Je, ni salama kutoa mimba zaidi ya moja?

Je, ni salama kutoa mimba zaidi ya moja? s2c alijibu hapa

Utoaji mimba umegubikwa na hekaya, na inaweza kuwa vigumu kujua ukweli. Kwa mfano ni salama kutoa mimba zaidi ya moja? Moja ya imani potofu kuhusiana na utoaji mimba ni kwamba kadiri mtu anavyotoa mimba nyingi, ndivyo utaratibu wa utoaji mimba unavyokuwa hatari zaidi, na hupunguza uwezekano wa mtu huyo kupata mimba. Dhana nyingine ni kuwa utoaji mimba hufanya uwezekano wa kutoa miba nyingine kuwa mdogo na hatarishi.

Haijulikani ni wapi dhana hizi hutokea, lakini ni muhimu kwa wale wanaotaka kutoa mimba mara ya pili au zaidi kujua ukweli kuhusu taratibu hizi, na jinsi zilivyo salama.

Utoaji Mimba Zaidi ya Moja

Nchini Uingereza, wastani wa mtu mmoja kati ya watatu walio na uterasi atatoa mimba, na theluthi moja zaidi ya hawa wametoa zaidi ya mara moja. Nchini Marekani, takriban asilimia 50 ya watu wanaotaka kutoa mimba tayari wameshawahi kutoa mimba.

Zipo sababu nyingi zinazo pelekea mtu kutaka kutoa mimba zaidi ya moja, sababu hizo ni pamoja na kushindwa kutumia aina nyingine za uzazi wa mpango, changamoto za kimaisha ambazo huathiri matumizi ya njia nyingine za uzazi wa mpango, ukosefu wa elimu ya kina ya ngono, na ukatili wa kijinsia. Vile vile, mtu anaweza kufikiri kuwa yuko tayari kwa mimba kisha kubadilisha mawazo yake; ngono, kama maisha, ni ngumu na yenye sura nyingi na si mara zote inawezekana kuwa tayari. Utoaji mimba hutoa mbadala salama kwa ujauzito.

Watoa huduma za afya wana uhakika kwamba watu ambao wametoa mimba katika mazingira salama kwa kawaida hawana changamoto ya kuchelewa kuzaa, kujifungua kabla ya wakati, au matatizo mengine ya matibabu. Uzazi hurudi takriban siku 8 baada ya kutoa mimba, haijalishi umetoa ngapi. Kila utoaji mimba huwa na uzoefu tofauti kuhusiana na hatari ambayo utoaji huo wanaweza kusababisha kwenye mimba zijazo. Watu wanaotoa mimba mimba mara nyingi wanaweza kuwa na uhakika kwamba utaratibu huo ni salama wakati wote.

Taratibu zote za matibabu ikiwa ni pamoja na utoaji mimba kwa njia ya upasuaji huwa na hatari zake, lakini utoaji mimba hauna hatari zaidi ukilinganisha utaratibu mwingine wowote. Nchini Uingereza na Marekani, hakuna kikomo cha kisheria juu ya idadi ya mimba ambazo mtu mmoja anaruhusiwa kutoa. Kama utoaji mimba ungekuwa ni jambo la hatari basi sheria hizi zisingekuwa hivi.

Utoaji mimba dhidi ya Kuzaa Bila Kutarajia

Mara nyingi, kuzaa bila kutarajiwa ni hatari zaidi kuliko kutoa mimba zaidi ya moja. Licha ya athari za kihisia na kisaikolojia zinazoweza kutokea kama matokeo ya utoaji mimba, athari hizi hazipaswi kupuuzwa kwani angalau zinalingana na zile za kuzaliwa bila kutarajiwa.

Mimba na kuzaa kuna athari kubwa kwenye mwili wa binadamu, pia huacha baadhi na uharibifu wa muda mrefu au usioweza kurekebishwa. Kwa hakika, idadi ya watu wanaokufa wakati wa kujifungua ni kubwa zaidi kuliko idadi ya wanaokufa kutokana na utoaji mimba wa kisheria; utafiti mmoja uligundua kuwa kiwango cha vifo miongoni mwa watu waliozaliwa hai kilikuwa 8.8 kwa kila 100,000, kinyume na 0.6 kwa 100,000 kutokana na utoaji mimba wa makusudi. Kadhalika, madhara ya kiafya yanayohusiana na ujauzito ikiwa ni pamoja na UTI na matatizo ya afya ya akili yana uwezekano mkubwa wa kuwapata wale wanaochagua kuzaa kuliko wale wanaotoa mimba.

Kutunza mtoto ni jambo kubwa sana kwa rasilimali za kihemko na kiakili hasa kwa wale wanaotoka katika familia zenye kipato duni, au wale ambao hawana mtu wa kuwasaidia kulea mtoto. Watoto waliozaliwa bila kutarajia wana uwezekano mkubwa wa kuingia katika mfumo duni wa matunzo, kupata umaskini, na kuteseka kutokana na hali za afya ya akili kama vile mfadhaiko au wasiwasi. Wazazi wanaozaa bila kutarajia pia wana uwezekano mkubwa wa kuhisi kuto fanikiwa na kupata hisia kali.

