Ili kupunguza uwezekano wa utoaji mimba kushindikana na kuongeza usalama wa mchakato wa utoaji mimba, ni muhimu kujua njia salama kulingana na umri wa ujauzito.
Kwa nini ni Muhimu Kuzingatia Umri wa Ujauzito Wakati wa Kuchagua Njia ya Utoaji Mimba
Mara nyingi, vipindi vitatu vya ujauzito na umri tofauti wa ujauzito hutajwa wakati wa mjadala kuhusu mimba, lakini ni muhimu pia kuwa na mjadala kuhusu vipindi hivyo vitatu na njia zinazofaa za utoaji mimba.
Njia ya utoaji mimba inayofaa zaidi kwako hutegemea umri wa ujauzito na mahitaji yako binafsi, ingawa upatikanaji wa njia nyingi zaidi za utoaji mimba unaendelea kupanuka siku kwa siku.
Hata hivyo, hakuna mfano unaoweza kufaa kwa kila mtu kwa kiwango kilekile, kwani hali yako huwa ya pekee kulingana na historia yako ya matibabu, asili ya ujauzito, mahali ulipo, na sheria za nchi unayoishi.
Kwa ujumla, yapo mambo mengi ya kuzingatia wakati wa kuamua ni njia ipi bora ya utoaji mimba, mambo hayo ni kama vile:
- Mimba yako imetungwa nje ya mfuko wa uzazi
- Una tatizo la damu kuganda au unatumia dawa za kupunguza uwezo wa damu kuganda
- Una mzio wa misoprostol au mifepristone
- Una ugonjwa mbaya wa ini, figo au mapafu
- Una kifaa cha uzazi kilichowekwa kwenye mfuko wa uzazi (IUD)
- Unatumia dawa za corticosteroids mara kwa mara
- Una mfuko wa uzazi wenye umbo lisilo la kawaida
Mambo haya yote, pamoja na mengine mengi, yanaweza kuamuai aina ya njia ya utoaji mimba inayokufaa. Ingawa si lazima, unaweza kuwasiliana na mtoa huduma wa afya au mshauri ili kupata taarifa zaidi. Pia unaweza kuzungumza na mshauri moja kwa moja kupitia tovuti ya safe2choose.org. Utashauriwa kuhusu njia ya utoaji mimba inayokufaa zaidi na kupata maelekezo ya jinsi ya kupata ushauri wa kitabibu endapo utahitaji.
Chapisho hili linakusudia kukusaidia kuelewa ni njia ipi ya utoaji mimba inayofaa zaidi kulingana na umri wa ujauzito wako. Kwanza kabisa, tutakuongoza kufahamu jinsi ya kujua umri wa mimba yako kisha tutaeleza kwa kina njia mbalimbali za utoaji mimba zinazofaa kulingana na hatua tofauti za ujauzito.
Jinsi ya Kujua Umri wa Ujauzito
Umri wa ujauzito, au umri wa kiinitete, huhesabiwa kuanzia siku ya kwanza ya hedhi ya mwisho ya mjamzito. Hii ni kwa sababu muda wa hedhi ya mwisho ni kiashiria kizuri cha wakati ambapo yai lilitolewa kwaajili ya kurutubishwa, hivyo huwa kiashiria kizuri cha wakati wa kutungwa mimba.
Njia za Utoaji Mimba Kulingana na Hatua ya Ujauzito
Utoaji Mimba kwa Njia ya Vidonge (hadi wiki 13)
Njia hii kwa kawaida huhusisha hatua mbili za kutumia mifepristone na misoprostol. Pia unaweza kutoa mimba kwa kutumia misoprostol pekee, ingawa hii hufanyika tu pale ambapo rasilimali ni chache na au mgonjwa ana mzio wa mifepristone, kwani tafiti zinaonyesha kuwa njia ya kutumia mchanganyiko wa vidonge vya mifepristone na misoprostol huwa ina ufanisi zaidi.
