa muhimu kuhusu sheria za utoaji mimba na upatikanaji wa huduma hiyo katika nchi mbalimbali.

Upatikanaji wa Rasilimali

Upatikanaji wa huduma ya utoaji mimba hutegemea rasilimali zilizopo kama vile dawa, vifaa, na madaktari waliopata mafunzo. Vidonge vya utoaji mimba kama Mifepristone na Misoprostol vinatambuliwa kama vidonge salama na vyenye ufanisi na vipo kwenye orodha ya dawa muhimu ya Shirika la Afya Duniani (WHO) (6, 7). Hata hivyo, vidonge hivi havipatikani kila mahali hivyo kuongeza vikwazo vya upatikanaji wa huduma ya utoaji mimba salama na kwa bei nafuu katika baadhi ya maeneo (8, 9).

Vikwazo vya Kisheria

Baadhi ya nchi zina sheria kama vile sheria ya muda wa lazima wa kusubiri au sheria ya kuomba ruhusa kutoka kwa wazazi au wenzi, ambazo zinaweza kuchelewesha mchakato na kuathiri maamuzi (5).

Changamoto za Kiuchumi na Kijiografia

Sababu za kiuchumi na kijiografia, kama vile gharama kubwa za kupata huduma na umbali wa kufuata huduma, zinaweza kupelekea ugumu wa kupata huduma za utoaji mimba.

Madhara ya Kitamaduni na Kidini

Imani za kitamaduni na kidini pamoja na aibu inayotokana na utoaji mimba pia iweza kuathiri upatikanaji wa huduma hiyo. Aibu inaweza kusababisha hukumu au ubaguzi, na kufanya iwe vigumu kwa watu kuzungumza au kupata huduma za utoaji mimba. Baadhi ya watoa huduma wa afya pia wanaweza kuchagua kutofanya utoaji mimba kutokana na imani zao binafsi (10).

Jifunze kuhusu utoaji mimba katika nchi yako

Check out this detailed overview of abortion laws and access in various countries. It includes information on whether abortion is legal, the types of abortion available, and details about abortion pills, including if a prescription is needed and the cost. You will also find information on local organizations and resources for additional support, tips for avoiding scams, and how to reach out to our team for live counseling.

If your country is not listed, please visit our partner website, How to Use Abortion Pills or contact our counselors via email at info@safe2choose.org.

Illustration of a globe with location markers, a gavel, books, a glass of water, and pills, symbolizing global healthcare law and justice.

Amerika ya Kusini na Karibiani

Huko Latin America na Caribbean, nchi nyingi zina sheria kali dhidi ya utoaji mimba. Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya nchi zimefanya mabadiliko na kuruhusu upatikanaji zaidi wa huduma ya utoaji mimba. Mabadiliko haya yamechochewa na harakati ya "Green Wave," ambapo raia wanapigania haki za uzazi. Licha ya mabadiliko haya, imani thabiti za kidini na kihafidhina bado zinakwamisha huduma za utoaji mimba sehemu nyingi katika ukanda huo.

Map of Latin America and the Caribbean showing abortion laws and access info

Argentina

Mnamo mwaka 2020, Argentina ilihalalisha utoaji mimba endapo mjamzito ataomba kufanya hivyo kwa mimba yenye umri wa hadi wiki 14 – Huu ni ushindi mkubwa kwa harakati za kifeministi na haki za wanawake katika eneo hilo.

Colombia

Mnamo mwka 2022, Colombia ili halalisha utoaji mimba zenye umri wa hadi wiki 24, na kuweka mfano muhimu katika ukanda huo.

Mexico

Sheria za utoaji mimba zinatofautiana kulingana na jimbo, na baadhi ya majimbo yanaruhusu utoaji mimba zenye umri wa hadi wiki 12. Mnamo mwaka 2021, mahakama kuu ilihalalisha utoaji mimba, ingawa utekelezaji wake bado ni hafifu.

Brazil

Nchi ya Brazil hairuhusu utoaji mimba, sababu pekee zinazoweza kuruhusu mtu kutoa mimba nchini humo ni kesi za ubakaji, hatari kwa maisha ya mama, au matatizo makubwa katika maendeleo ya mimba.

El Salvador

Hii, ni miongoni mwa nchi zenye sheria kali zaidi duniani dhidi ya utoaji mimba. Utoaji mimba hauruhusiwi kwa sababu yoyote ile, hata kama maisha ya mjamzito yako hatarini. Watu wanaotoa mimba na wale wanao wasaidia wanaweza kukumbana na vifungo vya gerezani.

Dominican Republic

Katika Dominican Republic, utoaji mimba unadhibitiwa vikali na huruhusiwa ikiwa maisha ya mama yako hatarini. Hata hivyo, kumekuwepo na mijadala na juhudi za kubadilisha sheria hizi, hasa katika kesi za ubakaji, ndugu wa karibu kupeana mimba, au matatizo makubwa ya uzazi.

