Utoaji mimba nyumbani, unaojulikana pia kama uavyaji mimba wa kimatibabu, ni maarufu miongoni mwa watu ambao hawataki kuendelea na ujauzito wao kwa vile ni utaratibu mzuri na salama sana, ambao unaweza kufanywa bila kulazimika kwenda kituo cha afya.
Watu walio na ujauzito wa chini ya wiki 13 wanaweza kufuata mwongozo wa uavyaji mimba nyumbani unaotolewa na safe2choose, ambao uliundwa na wataalamu wa afya.
Kwa kuongezea, njia za moja kwa moja za mawasiliano zimeanzishwa na washauri wa uavyaji mimba ambao wanaweza kukupa uandamani, kabla, wakati, au baada ya kutoa mimba.