Nini Maana ya Kutokwa na Damu Baada ya Mimba Kutungwa na Nitajuaje?

Kutokwa na damu baada ya kuwekwa mimba

Kutokwa na Damu Baada ya Kutungwa Mimba (Implantation bleeding)

Kutokwa na damu baada ya kutungwa mimba ni jambo la kawaida ambalo hutokea katika hatua za awali za ujauzito. Hata hivyo, inaweza kuwa vigumu kutofautisha mambo haya matatu yaani kutokwa na damu baada ya kutungwa mimba, kutokwa na damu ya kawaida ya hedhi na kutokwa na damu ambayo ni hatari. Makala hii imekusudia kujibu maswali yako kuhusu kutokwa na damu wakati wa hatua za awali za ujauzito na kujadili mambo ya ndani na nje kuhusiana na kutokwa na damu mara baada ya kutungwa mimba.

Utungwaji mimba ni nini?

Unapopata mimba, mbegu za kiume na yai huungana na kutengeneza kiinitete. Baadaye, seli za kiinitete huanza kugawanyika haraka, na kutengeneza kile kinachojulikana kama blastocyst. Kisha blastocyst husogea kupitia mrija wa fallopian hadi kwenye uterasi, ikishikamana na utando wa ukuta wa uterasi. Utaratibu huu unajulikana kama utungaji mimba, ambao ni muhimu katika kuanzisha mimba yenye mafanikio. Kwa kawaida, mimba hutungwa siku tano hadi sita baada ya yai kurutubishwa.

Ikiwa mimba haita tungwa, basi ukuta wa mfuko wa uzazi utatolewa na utapata hedhi ya kawaida ya kila mwezi 1.

Ni zipi dalili za Utungwaji Mimba?

Zipo dalili zinazoweza kuashiria kuwa mimba imetungwa katika mwili wako. Dalili hizi zaweza kujumuisha

 • Kutokwa na damu
 • Kuvimba
 • Maumivu ya tumbo
 • Kichefuchefu
 • Kutokwa na uchafu ukeni
 • Matiti kubana
 • Maumivu ya kichwa
 • Kubadilika kwa hisia 2

Makala hii itajikita kwenye dalili za kutokwa na damu, hasa kutokwa na damu wakati wa utungaji mimba. Tutajadili ni kwanini damu hutoka kipindi cha utungaji na nini unaweza kutarajia.

Je, ni kawaida kutokwa na damu kipindi cha awali cha ujauzito?

Miezi mitatu ya kwanza huhesabika kama kipindi cha ujauzito kati ya wiki sifuri hadi 13. Kutokwa na damu miezi mitatu ya kwanza ni kawaida na hutokea kwa asilimia 15 hadi 25 ya mimba zote. Kutegemeana na sababu kuu yakut kutokwa na damu, wanawake wanaweza kupata mifumo tofauti ya kutokwa na damu. Mifumo ya utokaji damu inaweza kutofautiana kati ya damu nyepesi au nzito, kutokwa na damu bila maumivu au kupata maumivu, kutokwa na damu kwa vipindi fulani au mara kwa mara 3,4.

Je, kutokwa damu kipindi cha awali cha ujauzito ni dalili mbaya?

Kuna sababu kadhaa zinazo pelekea kutokwa na damu ukeni kipindi cha awali cha ujauzito. Baadhi ya sababu hizi ni hatari na sababu nyingine si hatari. Yapo mambo manne yanayo sababisha kutokwa na damu katika hatua za awali za ujauzito. Mambo hayo ni pamoja na;

 • Kutokwa na damu pindi mimba inapo tungwa
 • Mimba kutungwa nje ya mfuko wa uzazi
 • Kuharibika kwa mimba
 • Hali zingine za kiafya kama vile polyps, maambukizi, au uvimbe 4

Kutokwa na damu kipindi cha awali cha ujauzito ni jambo la kawaida kwa kiasi fulani na mara nyingi halina madhara. Kutokwa na damu kwa kawaida kipindi cha awali cha ujauzito hujulikana kama kutokwa na damu kipindi cha utungaji mimba. Wanawake wengi wajawazito hupata damu mimba inapo tungwa na ni ishara ya kawaida ya mimba changa3.

Aina nyingine za kutokwa na damu zinaweza kuonyesha jambo kubwa zaidi, kama vile mimba iliyotungwa nje ya kizazi au kuharibika kwa mimba. Kwahiyo, ikiwa unapata aina yoyote ya kutokwa na damu wakati wa ujauzito, unapaswa kuwasiliana na daktari wako. Ingawa kutokwa na damu pindi mimba inapo tungwa ni kawaida, damu inaweza kuonyesha jambo zito zaidi linalohitaji matibabu.

Kutokwa na damu baada ya kutungwa mimba ni nini?

