Baada ya utoaji mimba kwa Njia ya kunyonya au Kufyonza, ni muhimu kupokea huduma sahihi za baada ya utoaji mimba na, ikihitajika, kupata chaguo za kuzuia mimba.
Haya ni baadhi ya mambo ya kuzingatia:
- Baada ya Njia ya kunyonya au Kufyonza yako, ni kawaida kuvuja damu kwa siku chache. Tumia pedi kufuatilia uvujaji damu; unaweza kubadilisha na kutumia tamponi au kikombe cha hedhi utakapo jishisi vizuri.
- Unaweza kuruejea kwenye shughuli zako za kawaida, kama shule, kazi au michezo, wakati wowote utakapo jihisi kuwa uko tayari.
- Kihisia, ni kawaida kuhisi hisia tofauti, kama afueni, huzuni, au mabadiliko ya hisia. Jipe muda wa kupona, na zungumza na mtu unayemwamini au wasiliana na timu yetu ya ushauri kwa usaidizi.
- Ni salama kufanya ngono tena wakati utakapohisi kuwa tayari kimwili na kihisia.
- Kumbuka, unaweza kushika mimba tena haraka, wakati mwingine ndani ya wiki mbili, hivyo kutumia dawa za kuzuia mimba ni muhimu ikiwa hutaki kushika mimba nyingine. Unaweza kuanza kutumia mbinu yoyote ya kuzuia mimba mara baada ya utoaji mimba kwa njia ya upasuaji. Kabla hujaondoka kwenye kliniki, unaweza kupewa taarifa kuhusu mbinu tofauti za kuzuia mimba zilizopo na uchunguze ni chaguo gani unahisi linafaa kwako. Ikiwa ungependa kupata taarifa zaidi kuhusu dawa za kuzuia mimba, tembelea Find My Method, au uwasiliane na kliniki ya upangaji uzazi iliyo karibu nawe kwa mwongozo zaidi.
- Wahudumu wa afya wanapaswa pia kutoa taarifa za mawasiliano ikiwa una maswali au wasiwasi wowote baada ya kufanyiwa utaratibu huo.