Nahitaji jaribio la mawimbi sauti ili kuthibitisha ikiwa tembe za kutoa mimba zilifanikiwa?
Jaribio la mawimbi sauti si lazima baada ya tembe ya kutoa mimba. Ingawa wakati mwingine itasaidia kuthibitisha kama utaratibu ulifanikiwa, inaweza pia wakati mwingine kutumika kubaini mwanamke aliye na ” utoaji mimba usio kamili” ikiwa damu na damu iliyokolea bado inaonekana ndani ya tumbo la uzazi Hii ni kawaida kupatikana kwa jaribio la mawimbi sauti wiki chache baada ya kutumia tembe ya kutoa mimba, lakini inaweza kutumika na baadhi ya watoaji wa huduma za afya kubaini “utoaji mimba usio kamili” na kumpendekezea kuwa na ufyonzaji kwa mrija au D & C.
Jaribio la mawimbi sauti linastahili kufanywa wakati ambapo kuna shuku ya utata (kutokwa damu zaidi, ambukizi, nk) Hata hivyo, ikiwa utaratibu wa tembe ya kutoa mimba unaenda inavyotarajiwa bila utata, mbinu isiyoingilia sana ya kuthibitisha ikiwa tembe ilifanikiwa ni jaribio la uja uzito linalofanywa nyumbani kwa mkojo majuma baada ya kutumia tembe.
Baada ya kumeza tembe za kutoa mimba FAQs
- Nahitaji jaribio la mawimbi sauti ili kuthibitisha ikiwa tembe za kutoa mimba zilifanikiwa?
- Utenda kazi wa tembe za kutoa mimba hupungua zinapotumika mara kwa mara?
- Nawezaje kuzuia mimba nyingine siku za usoni?
- Nastahili kupumzika siku ngapi baada ya kutumia tembe za kutoa mimba?
- Nini kitafanyika ikiwa bado nina uja uzito baada ya kutumia tembe za kutoa mimba?
- Nitahitaji kupanuka na kutotelwa vitu katika tumbo la uzazi (D & C) baada ya kutumia tembe za kutoa mimba?
- Naweza kuwa na uwezo wa kupata uja uzito baada ya utoaji mimba?
- Nastahili kungoja kipindi kipi ili kujamiiana baada ya kutumia tembe za kutoa mimba?
*Hakuna kinachotolewa hapa kinapaswa kudhaniwa kuwa ushauri wa kitaalam na hakuna dawa / tembe zinazopaswa kutumiwa bila agizo kutoka kwa mtaalamu aliye na leseni / aliye sajiliwa anayestahili kuagiza dawa hiyo katika mamlaka yako ya karibu.