Ibuprofen ipo ukitaka kununua katika nchi nyingi, na hii ni dawa iliyopendekezwa kutumia kwa ajili ya maumivu na msokoto. Unaweza kutumia tembe 3-4 (200mg) za ibuprofen kila saa 6-8 kwa maumivu.
Tylenol pia inaweza kutumika, tembe 2 (325mg ya tembe) kila saa 4-6 kwa maumivu. Visodo vya kuleta joto au kupapasa sehemu ya chini ya tumbo (tumbo la uzazi) inaweza pia kusaidia kwa maumivu.
*Hakuna kinachotolewa hapa kinapaswa kudhaniwa kuwa ushauri wa kitaalam na hakuna dawa / tembe zinazopaswa kutumiwa bila agizo kutoka kwa mtaalamu aliye na leseni / aliye sajiliwa anayestahili kuagiza dawa hiyo katika mamlaka yako ya karibu.