Unyanyapaa Karibu Kutoa Mimba Zaidi ya Moja

Kuna unyanyapaa mwingi unao husiana na utoaji mimba, unyanyapaa huwakumba zaidi wale wanaotoa mimba zaidi ya moja. Kuna nadharia kwamba watu wengi wanaotoaa mimba zaidi ya moja wanatumia njia hiyo kama njia yao kuu ya uzazi wa mpango. Kwa hakika, takwimu zinaonyesha kwamba iwe ni mimba ya kwanza au la, wale wanaotaka kutoa mimba wanafahamu chaguzi nyingine zinazopatikana kwao, na hatari za kisaikolojia na kimwili zinazohusiana na utoaji mimba. Hata kama mtu atachagua kutumia utoaji mimba kama njia yake pekee ya uzazi wa mpango, kuna sababu nyingi za kijamii zinaweza kupelekea mtu kufanya maamuzi hayo.

Unyanyapaa wa aina yoyote wa utoaji mimba huongeza ukimya wa kudhibiti uzazi na kuwaweka watu walio na uterasi katika hali ngumu au hatari. Ingawa kitakwimu kutoa mimba zaidi ya moja ni jambo la kawaida, wale wanaofanya chaguo hili wana uwezekano mdogo wa kuzungumza kuhusu uzoefu wao kwa sababu ya kuogopa kutengwa. Utoaji mimba ni taratibu za afya, na si haki watu kulazimishwa kukaa kimya kuhusu maamuzi yao binafsi kuhusu afya zao.

Ili kusaidia kudharau utoaji mimba zaidi ya moja, tunaweza kubadili lugha yetu. Tovuti ya 2PlusAbortions hutoa nyenzo nyingi za jinsi ya kufanya hivi. Kuzungumza zaidi juu ya utoaji mimba sio tu kwamba kunasawazisha uzoefu wa watu lakini pia kunatoa mwanga juu ya ukweli mwingine kuhusu utoaji mimba; utoaji mimba si uzoefu wa pekee bali ni taratibu zinazofanyika miongoni mwa mamilioni ya watu kwa njia nyingi tofauti na kwa watu wengi tofauti. Vivyo hivyo, kuepuka maneno ‘rudia kutoa mimba’ hutusaidia kubadili mawazo yetu kuhusu ni nani anayetaka kutoa mimba zaidi ya moja. ‘Rudia’ inadokeza kwamba aliyepata mimba hajajifunza jinsi ya kujikinga na mimba au hawawezi ‘kuvunja mzunguko wa utoaji mimba’ mambo ambayo si haki wala si kweli. Hatimaye, kuepuka msemo ‘utoaji mimba mara nyingi’ husaidia kuvunja dhana kati ya ‘watu wazuri’ wanaotoa mimba mara moja na ‘watu wabaya’ ambao wanatoa mara nyingi.

Songa mbele

Kutoa mimba zaidi ya moja ni jambo la kawaida sana kuliko watu wanavyoweza kuamini. Ni kwa kujenga utamaduni wa kuzungumza kuhusu utoaji mimba kwa uwazi na uaminifu ndipo unyanyapaa utaanza kusambaratika.

2plusabortions. (2022). Why Would Anyone Have More Than One Abortion? — 2 + Abortions Worldwide. 2 + Abortions Worldwide. Retrieved 11 July 2022, from https://www.2plusabortions.com/why-people-have-abortions.

2plusabortions. (2022). 6 Free & Easy Ways to Fight Stigma — 2 + Abortions Worldwide. 2 + Abortions Worldwide. Retrieved 11 July 2022, from https://www.2plusabortions.com/sixreasons.

Pittman, G. (2012). Abortion safer than giving birth: study. Reuters. Retrieved 11 July 2022, from https://www.reuters.com/article/us-abortion-idUSTRE80M2BS20120123.
Raymond, E., & Grimes, D. (2012). The Comparative Safety of Legal Induced Abortion and Childbirth in the United States. Obstetrics &Amp; Gynecology, 119(2, Part 1), 215-219. https://doi.org/10.1097/aog.0b013e31823fe923

Stone, N., & Ingham, R. (2011). Who presents more than once? Repeat abortion among women in Britain. Journal Of Family Planning And Reproductive Health Care, 37(4), 209-215. https://doi.org/10.1136/jfprhc-2011-0063

Women Help Women. (2018). Let’s talk about the stigma of multiple abortions. Women Help Women. Retrieved 11 July 2022, from https://womenhelp.org/en/page/984/let-s-talk-about-the-stigma-of-multiple-abortions.