Jinsi ya Kutoa Mimba na Mifepristone na Misoprostol

Utoaji mimba na Itifaki ya Mifepristone na Misoprostol

Mimba ya matibabu inaweza kufanywa na Mifepristone na Misoprostol mfululizo au kwa Misoprostol peke yake. Ukurasa huu unaelezea habari juu ya mchanganyiko wa Mifepristone na Misoprostol kwa utoaji wa mimba kwa kutumia tembe . Ikiwa tu unaweza kufikia Misoprostol, tafadhali tazama mwongozo huu.

Kabla ya kuanza

Kuchanganya Mifepristone na Misoprostol ni mwafaka sana (95%) [2] kutamatisha uja uzito wa wiki 13 au chini.

Kumbuka habari hii ni muhimu kwa utoaji mimba kwa tembe za kutoa mimba kwa mimba zilizo wiki kumi na tatu au chini zikihesabiwa kutoka siku ya kwanza ya kipindi chako cha mwisho cha hedhi [1, 2]. Kwa kuwa hatujapewa mafunzo ya kusaidia kuavya mimba za zaidi ya wiki kumi na tatu za uja uzito, tutafanya kila tuwezalo kukuelekeza kwa shirika ambalo lina uwezo wa kufanya hivyo

Ili kuthibitisha kuwa njia hii ni salama kwako, tunapendekeza usome sehemu ya awali kuhusu dalili kinzani unapotumia tembe za kutoa mimba. Ikiwa huna hakika utaratibu huu ni chaguo nzuri kwako, wasiliana nasi.

Kipimo cha Mifepristone na Misoprostol

Utahitaji kidonge 1 cha Mifepristone natembe 8 za Misoprostol.

Ikiwa ni ngumu kupata tembe 8, unaweza kuchagua kuendelea na tembe 4 tu za Misoprostol, lakini ufanisi utapungua, na unapaswa kuwasiliana na washauri wetu.
Ikiwa una ujauzito kati ya wiki 10-13, inashauriwa kutumia tembe 8 za Misoprostol. [1, 2, 3]

Tembe ya Mifepristone inapaswa kuwa 200 mg (au sawa na 200 mg) na kila tembe ya Misoprostol inapaswa kuwa 200 mcg. [8]

Ikiwa tembe unazopata zina kipimo tofauti cha mg na / au mcg, utahitaji kuhesabu tena idadi ya tembe ili uweze kutumia kiwango sahihi cha dawa.

Ikiwa una maswali yoyote, tafadhali usisite kuwasiliana nasi. Tuko hapa kukusaidia katika mchakato wako wote wa uaviaji mimba.

Jinsi ya kutumia Mifepristone na Misoprostol kwa utoaji mimba salama

Hatua ya kwanza: Meza tembe ya Mifepristone kwa maji.

Ikiwa utatapika dakika ya kwanza thelathini baada ya kumeza Mifepristone, inawezekana kuwa tembe haitafanya kazi. Katika hali hii, ikiwa una Mifepristone ya ziada, utahitaji kurudia hatua ya kwanza. la sivyo, wasiliana nasi.

Subiri saa ishirini na nne hadi arubaini na nane

Kati ya masaa 24 hadi masaa 48, hakuna tofauti kwa ufanisi wa Misoprostol.

Dalili nyingi zitaanza muda mfupi baada ya kutumia Misoprostol, kwa hivyo chagua wakati unaofaa kwako na mpangilio/ratiba yako. unapokuwa nyumbani bila majukumu.


Hatua ya pili: Meza 800 mg ya Ibuprofen saa moja kabla ya kutumia Misoprostol.

Hatua hii haihitajiki, lakini inapendekezwa sana. Ibuprofen itapunguza kiasi cha misokoto na kukusaidia kukabili uwezekano wa madhara Misoprostol [9]. Kumbuka, Ibuprofen inaweza kutumika katika utaratibu wote na baadaye inapohitajika. Wanawake wanaoathiriwa na Ibuprofen na NSAIDS wanaweza kushauri ukurasa wa FAQs kwa mapendekezo kuhusu njia mbadala za kukabili maumivu.

