Ushuhuda Meksiko, umri wa miaka 23

Nina umri wa miaka 23. Nilipogundua kwamba nina mimba rafiki yangu alinipa baadhi ya vidonge ambavyo alikuwa ametumia hapo awali na vikafanya kazi. Nilimeza vidonge ambavyo alinipa mimba yangu ikiwa na wiki 6, lakini hakuna kilichotendeka. Nilianza kutafuta mtandaoni haraka na kwa hofu: Mbona haikufanya kazi? Je, ninaweza kutumia vidonge gani? Miongoni mwa tovuti hizi, nilipata safe2choose na nikaona kwamba wana mazungumzo mtandaoni. Nilianza kuongea na nikaanzisha mazungumzo nao. Walinieleza kwamba nilitumia vidonge hivyo vibaya, na ndio kwa sababu havikufanya kazi. Walisema kwamba ninaweza kujaribu vidonge vile tena na nirudie mchakato, au kwamba ningeweza kununua vidonge kwenye tovuti yao. Kwa kweli, nilikuwa nimetumia pesa zangu zote kwa vidonge vya awali nilivyokuwa nimemeza. Niliwaeleza haya na wakasema kwamba bado wangeweza kunisaidia na wangenipa huduma bila malipo ikiwa singeweza kulipa. Sikuwaamini, ilionekana kana kwamba haiwezekani. Walisema kwamba muda wa usafirishaji ni takriban siku 5. Bado sikuwaamini. Kisha siku ambayo walisema watasafirisha furushi ikafika na nikapata ujumbe wa barua pepe uliokuwa na taarifa ya ufuatiliaji. Furishi liliwasili siku 2 baadaye. Mwanzoni nilikuwa na shaka kabla ya kumeza vidonge (Singeweza kuamini kwamba mtu, hasa asiyenijua na nisiyemjua, angeweza kunisaidia bila malipo), lakini hata hivyo nilivimeza. Nilifuata utaratibu sahihi walionipa na nilitoa mimba kwa fanaka. Huhitaji kuwa na shaka kuhusu safe2choose, ni shirika la kweli linalosaidia wanawake wakati wa mchakato wote.

  • Share your story!

    Share your testimonial with safe2choose! It'll take only a few minutes of your time.

  • Share your story: Upload your story in any of the following format (video, photo, voice recording):

  • safe2choose will not publish stories that are offensive in any way, nor that contradict the safe2choose medical abortion protocols which are based off international medical organizations and our medical team.

  • Sehemu hii ni kwa madhumuni ya uthibitishaji na inapaswa kuachwa bila kubadilishwa.