Zuia uzazi katika utoto na ujana. Kwa nini kubeba mimba hadi mwisho ni hatari sana kuliko kutoa mimba kwa watoto na vijana?

Zuia uzazi katika utoto na ujana

Kama jamii, tuna mtazamo pendwa kuhusu uzazi. Jamii inaamini kuwa mama bora ni mwanamke mwenye fadhili, anayejali na anayependa watoto. Ana hamu ya asili ya kutunza wengine, na maisha yake yanatimizwa kwa kubeba ujauzito na kujifungua. Mtazamo huu wa uzazi huchochewa na vyombo vya habari, ambapo mimba mara nyingi huonyeshwa kama jambo lisilo na madhara, na kulea mtoto huonekana kama jambo la fahari sana. Athari za simulizi hizi hazibagui umri, na vijana wadogo wanaweza kuvutiwa katika simulizi hizi kama ilivyo kwa wakubwa. Ni muhimu kwa vijana waliopata mimba iwe ni kwa kukusudia la, kupata muda wa kutathmini chaguzi zao baada ya kupatiwa elimu. Mimba za utotoni zinaweza kuwa na hatari na madhara ya muda mrefu kwa mzazi na mtoto, pia uzazi kwa vijana, hasa wasichana, unapaswa kuzuiliwa.

Athari za kimwili za mimba za utotoni

Kama ilivyo kwa mimba zote, watoto wenye ujauzito wanaweza kukabiliana na changamoto kadhaa za kimwili. Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, matatizo yanayo tokana na ujauzito na kujifungua ndiyo yanayoongoza duniani kwa kusababisha vifo vya watoto wenye umri wa miaka 15-19. Vijana wanaojifungua mara nyingi huwa na afya mbaya na hupuuza mahitaji yao wenyewe wanapo lea mtoto wao. Pia wana uwezekano mkubwa wa kuwa na tatizo la uzito mdogo au uzito mkubwa kupita kiasi ukilinganisha na wanawake wakubwa wanaojifungua. Vijana wadogo wenye ujauzito pia wako katika hatari kubwa ya kupata preeclampsia, anemia, kuambukizwa magonjwa ya zinaa, na kujifungua kabla ya wakati.

Watoto wanaozaliwa na wasichana wadogo wanaweza pia kuwa na matatizo mbalimbali ya kimwili. Licha ya uwezekano mkubwa wa kufia tumboni na mimba kuharibika, watoto wanaozaliwa na wasichana wadogo wana uwezekano mkubwa wa kuwa na uzito mdogo au kuzaliwa wakiwa na hali mbaya. Vile vile, wazazi wenye umri mdogo wana uwezekano mdogo wa kuzingatia utunzaji sahihi wa ujauzito ndani ya miezi michache ya kwanza ya ujauzito. Hii huwaweka wao na watoto wao katika hatari.

Mawazo ya kupenda kubeba mimba na uzazi yanaweza kusababisha madhara makubwa, ikiwa ni pamoja na kifo cha mtoto mjamzito, fetusi, au motto aliye tumboni. Wasichana wadogo wenye ujauzito wanaweza kukabiliwa na changamoto ndogo za kimwili ikiwa watatoa mimba kwa kutumia njia salama. Kadhalika, madhara yanaweza kuwa makubwa ikiwa wataamua kubaki na mimba. Kutoa mimba ni utaratibu salama wa kimatibabu na unapaswa kuzingatiwa wakati wa kujadili athari za kiafya za muda mrefu za mimba za utotoni.

Athari za kiakili zinazo sababishwa na mimba za utotoni

Madhara ya kiakili ya ujauzito yanawaumiza vijana wadogo, kwa sababu miili yao bado inapitia mabadiliko ya homoni, pia hawana utayari wa kimwili na kihisia wa kuwawezesha kubeba mimba na kuzaa. Utafiti unaonyesha kwamba vijana wadogo wenye miaka kati ya 15-19 wanaopata ujauzito, wana uwezekano mara mbili zaidi wa kukumbwa na mfadhaiko baada ya kuzaa kuliko wale walio na umri wa miaka 25 na zaidi.