Ikiwa una dawa ya kupambana na kichefuchefu, unaweza kuitumia wakati huu.

Subiri saa 1


Hatua ya tatu: Weka tembe za Misoprostol chini ya ulimi wako kwa dakika thelathini.

Ni muhimu sana tembe zisalie chini ya ulimi wako kwa dakika thelathini ili kuzipa wakati wa kuchukuliwa katika mfumo wako. Baada ya dakika thelathini unaweza kunywa maji ili kuosha na kumeza mabaki yoyote ya tembe. [1]

Ikiwa utatapika dakika thelathini ambapo tembe za Misoprostol ziko chini ya ulimi wako, inawezekana hazitafanya kazi. Katika hali hii, ni muhimu kurudia hatua ya tatu mara moja.

Ikiwa utatapika baada ya tembe za Misoprostol kuwa chini ya ulimi wako kwa muda wa dakika thelathini, inawezekana zitakuazimefanya kazi na hakuna haja ya kurudia hatua ya tatu.

Subiri saa 3


Hatua ya nne: Weka tembe zingine nne za Misoprostol chini ya ulimi wako kwa dakika thelathini

Damu kawaida huanza ndani ya masaa kadhaa. Ikiwa imekuwa masaa 24 yamepita tangu utumie tembe zako nne zaa kwanza za Misoprostol na bado huna kutokwa na damu au kubanwa na tumbo, wasiliana nasi. Usitumie vidonge zaidi hadi tuweze kutathmini hali hiyo pamoja.

Dalili zinazotarajiwa za Mifepristone na Misoprostol

Baada ya kutumia Mifepristone, wengi wa wanawake hawana dalili zozote zinazoonekana, kumaanisha hawahisi chochote. Ikiwa utatokwa damu baada ya kutumia Mifepristone, bado ni muhimu sana kutumia Misoprostol ili utaratibu huo ufanye kazi. [16]

Baada ya kutumia Misoprostol utashuhudia msokoto na kutokwa damu. Wanawake wengine (si wote) watatoa damu iliyokolea. Jua kuwa haiwezekani kujua hasa msokoto na kutokwa damu kutaanza lini, kwa kawaida ni ndani ya masaa 24 ya kwanza ya kipimo cha kwanza cha Misoprostol, lakini inaweza kuwa masaa kadhaa baadaye. [10]

Damu inayotarajiwa kutoka lazima iwe zaidi na ile ya kipindi chako cha hedhi au angalau ifanane. Unaweza kutokwa au kutotokwa damu kwa siku kadhaa au majuma baada ya kutumia tembe. Uvujaji damu wako unastahili kuwa bora polepole kwa wiki chache zijazo.[11]

Kwa wanawake walio kati ya wiki kumi hadi kumi na tatu,watakuwa na dalili za kuvuja damu na msokoto, hata hivyo unaweza kuona kijusi kinapopita [1]. Kwa kawaida kijusi hiki huchanganyika na damu na damu iliyokolea na kinaweza kupita bila kugunduliwa, lakini ni muhimu kujua kuwa ni kawaida kukiona. Usiwe na shaka, kinaweza kutupwa au kuwekwa kwa visido au kusukumwa na maji chooni

Kumbuka kwamba kila tukio la utoaji mimba ni tofauti na dalili zinaweza kutofautiana kutoka mwanamke mmoja hadi mwanamke mwingine.

