safe2choose

Ujauzito na Mbinu za Kuzuia Kupata Mimba - FAQ

Kuna njia tofauti za kuzuia kupata ujauzito baada ya utoaji mimba, na chaguo bora ni ile inayoendana na mahitaji yako na mtindo wako wa maisha. Ni bora kutafuta mbinu ya kuzuia kupata mimba ambayo inakufaa; kuna chaguo nyingi, zinazojumuisha utumiaji wa kondomu, tembe za kupanga uzazi, kifaa cha ndani ya mfuko wa uzazi, na vipandikizi, n.k. Iwe unatafuta mbinu ya muda mrefu, inayotumia homoni au isiyotumia homoni, kuna chaguo mbalimbali zinazopatikana.

Ikiwa ungependa kuchunguza chaguo zako, tazama Find My Method– ni rasilimali nzuri ya kulinganisha mbinu na kupata ile ambayo unahisi kuwa inafaa.

Pia, kumbuka, ni salama kufanya ngono tena pale unapojihisi tayari kimwili na kihisia baada ya utoaji mimba. Lakini kumbuka, unaweza kushika mimba baada ya kipindi cha wiki 2 baada ya utoaji mimba, hata ikiwa bado unavuja damu. Mzunguko wako wa hedhi unaweza kubadilika kidogo pia, hivyo basi ni muhimu kuujua vizuri mzunguko wako.

Pata usaidizi wa utoaji mimba na ushauri

Tunatoa taarifa za msingi za ushahidi kuhusu utoaji mimba salama. Huduma yetu ya ushauri wa bure ni salama, ya siri, rahisi, na bila hukumu. Tunasubiri ujumbe wako!

Woman holding laptop offering safe, confidential abortion counseling