Kuna tofauti gani kati ya tembe ya asubuhi baadaye na tembe ya kutoa mimba?

Tembe ya asubuhi baadaye [1] (levonorgestrel, ulipristal) ni njia ya dharura ya upangaji uzazi inayoweza kutumika kuzuia mimba kutokea baada ya kujamiiana bila kinga. Inafanya kazi kwa kuzuia uachiliaji wa yai la kike (kuachilia yai) au kwa kuzuia yai kukutana na mbegu za kiume. Tembe ya kutoa mimba ni tofauti kwa sababu hutamatisha mimba ambayo tayari imetokea.

TAZAMA MASWALI ZAIDI

*Hakuna kinachotolewa hapa kinapaswa kudhaniwa kuwa ushauri wa kitaalam na hakuna dawa / tembe zinazopaswa kutumiwa bila agizo kutoka kwa mtaalamu aliye na leseni / aliye sajiliwa anayestahili kuagiza dawa hiyo katika mamlaka yako ya karibu.