Wengi wa wanawake ambao wana dalili za uja uzito wanaacha kuwa nazo siku tano baada ya kutumia Misoprostol. Ikiwa dalili zako za uja uzito zitaanza kupungua na kutoweka baada kutumia tembe, hii ni dalili nzuri kuwa wewe si mja mzito tena.[12]

Madhara ya Mifepristone na Misoprostol

Baada ya kutumia Misoprostol, wanawake wengine hushuhudia madhara ambayo yanaweza kudumu kwa saa chache au siku [1]. Madhara haya ni pamoja na:

  • joto
  • kuendesha
  • Kichefuchefu / kutapika
  • kuumwa kichwa
  • kibaridi
Madhara ya Mifepristone na Misoprostol

Tahadhari

Ili kuepuka uvujaji damu zaidi na / au maambukizi, ni muhimu kwa wiki zifuatazo, au hadi uvujaji damu wako upungue [14], uchukue tahadhari zifuatazo:

  • Kutumia pedi kunapendekezwa kufuatilia kutokwa na damu kwako wakati wa siku chache za kwanza za uavyaji mimba, lakini unaweza kubadili kutumia tamponi au kikombe mara tu unapopata raha.
  • Rudi kwenye shughuli zako za kawaida (mazoezi, kazi, n.k.) mara tu unapohisi kuwa tayari.
  • Unaweza kufanya ngono wakati wowote uko tayari; muhimu zaidi ni kusikiliza mwili wako na tamaa.
  • Tafadhali fahamu kuwa unaweza kupata mimba tena muda mfupi tu baada ya kutoa mimba, ndani ya wiki mbili tu.

Kumbuka: Hakuna ushahidi kwa wakati uliopendekezwa kusubiri kabla ya kujamiiana baada ya kutumia tembe za kutoa mimba, lakini kwa jumla inapendekezwa kuwa usubiri hadi uvujaji damu zaidi ukome, na usikize mwili wako na mahitaji. [2]

tahadhari-kuchukua-baada-ya-utoaji-mimba-kwa-tembe

Ishara za onyo: kutafuta msaada

Ikiwa una mojawapo ya dalili zifuatazo, hii inachukuliwa kuwa ishara ya onyo kuwa unaweza kuwa na utata na unapaswa kutafuta matibabu mara moja.

Ukijaza pedi mbili au zaidi (ijae kabisa mbele hadi nyuma, upande kwa upande) katika saa moja au chini na idumu kwa saa mbili mfululizo.

  • Joto ya nyuzi Thelathini na nane ya Celsius (100.4 digrii Fahrenheit) ambayo haipungui baada ya kumeza Ibuprofen. Mara kwa mara thibitisha kwa kipima joto.
  • Joto ya nyuzi Thelathini na nane Celsius za digrii (100.4 digrii Fahrenheit) ambayo haipungui saa Ishirini na nne baada ya kutumia Misoprostol. Mara kwa mara thibitisha kwa kipima joto.
  • Maumivu ambayo hayapungui baada ya kutumia Ibuprofen.
  • Dor que não diminui mesmo com o uso do Ibuprofeno
  • Rangi au harufu ya damu yako ni tofauti sana na kipindi chako cha kawaida cha hedhi au ina harufu mbaya.
  • Ikiwa una wekundu, unahisi kujikuna au mikono inavimba, shingo na uso, inawezekana kuwa una athari ya dawa. Unaweza kutumia antihistamine, lakini ikiwa unapata ugumu kupumua basi athari ya dawa ni mbaya sana na unahitaji utunzi wa matibabu mara moja. [15]
tahadhari-kuchukua-baada-ya-utoaji-mimba-kwa-tembe

Waandishi:

Timu ya safe2choose na wataalam wanaounga mkono kwenye carafem, kulingana na mapendekezo ya 2020 ya Ipas na mapendekezo ya Shirika la Afya Ulimwenguni ya2012 na 2014.

carafem hutoa utunzaji rahisi na wa kitaalam wa utoaji mimba na upangaji wa uzazi ili watu waweze kudhibiti idadi na nafasi ya watoto wao.

Ipas ndio shirika pekee la kimataifa linalolenga tu kupanua ufikiaji wa utoaji mimba kwa njia salama na upangaji wa uzazi.

WHO ni wakala maalum wa Umoja wa Mataifa unaohusika na afya ya umma ya kimataifa.

