Nitahitaji kupanuka na kutotelwa vitu katika tumbo la uzazi (D & C) baada ya kutumia tembe za kutoa mimba?
Ikiwa tembe za kuto mimba zilitamatisha mimba kwa ufanisi wanawake wengi hawatahitaji kutumia dawa zozote zaidi, wala kuwa na utaratibu wowote wa upasuaji baadaye.
Baadhi ya watoaji wa huduma za afya hawana mafunzo bora na wanaweza kupendekeza utaratibu wa upasuaji visivyofaa ili kutoa mabaki ya vijinyama katika tumbo la uzazi Hata hivyo, hii inafanywa kwa kawaida na tumbo la uzazi wako Kumbuka kuwa kwa wastani tembe za kutoa mimba zinaweza kuchukua wiki chache kujikamilisha zenyewe.
Ikiwa kutakuwa na sababu halisi ya utabibu ya kutoa vijinyama katika umbo lako la uzazi, utaratibu salama ni ufyonzaji [1] kwa mrija si D&C. Kwa bahati mbaya, sehemu nyingi D&C ndiyo njia tu inayopatikana
Ikiwa tembe hazikutamatisha uja uzito unaweza kujaribu tena kwa tembe za kutoa mimba. Kurudia utaratibu ni salama muradi tu usubiri saa 72 tangu wakati wa mwisho ulipotumia tembe za kutoa mimba.
[1] Ipas. (2019). Clinical Updates in Reproductive Health. L. Castleman & N. Kapp (Eds.). Chapel Hill, NC: Ipas. Retrieved from: https://www.ipas.org/wp-content/uploads/2023/09/Ipas-Clinical-Updates-in-Reproductive-Health-CURHE23b.pdf
Baada ya kumeza tembe za kutoa mimba FAQs
- Nahitaji jaribio la mawimbi sauti ili kuthibitisha ikiwa tembe za kutoa mimba zilifanikiwa?
- Utenda kazi wa tembe za kutoa mimba hupungua zinapotumika mara kwa mara?
- Nawezaje kuzuia mimba nyingine siku za usoni?
- Nastahili kupumzika siku ngapi baada ya kutumia tembe za kutoa mimba?
- Nini kitafanyika ikiwa bado nina uja uzito baada ya kutumia tembe za kutoa mimba?
- Nitahitaji kupanuka na kutotelwa vitu katika tumbo la uzazi (D & C) baada ya kutumia tembe za kutoa mimba?
- Naweza kuwa na uwezo wa kupata uja uzito baada ya utoaji mimba?
- Nastahili kungoja kipindi kipi ili kujamiiana baada ya kutumia tembe za kutoa mimba?
*Hakuna kinachotolewa hapa kinapaswa kudhaniwa kuwa ushauri wa kitaalam na hakuna dawa / tembe zinazopaswa kutumiwa bila agizo kutoka kwa mtaalamu aliye na leseni / aliye sajiliwa anayestahili kuagiza dawa hiyo katika mamlaka yako ya karibu.