Nastahili kupumzika siku ngapi baada ya kutumia tembe za kutoa mimba?
Kupumzika baada ya utoaji mimba kwa utabibu si lazima, ingawa inapendekezwa ili wewe ujihisi kuwa sawa zaidi.
Ikiwa unatumia Mifepristone kuna uwezekano utaendelea na shughuli zako za siku na kuelekea hadi kabla ya kutumia Misoprostol. Mara tu baada ya kutumia Misoprostol utakuwa na msokoto na kutokwa damu Wanawake wengi wanapendelea kupumzika msokoto na kutokwa damu unapokuwa mwingi Wanawake wengi watakuwa na dalili nyingi katika saa 12 za kwanza; kwa kawaida baada ya saa 48 baada ya kutumia Misoprostol dalili zote hupungua Kutegemea na vile unavyohisi unaweza kutaka kufanya shughuli zako za kila siku au unaweza kupendelea kupumzika. Tena, kila mwanamke ana tajriba tofauti hivyo itategemea jinsi unavyohisi
Baada ya kumeza tembe za kutoa mimba FAQs
- Nahitaji jaribio la mawimbi sauti ili kuthibitisha ikiwa tembe za kutoa mimba zilifanikiwa?
- Utenda kazi wa tembe za kutoa mimba hupungua zinapotumika mara kwa mara?
- Nawezaje kuzuia mimba nyingine siku za usoni?
- Nastahili kupumzika siku ngapi baada ya kutumia tembe za kutoa mimba?
- Nini kitafanyika ikiwa bado nina uja uzito baada ya kutumia tembe za kutoa mimba?
- Nitahitaji kupanuka na kutotelwa vitu katika tumbo la uzazi (D & C) baada ya kutumia tembe za kutoa mimba?
- Naweza kuwa na uwezo wa kupata uja uzito baada ya utoaji mimba?
- Nastahili kungoja kipindi kipi ili kujamiiana baada ya kutumia tembe za kutoa mimba?
*Hakuna kinachotolewa hapa kinapaswa kudhaniwa kuwa ushauri wa kitaalam na hakuna dawa / tembe zinazopaswa kutumiwa bila agizo kutoka kwa mtaalamu aliye na leseni / aliye sajiliwa anayestahili kuagiza dawa hiyo katika mamlaka yako ya karibu.