Misoprostol Pekee
Ili kutoa mimba kwa usalama kwa kutumia misoprostol pekee, utahitaji vidonge 12 vya misoprostol, kila kimoja kikiwa na 200 mcg ya kiungo hai. Hii inajumuisha dozi yenye jumla ya 2400 mcg, ambazo zinapaswa kutumika katika dozi tatu tofauti za 800 mcg (vidonge 4), ambazo hutumika kila baada ya saa 3.
Ikiwa mimba yako ina wiki 10 hadi 13, inashauriwa kutumia vidonge vyote 12 ili kuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kufanikisha utoaji mimba. Ikiwa unaweza kupata vidonge 8 tu, pia unaweza kutumia, lakini ufanisi utakuwa mdogo, na ni vema kushauriana na mshauri kwa msaada zaidi kabla ya kuanza mchakato.
Iwapo vidonge vyako vina kiwango tofauti cha dozi, mfano vidonge vya 400 mcg kila kimoja, unapaswa kubadili idadi ya vidonge ili kuhakikisha unatumia dozi sahihi. Ni muhimu sana kutumia dozi sahihi na kwa wakati sahihi, hivyo hakikisha uko mahali salama penye faragha, na tumia dawa za kupunguza maumivu kama ibuprofen (800 mg) au diclofenac (50 mg) kabla ya kila dozi ili kusaidia kudhibiti maumivu ya tumbo.
Mifepristone + Misoprostol
Ili kutumia mifepristone na misoprostol katika mchakato wa utoaji mimba salama na wenye ufanisi, anza kwa kumeza kidonge kimoja cha mifepristone cha 200 mg kwa kutumia maji. Dawa hii huzuia homoni inayohitajika kudumisha ujauzito.
Baada ya kutumia mifepristone, subiri angalau saa 24 lakini si zaidi ya saa 48 kabla ya kutumia misoprostol. Wakati huu wa kusubiri, chagua muda ambao unaweza kupumzika, kuwa na faragha, na kupata choo kwa urahisi. Takriban dakika 30 kabla ya kutumia misoprostol, tumia dawa ya kupunguza maumivu kama ibuprofen 800 mg ili kusaidia kudhibiti maumivu ya tumbo yatakayofuata.
Ili kutumia misoprostol, weka vidonge 4 (kila kimoja chenye 200 mcg) chini ya ulimi wako kisha subiri viyeyuke kwa dakika 30 bila kula au kunywa. Unaruhusiwa kumeza mate kwa kipindi chote dawa inapokuwa chini ya ulimi. Baada ya dakika 30, kunywa maji ili kumeza vipande vilivyobaki.
Kwa kawaida, maumivu ya tumbo na damu huanza kutoka ndani ya saa 4 hadi 6, wakati mwingine yanaweza kuchukua hadi saa 24 kuanza. Hivi ni viashiria vya kawaida kuwa mchakato wa utoaji mimba umeanza. Ikiwa una ujauzito wa chini ya wiki 9 na bado hujaanza kutokwa damu kama ile ya kipindi cha hedhi ndani ya saa 24, unaweza kutumia dozi ya pili ya vidonge 4 vya misoprostol kwa njia hiyo hiyo.
Ikiwa mimba yako ina wiki 9 hadi 13, inashauriwa kutumia dozi ya pili saa 4 baada ya dozi ya kwanza ili kuongeza ufanisi. Katika mchakato mzima, unaweza kuendelea kutumia dawa za maumivu kadri unavyohitaji, lakini epuka aspirini kwani inaweza kupelekea kutokwa na damu nyingi. Daima hakiki dozi ya vidonge vyako na rekebisha kama si 200 mcg kila kimoja.
Ikiwa mimba yako ina zaidi ya wiki 13, unaweza kuwasiliana na washauri wa safe2choose kwa msaada zaidi. Pia unaweza kusoma zaidi kuhusu vidonge vya utoaji mimba.
Vacuum Aspiration (Hadi Wiki 16)
Manual Vacuum Aspiration (MVA) na Electric Vacuum Aspiration (EVA) (hadi wiki 16)
Njia hii kwa kawaida hutumika kwa mimba zenye umri wa chini ya wiki 16.
