Kutokwa na Damu Baada ya Kutumia Tembe za Kutoa Mimba

Kutokwa na Damu Baada ya Kutumia Tembe za Kutoa Mimba

Tembe za kutoa mimba hutumiwa sana kutoa ujauzito. Tembe ya kutoa mimba huwaruhusu watumiaji kutoa mimba wakiwa nyumbani au katika mazingira mengine watakayochagua. Si lazima waende hospitali au kusimamiwa na mtoa huduma wa afya. Zaidi ya hayo, tembe hizi zina ufanisi wa asilimia 95 hadi 99. Kwa hiyo, ni njia bora na rahisi kwa wagonjwa wanaotafuta kutoa mimba 1.

Jinsi Tembe za kutoa mimba zinavyofanya kazi

Tembe za kutoa mimba hujumuisha dawa mbili ambazo hufanya kazi kwa pamoja: mifepristone na misoprostol. Dawa hizi mbili hufanya kazi kwa namna tofauti tofauti ili kutoa mimba.

Mifepristone
Mifepristone hufanya kazi kwa kubadilisha homoni ya projesteroni. Projesteroni ni homoni kuu inayohusika kuandaa mwili kwa ujauzito. Projesteroni hufanya kazi kwenye endometriamu, ambayo ni tishu zinazoweka uterasi. Viwango vya projesteroni vinapo ongezeka, endometriamu huongezeka, na kujenga mazingira ambayo yanaweza kubeba mimba. Tokea hapo, yai lililorutubishwa linaweza kujipandikiza kwenye utando wa endometriamu, kukaa hapo na kukua.

Mifepristone hufanya kazi ya kuzuia projesteroni. Kwa kufanya hivyo, safu ya endometriamu huvunjika. Kuvurugika kwa endometriamu huzuia yai kupandikizwa na kuendelea kuishi, hivyo mimba kutoka 2.

Misoprostol
Dawa ya pili katika “kidonge cha kutoa mimba” ni misoprostol. Misoprostol hutumika kuondoa uterasi baada ya mifepristone kutoa ujauzito. Hufanikisha hili kwa kuamilisha vipokezi kwenye uterasi, na hivyo kusababisha kuongezeka kwa mkazo na nguvu. Mikazo yenye nguvu zaidi husaidia katika kuondolewa kwa tishu. Hatua hii hufanana na kuharibika kwa mimba kwa kuwa inaweza kusababisha maumivu makali ya tumbo 1,3,4.

Nifanyeje kabla ya kutumia vidonge vya kutoa mimba?

Kutoa mimba inaweza kuwa changamoto kimwili na kihisia. Kwa hiyo, kuna mambo machache unapaswa kuzingatia kabla ya kumeza kidonge cha kutoa mimba:

  • Kaa kwenye mazingira huru na salama. Kumeza kidonge cha kutoa mimba mara nyingi husababisha maudhi mbalimbali kama vile kuumwa sana na tumbo na kutokwa na damu. Kukaa mahali pa faragha ambapo utajisikia huru na salama kunaweza kuondoa baadhi ya mifadhaiko inayohusiana na kutoa mimba.
  • Zingatia kuwa na msaidizi. Licha ya changamoto za kimwili, unaweza kukumbana na unyanyapaa wa kifamilia, kitamaduni na kijamii unaohusishwa na utoaji mimba, jambo hili linaweza kukuletea hisia mbaya hivyo ni muhimu kuwa na mtu ambaye anaelewa na kukupa faraja.
  • Andaa zana za kukusaidia kudhibiti hali yako. Kama ilivyoelezwa hapo juu, utoaji mimba kwa kutumia dawa unaweza kusababisha maudhi mbalimbali. Kumeza dawa kama vile dawa za kuzuia maumivu(NSAID) mfano: ibuprofen, au Tylenol inaweza kusaidia kudhibiti maumivu. Kamwe usimeze aspirin, kwani inaweza kufanya utokwe na damu nyingi zaidi. Unaweza kumeza dawa ya kutuliza maumivu dakika 30 kabla ya kutumia misoprostol (dawa ya pili ya kutoa mimba). Pia waweza kutumia taulo maalumu za kike zinazo zalisha joto (heating pad) kukusaidia kukupa unafuu. Ni muhimu pia kuwa na taulo za kike za maxi (taulo za kike zenye uwezo mkubwa wa kunyonya unyevu) kwani kuna uwezekano wa kutokwa damu nyingi.
  • Pata muda wa kupumzika. Madhara ya vidonge vya kutoa mimba yanaweza kudumu kwa siku moja hadi tatu, kutegemeana na wakati ulio meza dawa. Hivyo, hakikisha unapata wakati wa kutosha kwaajili ya kupumzika ili kujenga afya yako5.

Ni nini hufanyika wakati wa kutoa mimba kwa kutumia vidonge?

Vidonge vha kutoa mimba hufanya kazi katika hatua mbili. Katika hatua ya kwanza kidonge cha Mifepristone huzuia ukuaji wa mimba, na kidonge cha misoprostol huondoa uchafu ndani ya uterasi.