[1] World Health Organization. Safe abortion: technical and policy guidance for health systems. Retrieved from: https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/70914/;jsessionid=AB2B02D2E41FB4F6CF95B5F59B0A9AF4?sequence=1

[2] Ipas. (2020). Clinical Updates in Reproductive Health. L. Castleman & N. Kapp (Eds.). Chapel Hill, NC: Ipas. Retrieved from: https://www.ipas.org/wp-content/uploads/2020/08/ClinicalUpdatesInReproductiveHealthCURHE20-English-digital.pdf

[3] World Health Organization. Clinical guidelines for safe abortion. 2014. Retrieved from: https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/97415/9789241548717_eng.pdf?sequence=1

[4] National Abortion Federation. 2020 Clinical Policy Guidelines for Abortion Care. Retrieved from: https://5aa1b2xfmfh2e2mk03kk8rsx-wpengine.netdna-ssl.com/wp-content/uploads/2020_cpgs_final.pdf

[5] Guttmacher institute. Early Pregnancy Failure: Misoprostol May Be Good Alternative to Surgery. Retrieved from: https://www.guttmacher.org/journals/psrh/2006/early-pregnancy-failure-misoprostol-may-be-good-alternative-surgery

[6] Platais I, Tsereteli T, Grebennikova G, Lotarevich T, Winikoff B. Prospective study of home use of mifepristone and misoprostol for medical abortion up to 10 weeks of pregnancy in Kazakhstan. Retrieved from: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/?term=Prospective+study+of+home+use+of+mifepristone+and+misoprostol+for+medical+abortion+up+to+10+weeks+of+pregnancy+in+Kazakhstan

[7] Gynuity. Efficacy of Misoprostol Alone for First-Trimester Medical Abortion: A Systematic Review. Retrieved from: https://gynuity.org/resources/efficacy-of-misoprostol-alone-for-first-trimester-medical-abortion-a-systematic-review

[8] Elizabeth G. Raymond, Caitlin Shannon, Mark A, Weaver, Beverly Winikoff. First-trimester medical abortion with mifepristone 200 mg and misoprostol: a systematic review. Retrieved from: https://www.contraceptionjournal.org/article/S0010-7824(12)00643-9/fulltext

[9] Livshits, Anna et al. Fertility and Sterility, Volume 91, Issue 5, 1877 – 1880. Ibuprofen and paracetamol for pain relief during medical abortion: a double-blind randomized controlled study. Retrieved from: https://www.fertstert.org/article/S0015-0282(08)00176-3/fulltext

[10] Gynuity. providing medical abortion in low-resource settings: an introductory guidebook. Second Edition. Retrieved from: https://gynuity.org/assets/resources/clinguide_maguide2nd_edition_en.pdf

[11] Planned Parenthood. How does the abortion pill work? Retrieved from: https://www.plannedparenthood.org/learn/abortion/the-abortion-pill/how-does-the-abortion-pill-work

[12] Gynuity. Self-Assessment of Medical Abortion Outcome using Symptoms and Home Pregnancy Testing. Retrieved from: https://gynuity.org/resources/self-assessment-of-medical-abortion-outcome-using-symptoms-and-home-pregnan

[13] National Abortion Federation. Expected Side Effects of Medical Abortion. Retrieved from: https://prochoice.org/online_cme/m2expected2.asp

[14] A.R. Davis, C.M. Robilotto, C.L. Westhoff, S. Forman, J. Zhang. Bleeding patterns after vaginal misoprostol for treatment of early pregnancy failure. Retrieved from: https://academic.oup.com/humrep/article/19/7/1655/2356520

[15] NHS. Risks-Abortion. Retrieved from: https://www.nhs.uk/conditions/abortion/risks/

[16] De Nonno LJ, Westhoff C, Fielding S, Schaff E. Timing of pain and bleeding after mifepristone-induced abortion. Retrieved from: https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/11239617

Chaguzi za Utoaji Mimba Salama kwa kutumia Tembe

Huduma zetu