Dalili za unyogovu baada ya kujifungua ni pamoja na kukosekana ukaribu kati ya mama na mtoto, uchovu, wasiwasi, hofu, na mawazo ya kujidhuru wenyewe au kudhuru mtoto. Wazazi wenye umri mdogo pia wana viwango vya juu vya unyogovu, mfadhaiko, na mawazo ya kujiua kuliko wenzao ambao hawajazaa.

Vijana wadogo wenye ujauzito wana uwezekano mdogo wa kuwa na mitandao mizuri ya usaidizi. Uhusiano kati ya mambo haya huenda kwa njia zote mbili, vijana wengi wanaopata ujauzito hutoka katika malezi ya kushambuliwa, elimu duni, kipato duni, au nyumba zisizo imara na jamii zisizo imara. Vivyo hivyo, vijana wanaopata mimba huenda wakakataliwa na wazazi na marafiki zao. Ukosefu huu wa mtandao wa usaidizi unawaweka katika hatari kubwa ya kupata athari za kiakili kutokana na ujauzito wao.

Ingawa kutoa mimba ni utaratibu unaosumbua sana kiakili, madhara ya mimba za utotoni kwa afya ya akili yana athari sawa. Matokeo ya uzazi huwa tofauti kabisa na matarajio yanayo oneshwa katika vyombo vya habari hasa kwa vijana ambao hawana usaidizi au uthabiti unaohitajika. Utoaji mimba unaweza kuwa chaguo salama zaidi kwa kijana mwenye mimba na mtoto ambaye hajazaliwa, na haumzuii kijana huyo kupata mtoto ikiwa atahitaji katika siku zijazo.

Madhara ya mimba za utotoni kwenye mustakabali wa kijana

Vijana wadogo wenye ujauzito pia hupata athari za kijamii na kiuchumi. Wazazi wenye umri mdogo wana uwezekano mkubwa wa kuacha shule hivyo wana vikwazo zaidi katika nafasi za kazi wanazoweza kupata. Hii inawaweka katika hali mbaya ya kiuchumi. Pia wana uwezekano mdogo wa kushiriki katika matukio mbalimbali ya kijamii kuliko wenzao, hivyo kufanya iwe ngumu kujenga urafiki na jamii ambao ungewasaidia kupanua mitandao yao ya usaidizi. Madhara ya kimwili na kiakili ya ujauzito yanaweza pia kumzuia kijana asipate nafuu na kujirekebisha baadaye maishani, kwa sababu madhara yanaweza kuwa ya muda mrefu, na kwa sababu anakabiliwa na jukumu la kumlea mtoto wake kwa miaka 18 ijayo.

Utoaji mimba huruhusu wajawazito wa rika zote kudhibiti maisha yao. Utoaji mimba unapaswa kuonekana kama zana ya kuandaa maisha bora ya baadaye, na kurekebisha makosa ya zamani. Idadi ya vijana wanaopata mimba imepungua katika kipindi cha muongo mmoja uliopita, kutoka vijana milioni 16 mwaka 2000 mpaka milioni 13 mwaka 2019. Hata hivyo, kupungua kwa idadi hii hakuna uwiano sawa; baadhi ya maeneo kama vile India na Asia ya Kusini yanaongoza, huku maeneo mengine kama vile Afrika ya Kaskazini na Mashariki ya Kati yakifuatia nyuma. Ni muhimu kwa mzazi yeyote hususa ni kwa vijana, kuona “umama” kama dhamira ya dhati yenye athari za kimwili, kiakili na kijamii.
Pia waweza vutiwa na: “Mimba zisizotarajiwa na utoaji mimba” or “Utoaji mimba, haki za uzazi na vifo vya uzazi

Patel, P. H., & Sen, B. (2012). Teen motherhood and long-term health consequences. Maternal and child health journal, 16(5), 1063–1071. https://doi.org/10.1007/s10995-011-0829-2

Koniak-Griffin, D., Walker, D. S., & de Traversay, J. (1996). Predictors of depression symptoms in pregnant adolescents. Journal of perinatology : official journal of the California Perinatal Association, 16(1), 69–76.

Save the Children. (2019). CHANGING LIVES IN OUR LIFETIME.
World Health Organisation. (2020). Adolescent pregnancy. Who.int. Retrieved 5 June 2022, from https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/adolescent-pregnancy