Nahitaji kutumia dawa za kuzuia maambukizi ya bakteria wakati wa kutoa mimba?

Si lazima, wala muhimu kutumia dawa za kuzuia maambukizi ya bakteria wakati wa utoaji mimba kwa utabibu Kumbuka hatari ya kupata maambukizi ni chini (chini ya 1%) [1], na wanawake wengi hawana maambukizi baada ya utaratibu huu.

Ikiwa una dalili za maambukizi baada ya utoaji mimba (usaha wenye uvundo au wenye rangi kutoka kwa uke na joto, kibaridi, maumivu ya mifupa, kichefuchefu, kutapika), unastahili kutafuta utathmini wa matibabu Ikiwa ambukizi litathibitishwa, daktari wa matibabu atakuelekeza dawa za kuzuia maambukizi ya bakteria zinazokufaa. Haushauriwi kutumia dawa za kuzuia maambukizi ya bakteria labda uelekezwe na daktari.

[1] Ipas. (2019). Clinical Updates in Reproductive Health. L. Castleman & N. Kapp (Eds.). Chapel Hill, NC: Ipas. Retrieved from: https://ipas.azureedge.net/files/CURHE19-april-ClinicalUpdatesInReproductiveHealth.pdf

TAZAMA MASWALI ZAIDI

*Hakuna kinachotolewa hapa kinapaswa kudhaniwa kuwa ushauri wa kitaalam na hakuna dawa / tembe zinazopaswa kutumiwa bila agizo kutoka kwa mtaalamu aliye na leseni / aliye sajiliwa anayestahili kuagiza dawa hiyo katika mamlaka yako ya karibu.