Kanusho: HUU SI USHAURI WA MATIBABU
Misoprostol ni nini na hutumika kwa nini?
Misoprostol ipo katika kundi la dawa linaloitwa prostaglandins na hutumiwa kutibu changamoto zinazo husiana na uzazi. Dawa hii huhusika katika Utoaji mimba, husaidia kukabiliana na madhara ya kuharibika kwa mimba, uchungu wa kuzaa, kukomaa kwa seviksi kabla ya upasuaji, na matibabu ya kutokwa na damu baada ya uzazi (1; 2; 3; 4). Misoprostol inaweza kutumika kutoa mimba yenye wiki hadi 24 (5).
Kwakuwa inatumika sana katika matibabu kwa ajili ya kuzuia na kutibu hali mbalimbali, misoprostol ipo kwenye orodha ya dawa muhimu ya Shirika la Afya Duniani. Misoprostol ni dawa muhimu kwani inatoa huduma ya matibabu ya utoaji mimba, dawa hii husaidia katika utoaji mimba ulio salama na wenye ufanisi. Shirika la Afya Duniani wameeleza taratibu za kutumia misoprostol nyumbani, ambazo baadhi yake zitachambuliwa katika makala hii (4;6). Tutajadili kwa kina huhusu misoprostol na matumizi yake katika utoaji mimba wa kimatibabu.
Historia ya misoprostol
Misoprostol ilitengenezwa kwa mara ya kwanza nchini Marekani mwaka 1973 ili kutibu vidonda vya tumbo kwa kuzuia asidi kali tumboni; lakini moja ya madhara yake makubwa kwa mjamzito ilikuwa kuathiri uterasi. Kwa vile misoprostol ilitengenezwa kwa mara ya kwanza kutibu vidonda vya tumbo, hii ilipelekea dawa hii kupatikana kwa urahisi zaidi katika nchi zilizo na vikwazo vya kisheria.
Katika miaka ya 1980, watafiti wa Ufaransa walitengeneza mifepristone ambayo pia pia hujulikana kama RU-486, kidonge ambacho kinaweza kutumiwa kwa pamoja na misoprostol ili kutoa mimba. Ufaransa ilihalalisha utaratibu huu mnamo 1988 na kufuatiwa na Uchina, Uingereza na Uswidi. Kwa vile mifepristone inatumiwa kwa utoaji mimba pekee, imekuwa vigumu zaidi kufika katika nchi zilizowekewa vikwazo vya kisheria.
Je, misoprostol inatumikaje?
Misoprostol inaweza kutumika peke yake au kwa pamoja na mifepristone kusababisha utoaji mimba. Ikiwa inatumika pamoja na mifepristone, mifepristone humezwa kwanza kisha kufuatiwa na misoprostol baada ya angalau saa 24 lakini si zaidi ya saa 48. Inapendekezwa kuwa tembe za misoprostol zitumike chini ya ulimi.Kwa kawaida, utachukua tembe kadhaa za misoprostol kwa wakati mmoja. Kulingana na hatua ya ujauzito, huenda ikahitajika kurudia mchakato huu baada ya saa nne.
Je, unaweza kuingiza misoprostol kwa njia ya uke?
Misoprostol inaweza kutumika kwa ufanisi kwa njia tatu tofauti: chini ya ulimi, ndani ya mashavu, na kwa njia ya ukeni, huku mifepristone ikimezwa kama tembe.
Ingawa matumizi ya misoprostol kwa njia ya chini ya ulimi, ndani ya mashavu au kwa njia ya ukeni yote ni yenye ufanisi sawa, haipendekezwi kuitumia kwa njia ya ukeni ikiwa eneo lako lina sheria au vikwazo dhidi ya utoaji mimba. Hii ni kwa sababu misoprostol wakati mwingine inaweza kuacha mabaki yanayoonekana, ambayo yanaweza kutambulika na wahudumu wa afya ikiwa utahitaji matibabu. Matumizi ya misoprostol kwa njia ya chini ya ulimi au ndani ya mashavu hayaachi mabaki yanayoonekana ya tembe (1).
Je! ni tembee ngapi za misoprostol zinapaswa kutumika?
Kiasi cha misoprostol kinachopendekezwa kwa utoaji mimba kamili na wenye mafanikio hutegemea kama unatumia misoprostol baada ya kutumia mifepristone na pia idadi ya wiki za ujauzito.
Ikiwa unatumia mifepristone na misoprostol kwa ujauzito wa hadi wiki tisa, tembe nne za misoprostol mara nyingi zinatosha. Hata hivyo, ikiwa hakutakuwa na damu yoyote baada ya saa 24 tangu utumie misoprostol, unaweza kutumia tembe zingine nne za misoprostol.