Ni muda gani hupita tangu kumeza mifepristone mpaka damu kuanza kutoka?

Watu wengi huanza kutokwa na damu saa moja hadi nne baada ya kutumia misoprostol. Kipindi hiki huambatana na changamoto kubwa sana, kwani mchakato wa kutoa mimba kwa vidonge hufanana na kuharibika kwa mimba. Unaweza kushuhudia mabonge ya damu yakitoka au hata kutokwa na tishu zilizo ganda zenye ukubwa unao lingana na limao. Kwa kawaida, mwilii humaliza kutoa tishu za ujauzito baada ya saa nne hadi tano, lakini inaweza kuchukua muda mrefu zaidi. Kuvuja damu kunapaswa kupungua polepole baada ya tishu za ujauzito kutoka, lakini hali hiyo inaweza kuendelea kwa muda mrefu. Ikiwa utatumia kidonge cha misoprostol (kidonge chapili) na usipo ona damu ndani ya saa 24, wasiliana na mtoa huduma wa afya.

Katika wiki zinazofuata baada ya utoaji mimba, ni kawaida kuendelea kutokwa na damu na uchafu. Unaweza kutumia taulo za kike, kisodo au kikombe cha hedhi ili kudhibiti utokaji wa damu. Faida nyingine ya kutumia taulo za kike katika kipindi hiki ni kujua kiasi cha damu kinacho toka.

Unahisije unapo tumia dawa kutoa mimba?

Licha ya kutokwa na damu, changamoto nyingine kuu ya utoaji mimba kwa kutumia vidonge ni kuumwa na tumbo. Kama ilivyo changamoto ya kutokwa na damu, kuumwa na tumbo kunaweza kudumu kwa saa kadhaa na kupungua baada ya kutolewa kwa tishu za ujauzito. Pia changamoto nyingine ni kuvimba, changamoto hii inaweza kudumu kwa siku nyingine mbili.

Athari zitokanazo na matumizi ya vidonge vya kuzuia mimba hutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine. Athari nyingine unazoweza kupata baada ya kutoa mimba kwa kutumia vidonge ni kama vile;

  • Tumbo kuuma au kutapika
  • Kuharisha
  • Uchovu
  • Kizunguzungu
  • Homa na baridi
  • Maumivu ya matiti na kutoa maji maji

Homa, kichefuchefu, na dalili za baridi zinapaswa kutatuliwa haraka. Hata hivyo, ikiwa dalili zako za homa, kichefuchefu, kutapika, au kuhara zitaendelea kwa zaidi ya saa 24 baada ya kumeza kidonge cha mwisho, unapaswa kutafuta matibabu ya ziada kwani zinaweza kuwa dalili za maambukizi.

Kama ilivyoelezwa hapo mwanzo, dawa za kupunguza maumivu na taulo ya kike yenye joto inaweza kusaidia kupunguza maumivu. Njia nyingine zinazo weza kusaidia kupunguza maumivu ni kama vile;

  • Kumeza dawa za kuzuia kichefuchefu
  • Kusuguliwa mgongoni
  • Kuoga
  • Kuketi kwenye choo

Ikiwa unajisikia vizuri siku inayofuata, unaweza kuendelea na shughuli nyingine za kawaida kama vile kufanya kazi ndogondogo na kuendesha gari. Kamwe usishiriki katika mazoezi magumu au kazi ngumu mpaka siku kadhaa zipite.

Mbali na changamoto za kimwili zinazo sababishwa na matumizi ya kidonge cha kutoa mimba, watu wengi hupata hisia mbalimbali baada ya kutoa mimba. Ingawa wengine hupata hisia nzuri, wapo ambao hupata hisia za majuto au huzuni. Hii ni kawaida kabisa, hata hivyo, ikiwa hisia zako zinaathiri maisha yako ya kila siku, ni vema kuzungumza na mtaalamu wa afya ya akili 6.

  1. The Facts on Mifepristone. (2019). Retrieved September 4, 2022, from https://www.plannedparenthood.org/uploads/filer_public/42/8a/428ab2ad-3798-4e3d-8a9f-213203f0af65/191011-the-facts-on-mifepristone-d01.pdf
  2. Autry, B. M., & Wadhwa, R. (2022). Mifepristone. In StatPearls. StatPearls Publishing. http://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK557612/
  3. Misoprostol. (n.d.). Retrieved September 4, 2022, from https://go.drugbank.com/drugs/DB00929
  4. Autry, B. M., & Wadhwa, R. (2022). Mifepristone. In StatPearls. StatPearls Publishing. http://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK557612/
  5. Here’s how to prepare for an abortion pill dose. (2022, April 25). Well+Good. https://www.wellandgood.com/abortion-pill/
  6. How does the abortion pill work? | Abortion pill function. (n.d.). Retrieved September 4, 2022, from https://www.plannedparenthood.org/learn/abortion/the-abortion-pill/how-does-the-abortion-pill-work