Visa halisi toka kwenye jumuiya yetu

Gundua visa vya kweli na uzoefu wa watu ambao wameiamini safe2choose. Ushuhuda huu unaonyesha msaada na mwongozo tunaotoa, na matokeo ya huduma zetu.

Illustration of two women talking: one, a safe2choose counselor, with curly hair in teal floral dress, the other with long black hair in yellow floral dress sharing real stories from the community

Even though I was still very apprehensive, I decided to trust them and share my despair. To my surprise, I was warmly welcomed by the counselors and received all the guidance I needed.

I reached out here because I was desperate and didn’t know who to turn to. I had been searching on Google and found this wonderful team. Even though I was still very apprehensive, I decided to trust them and share my despair. To my surprise, I was warmly welcomed by the counselors and received all the guidance I needed. I was quickly referred to the appropriate place, where I was also treated with great care, and I was able to have my abortion in about a week. It was a very positive experience, with kind support and without judgment.

Anonymous, Brazili

Age: 40, October 2025

I don’t feel ready to have another baby. They inserted a copper IUD incorrectly, and I got pregnant.


I decided to have an abortion because I don’t feel ready to have another baby. They inserted a copper IUD incorrectly, and I got pregnant. My baby was born six months ago, I had postpartum depression, and it’s still hard to feel like I’m doing things right. I don’t think a new baby deserves all the stress from work, a small child, and a complicated relationship. The baby’s father didn’t want the pregnancy either.
After the abortion, I felt very guilty. I’m still sad about what happened because I tried to take care of myself and this still happened. I didn’t know what to do or where to go because abortion is illegal in my country. I found this page, and they helped me a lot and gave me contacts to make this a safe process, especially because I had the IUD and that complicated things.
If you’re in a similar situation, the best thing is to talk about it and cry as much as you need to let the grief out. I don’t think this is easy for anyone, especially if you’re a first-time mom.
Also, it’s better to be well informed about contraceptive methods and their side effects... I learned that you have to visit several doctors to get different opinions and inform yourself better. The copper IUD was inserted at my public health provider very soon after my C-section and didn’t protect me for even six months, and it caused this situation that I will never forget.

Anonymous, Bolivia

Age: 30, October 2025

In a country where choice is denied, discovering support reaffirmed the belief in personal freedom.

It was amazing to know that even in a country where we are told we have no choice, there are people out there that still believe in a persons right to choose what to do with their life. Keep up the great work!

Anonymous, Kostarika

Age: 29, May 2025

Ninawashukuru sana. Hakikisha kuwa watakutunza vyema, haijalishi uko wapi. Uamuzi ni wako, lakini hutatakuwa peke yako.

Hofu ndiyo hisia ya kwanza niliyohisi nilipogundua kuwa nina mimba. Lakini baada ya kuwasiliana na safe2choose, walinifanya nijisikie salama na kuwa na ujasiri kwamba wangeniongoza katika mchakato huu. Mchakato huu ulikuwa wa faragha na rahisi, na washauri walinipa uangalizi niliouhitaji kwa dhati. Ninawashukuru sana. Hakikisha kuwa watakutunza vyema, haijalishi uko wapi. Uamuzi ni wako, lakini hutatakuwa peke yako.

Anonymous, Meksiko

Age: 28, July 2024

0/0
User questioning herself, face resting on hand, question mark above her head

MAELEZO YA ZIADA

Maswali yanayo ulizwa mara kwa mara kuhusiana na utoaji mimba

Sababu kwa nini watu wanaweza kuchagua kufanya utoaji mimba ni za kibinafsi sana na hutofautiana kutoka mtu mmoja hadi mwingine. Mtu anapochagua kufanya utoaji mimba, uamuzi huo mara nyingi hufanywa baada ya kutafakari kwa makini mambo mengi, yakiwemo ya kibinafsi, kiafya, kifedha, na hali za kifamilia. Hatimaye, chaguo la mtu kuhusu mwili wake na afya ya uzazi ni jambo la kibinafsi. Kila mtu ana haki ya kufanya maamuzi ambayo ni bora kwa maisha na hali yake, na ni muhimu kuheshimu uhuru huo bila hukumu au uingiliaji.

NYENZO MUHIMU

Fuata, Jifunze na Shiriki

Jiandae kwa ajili ya utoaji mimba

Ili kujiandaa vyema kwa ajili ya utoaji mimba, tembelea kurasa zifuatazo:

Machapisho ya Hivi Punde Kuhusu Huduma Salama ya Utoaji Mimba

Pata taarifa za hivi punde, habari, na maarifa ukiwa na safe2choose. Yaani taarifa kuhusu maendeleo ya afya ya uzazi, matangazo muhimu na hadithi kutoka kwa jamii yetu, Ukurasa wetu wa Makala unakuhabarisha na kufanya uendelee kushiriki katika taarifa mpya.

Wasiliana nasi.

Ni sahihi kuomba msaada

Ikiwa unahitaji taarifa zaidi au hujapata ulichokuwa unatafuta, tafadhali wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa ushauri au kupitia njia nyingine za mawasiliano.