Tube hupandikizwa ndani ya mfuko wa uzazi kupitia kwenye kizazi (cervix), na mimba huondolewa kwa kutumia mvuke wa msuguano (suction). Msuguano huu unaweza kuwa wa mkono (manual) au wa umeme (electric), hiki ndicho hutofautisha MVA na EVA. Watoa huduma wengi hupendelea kutumia vacuum aspiration kwa sababu ni njia ya haraka, rahisi, na inahitaji vifaa vichache tu. Vacuum aspiration pia inaweza kutumika baada ya utoaji mimba kwa nia ya vidonge kushindikana au mimba kuharibika (miscarriage).
Vacuum aspiration inaweza kutumika kuharibu mimba ya kuanzia wiki 2 hadi wiki 16. Soma mwongozo wa matumizi salama ya MVA hapa
Dilation and Evacuation (Wiki 15–24)
Njia hii kwa kawaida hufanyika kwa mimba ambayo ipo nje ya kipindi cha trimester ya kwanza. Njia hii hujumuisha matumizi forceps zinazowekwa ndani ya kizazi na mfuko wa uzazi ili kuondoa mimba. Mtaalamu wa afya huanza kwa kutoa dawa itakayofungua kizazi (cervix).
Dawa hizi zinaweza kuwa vidonge maarufu vya utoaji mimba, Mifepristone au Misoprostol, au dawa inayoitwa osmotic dilator. Osmotic dilators hufanywa kwa kutumia mwani wa baharini, na vinapowekwa kwenye njia ya uke husaidia kufungua kizazi ili forceps ziweze kupita.
Baada ya hapo, utachomwa sindano za ganzi (local au general anaesthesia) kutegemeana na umri wa ujauzito, na mchakato huu kawaida hutumia wastani wa dakika 15.
D&E ni njia inayotumika kwa mimba zenye umri wa wiki 15 hadi 24.
Ili kupata njia inayofaa ya utoaji mimba kwa hatua tofauti za ujauzito inaweza kuwa changamoto kwa wengi, lakini washauri wetu wa safe2choose wako tayari kukusaidia katika kila hatua na kukuwezesha kupitia hatua zote muhimu. Wasiliana nao moja kwa moja au kwa njia ya barua pepe kupitia info@safe2choose.org.
Ni wakati gani Unapaswa Kutafuta Huduma za Afya?
Tafuta msaada wa haraka wa kitabibu ikiwa:
- Unatokwa na damu nyingi kiasi cha kutumia pedi mbili au zaidi kila saa kwa saa mbili mfululizo.
- Umepatwa na homa iliyotokea saa 24 au zaidi baada ya kutumia misoprostol na haipungui baada ya kutumia ibuprofen.
- Una maumivu makali ambayo hayapungui baada ya kutumia dawa za maumivu kama ibuprofen.
- Unatokwa na uchafu wenye harufu mbaya au wenye mwonekano tofauti na damu ya kawaida ya hedhi.
- Unahisi hali ya ugonjwa au udhaifu mwilini.
- Una wekundu, uvimbe, au muwasho kwenye uso, mikono, au shingo. Dalili hizi zinaweza kuwa za mzio.
- Unapata shida ya kupumua.
Ikiwa una hata dalili moja kati ya hizi, tafadhali tafuta msaada wa kitabibu haraka iwezekanavyo.
Unahitaji Msaada Kuchagua Njia?
Safe2choose, washauri wetu wenye mafunzo wapo hapa kutoa msaada wa huruma na usiri kukusaidia kufanya maamuzi sahihi kuhusu ujauzito wako. Ikiwa unahitaji msaada kuelewa umri wa mimba yako, mwongozo juu ya njia salama za utoaji mimba, au taarifa kuhusu huduma za baada ya utoaji mimba, tuko pamoja nawe katika kila hatua. Usalama na ustawi wako ndiyo vipaumbele vyetu, na tunahakikisha unapata taarifa sahihi na huduma salama za utoaji mimba. Tembelea tovuti zetu: safe2choose.org