Ikiwa unatumia mifepristone na misoprostol kwa ujauzito wa kati ya wiki 9 hadi 13, inapendekezwa kutumia dozi mbili za tembe nne za misoprostol (jumla ya tembe nane). Unaweza kutumia tembe nne za misoprostol, usubiri kwa saa nne, kisha utumie tembe nyingine nne.
Ikiwa unatumia misoprostol pekee kwa ujauzito wa hadi wiki 13, utahitaji tembe 12 za misoprostol. Zinatumika kwa dozi ya tembe nne kila baada ya saa tatu.
Kwa ujauzito wa zaidi ya wiki 13, unaweza kuwasiliana na washauri wa safe2choose kwa usaidizi. Pia unaweza kupata taarifa zaidi na njia mbadala hapa
Je, inachukua muda gani misoprostol kuyeyuka?
Muda unaohitajika kwa misoprostol kuyeyuka hutegemea chapa ya dawa; baadhi huyeyuka vizuri na/au haraka kuliko nyingine. Hata hivyo, haijalishi kama tembe zimeteyuka kabisa au la, mradi zimewekwa kwa dakika 30 katika njia uliyopendelea, huo ni muda wa kutosha kwa mwili kuzipokea.Iwapo unatumia tembe kwa njia ya mdomo, unaweza kumeza mabaki ya tembe hizo kwa maji baada ya dakika 30.
Je, misoprostol hufanyaje kazi mwilini?
Kama ilivyotajwa, misoprostol hutumika mara nyingi kwa pamoja na mifepristone katika utoaji mimba wa kutumia dawa. Mifepristone hutumiwa kwanza, kwani husaidia kusitisha mimba kwa kuzuia homoni inayoitwa projesteroni. Bila projesteroni, ukuta wa mfuko wa uzazi huvunjika na mimba haisongi mbele tena.
Baada ya mifepristone kuzuia projesteroni, huandaa mazingira bora kwa misoprostol kufanya kazi. Misoprostol hufanya kazi moja kwa moja kwenye mfuko wa uzazi kwa kusababisha mikazo ya uterasi ambayo husababisha kutolewa kwa bidhaa za mimba.
Je, utapata maumivu ya tumbo kwa muda gani baada ya kutumia misoprostol?
Maumivu ya tumbo, maumivu ya wastani na kutokwa damu nyingi, pamoja na uwezekano wa kuonekana kwa gando za damu, ni dalili za kawaida za mchakato. Mara nyingi maumivu na kutokwa damu kali hutokea ndani ya saa 48 za kwanza baada ya kutumia misoprostol, lakini huenda kiasi hicho kikadumu kwa siku au wiki kadhaa.
Dalili hizi ni sawa na hedhi nzito au mimba kuharibika.
Ikiwa unatumia mifepristone, tiba hii hailetei dalili nyingi; dalili nyingi huanza tu baada ya misoprostol.
Misoprostol inaweza kusababisha athari za muda mfupi kama: homa, baridi, kuhara, kichefuchefu, kutapika, na kichwa kuuma. Ikiwa haupati dalili hizi, ni kawaida kabisa. Ikiwa upate, zitapotea ndani ya saa 24 au chini.
Je, ni yapi madhara ya kutumia misoprostol?
Kuna mazingira ambapo si salama kutumia misoprostol na mifepristone kwa pamoja. Unaweza kupata sintofahamu hizi hapa.
Ikiwa una Kifaa cha Kuzuia Mimba cha Kupandikizwa Kwenye Uterasi imewekwa, unaweza kutumia misoprostol kwa kuwa si kinyume kikali; hata hivyo, unahitaji tahadhari kabla. Utoaji mimba kwa misoprostol ukiwa na Kifaa cha Kuzuia Mimba cha Kupandikizwa Kwenye Uterasi unaweza kuwa na hatari zaidi kuliko kawaida. Ni salama zaidi kuondoaKifaa cha Kuzuia Mimba cha Kupandikizwa Kwenye Uterasi kabla ya kutumia misoprostol kwa mimba. Hiyo inamaanisha ikiwa uko katika hali hii, unapaswa kuwa makini na hatari zilizopo. Unaweza kupata maelezo zaidi kutoka kwa washauri wetu hapa.
Hitimisho
Misoprostol ni dawa salama na yenye ufanisi ambayo unaweza kujiingizia nyumbani ili kusababisha utoaji mimba. Kwa kawaida huchukuliwa baada ya mifepristone, lakini pia inaweza kutumika pekee.
Baada ya kutumia misoprostol, ni kawaida kupata maumivu ya tumbo, kutokwa damu, na maumivu ya wastani. Dalili za kutokwa damu zinaweza kudumu siku kadhaa hadi wiki kadhaa, wakati athari nyingine za misoprostol kawaida hupotea ndani ya saa 24.
Ikiwa unataka kujifunza zaidi kuhusu utoaji mimba kwa kutumia tembe za misoprostol pekee, tafadhali angalia sehemu yetu ya rasilimali au wasiliana na washauri wetu.