Kutokwa na damu pindi mimba inapotungwa huja kama matokeo ya yai lililorutubishwa na kupandikizwa kwenye mfuko wa uzazi. Yai linaweza kusafiri, na kusababisha kuka kwa kiasi kidogo cha damu kinachojulikana kama spotting. Kutokwa na damu pindi mimba inapotungwa hutokea kati ya siku 10 hadi 14 baada ya yai kurutubishwa. Kwa kawaida, hutokea karibu na wakati wa hedhi iliyo kosekana. Hivyo, wakati mwingine wanawake huchanganya kati ya kutokwa na damu kipindi mimba inapo tungwa na damu ya hedhi 4.

Je unawezaje kutambua kutokwa na damu pindi mimba inapotungwa?

Kutokwa na damu pindi mimba inapotungwa kwa kawaida hutokea kipindi tofauti na kile cha siku zako za hedhi. Hata hivyo, wanawake hutofautiana linapokuja suala la siku zao, hivyo inaweza kuwa ngumu kutofautisha matukio haya mawili. Unapo tafakari ikiwa damu inayotoka inatokana na mimba kutungwa au ni hedhi ya kawaida, angalia mambo yafuatayo katika damu yako;

 • Rangi. Wanawake wengi wanafahamu rangi ya damu katika siku zao za kawaida. Mara nyingi, damu katika siku zao huwa nyekundu. Kutokwa na damu pindi mimba inapotungwa kunaweza kuwa tofauti kidogo kwani rangi inaweza kuwa pinki iliyoiva au kahawia.
 • Kiasi. Wakati wa hedhi ya kawaida, wanawake wengi hutumia pedi na taulo kwa sababu ya wingi wa damu. Wakati ambapo damu inayotoka pindi mimba inapo tungwa huwa ni kidogo au matone matone na si lazima kutumia pedi au unaweza kuhitaji pantyliner pekee.
 • Mzunguko. Wakati wa hedhi ya kawaida, wanawake hupata mtiririko wa damu mara kwa mara kwa siku kadhaa. Wakati mimba inapo tungwa damu hutokea mara nyingi zaidi.
 • Kuganda. Damu ya hedhi ya kawaida huganda wakati damu inayotoka wakati mimba inapotungwa haigandi.

Hatua zinazofuata

Ikiwa utaona dalili za kutokwa kwa damu pindi mimba inapo tungwa, unaweza kuwa mjamzito. Ikiwa unapata dalili kama hizo, fikiria kupima ujauzito baada ya kukosa hedhi. Hata hivyo, ni muhimu kufahamu kwamba si kila mwanamke mjamzito anaweza kutokwa na damu wakati mimba inapo tungwa. Kwa hiyo, unaweza usione dalili hizo na bado ukawa na ujauzito.

Aidha, ikiwa unapata aina yoyote ya kutokwa damu wakati wa ujauzito, wasiliana na daktari wako. Kutokwa na damu kunaweza kuwa ishara ya kitu kibaya zaidi hivyo ni bora kufanya uchunguzi kila wakati.

Hitimisho

Kumbuka mambo yafuatayo ambayo ni muhimu kuyafahamu kuhusu kutokwa na damu pindi mimba inapo tungwa:

 • Utungwaji mimba hutokea wakati yai lililo rutubishwa linapo pandikizwa kwenye utando wa mfuko wa uzazii.
 • Kutokwa na damu kunaweza kutokea pindi mimba inapo tungwa na inaweza kuwa jambo la kawaida au baya kutegemeana na sababu.
 • Kutokwa na damu pindi mimba inapotungwa ni kawaida na ni ishara ya kawaida ya mimba changa.
 • Damu inayotoka kipindi cha upandikizaji kwa kawaida huwa nyepesi na hutokea mara kwa mara ikilinganishwa na hedhi ya kawaida.
 • Ikiwa utatokwa na damu yoyote wakati wa ujauzito, wasiliana na mtoa huduma wako wa afya.
 1. Kim, S.-M., & Kim, J.-S. (2017). A review of mechanisms of implantation. Development & Reproduction, 21(4), 351–359. https://doi.org/10.12717/DR.2017.21.4.351
 2. Implantation signs and symptoms: Bleeding, cramps, and more. (2019, July 17). Healthline. https://www.healthline.com/health/implantation-signs
 3. Bleeding during pregnancy. (n.d.). Retrieved July 10, 2022, from https://www.acog.org/en/womens-health/faqs/bleeding-during-pregnancy
 4. Uptodate. (n.d.). Retrieved July 10, 2022, from https://www.uptodate.com/contents/overview-of-the-etiology-and-evaluation-of-vaginal-bleeding-in-pregnancy
 5. What is implantation bleeding? (2022, April 19). American Pregnancy Association. https://americanpregnancy.org/pregnancy-symptoms/what-is-implantation-bleeding/