Ukubwa wa maandishi
safe2choose

Shirikiana na Watoa Huduma za Utoaji Mimba Duniani kwa Upatikanaji wa huduma Salama

World map illustration showing two women in circles, one in a yellow floral dress, one in a lab coat, linked to represent global abortion provider partnerships with safe2choose

Hapa safe2choose, tumejikita kuhakikisha kila mtu anapata taarifa sahihi na huduma salama za afya ya uzazi. Dhamira yetu ni kutoa msaada jumuishi, wa huruma, na wa siri kwa wale wanaotafuta njia salama za utoaji mimba, tukiwawezesha kufanya maamuzi yaliyo sahihi kuhusu afya na ustawi wao.

Kwa kushirikiana na safe2choose, unaweza kusaidia kuendeleza dhamira yetu na kuchangia katika mtandao wa kimataifa wa watetezi wa afya ya uzazi waliojitolea kuunda dunia salama yenye afya njema.

Video Background

VIDEO YA RUFAA

Video Background

VIDEO WANGARI

Video Background

VIDEO NAFULA

SHIRIKIANA NASI

Jiunge Nasi na Uwe Sehemu ya Mtandao Wetu wa Watoa Huduma za Utoaji Mimba

Jiunge na mtandao wa kimataifa wa watoa huduma wa utoaji mimba wanaofanya kazi kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi na kijinsia kwa kila mtu duniani. Kuwa sehemu ya mtandao wetu wa rufaa ni rahisi. Tunakaribisha watoa huduma za afya, makundi ya utetezi, na mashirika yanayoshiriki dhamira yetu ya kutetea haki za uzazi na huduma salama za utoaji mimba.

Hatua ya 1:

Wasiliana nasi kupitia partnerships@safe2choose.org kuonesha nia yako ya kujiunga na mtandao. Tutafurahi kusikia kutoka kwako!

Hatua ya 2:

Timu yetu itawasiliana nawe ili kutathmini ulinganifu na kujadili fursa za ushirikiano.

Hatua ya 3:

Shirikiana na safe2choose ili kuongeza upatikanaji wa huduma za afya ya uzazi katika eneo lako.

Kwanini Ushirikiane na safe2choose?

Ufikiaji wa Kimataifa, athari za ndani

safe2choose inakuza ufikiaji wa kimataifa na athari za ndani, ikipanua upatikanaji wa huduma salama za utoaji mimba na taarifa za kuaminika kuhusu afya ya uzazi ili kuwawezesha jamii duniani kote.

Mwongozo na Msaada wa Kitaalamu

Timu yetu ya washauri na watetezi waliyojifunza kitabibu hutoa huduma binafsi ya kitaalamu inayojikita katika heshima na mbinu bora za matibabu, ikiwasaidia watu katika kila hatua.

Jukwaa bunifu la kidijitali

safe2choose hutumia teknolojia ya kisasa kutoa ushauri mtandaoni na taarifa sahihi kuhusu utoaji mimba kwa njia ya siri, kwa wakati, na kulingana na mahitaji ya mtu binafsi.

Rasilimali za Kina

Jukwaa letu linawezesha watu kwa kutoa miongozo ya hatua kwa hatua, video, na zana shirikishi, likiwapa maarifa ya kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya yao.

Aina za Ushirikiano

Tunakaribisha fursa mbalimbali za ushirikiano, zikiwemo:

Illustration of two women against a teal background. One wears medical scrubs with hands on hips, and the other in a casual outfit pointing right representing types of partnerships.
Light blue open padlock icon representing access. Invitation to collaborate in expanding safe abortion services worldwide.

Kupanua Upatikanaji wa Huduma za Utoaji Mimba

Shirikiana nasi ili kupanua upatikanaji wa huduma salama za utoaji mimba na kuboresha matokeo ya afya ya uzazi duniani kote.

Icon of two overlapping documents symbolizing partnership to promote reproductive health rights and safe, legal, affordable abortion access.

Kutetea Haki za Afya ya Uzazi

Shirikiana nasi kutetea na kuendeleza haki za afya ya uzazi, kuhakikisha kila mtu anapata huduma za utoaji mimba salama, halali, na nafuu.

Blue hand icon holding a heart, symbolizing efforts to promote sexual education and reproductive health through research and campaigns.

Kukuza Uelewa kuhusiana na Afya

Jiunge nasi katika kukuza elimu ya kina ya masuala ya kijinsia na uelewa wa afya ya uzazi kupitia utafiti, warsha, na kampeni za kidijitali.

Two teal overlapping circles symbolizing people, representing corporate partnerships to improve abortion access and reproductive health.

Ushirikiano wa Kibiashara kwa Mchango Chanya

Tunakaribisha ushirikiano na kampuni ili kuboresha afya ya kijinsia na uzazi kupitia suluhisho bunifu, ufadhili wa miradi, au kampeni za pamoja zinazolenga upatikanaji wa huduma za utoaji mimba.

Mtandao Wetu wa Rufaa wa Kimataifa

Logo

safe2choose inadumisha mtandao wa kimataifa wa watoa huduma waliothibitishwa wanaotoa huduma za utoaji mimba kwa ukamilifu, bila hukumu, kuhakikisha watu duniani kote wanapata msaada binafsi wa afya ya uzazi salama na wenye heshima. Mtandao wetu unajumuisha zaidi ya nchi 80, ukiwa na aina mbalimbali za watoa huduma za afya, mitandao ya kikanda na kimataifa, pamoja na makundi ya uandamani, wote wakiwa wamejitolea kutoa huduma za hali ya juu.

Mtandao wetu wa rufaa huwaunganisha watu na huduma mbalimbali, zikiwemo upatikanaji wa tembe za kutoa mimba na utoaji mimba wa hospitalini, mpango wa uzazi , msaada wa kisheria, na ushauri wa kihisia, kuhakikisha mbinu jumuishi ya afya ya uzazi.

MSI Reproductive Choices logo in blue and grey, representing global reproductive health organization.

MSI Reproductive Choices

IPPF logo with globe icon and blue lettering, representing global reproductive rights network.

International Planned Parenthood Federation (IPPF)

Carafem logo in pink and teal, representing the U.S.-based reproductive health provider

Carafem

Women on Web logo in pink with hexagonal symbol, representing the global telemedicine abortion service

Women on Web

Mchakato Wetu wa Rufaa ya Utoaji Mimba

Washauri wa safe2choose hutoa msaada kupitia mazungumzo ya moja kwa moja na barua pepe kwa wale wanaotafuta njia salama za utoaji mimba. Wanaohitaji msaada wa ziada, hupatiwa rufaa ya kwenda kwa watoa huduma walio thibitishwa walio karibu nao baada ya uchunguzi wa awali na wa kina. Kwa kushirikiana na washirika walioko kwenye maeneo husika, safe2choose inahakikisha upatikanaji wa huduma kamili za utoaji mimba.

Kutambua changamoto za kiusalama zinazohusiana na huduma za utoaji mimba, hasa katika maeneo ambako utoaji mimba umepigwa marufuku, tunahifadhi taarifa zote katika kanzidata iliyo na usimbaji fiche wa hali ya juu ili kuhakikisha faragha na ulinzi.

Tumejikita katika kudumisha ubora wa mtandao wetu kwa kuwasaidia watoa huduma kwa nyenzo za mafunzo ya mtandaoni na kuhakikisha kuwa wana sifa kamili katika utoaji wa huduma za utoaji mimba na utoaji wa taarifa sahihi.

Download Default IconPakua Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara kuhusu mchakato wa rufaa wa safe2choose.

Mchakato wa Rufaa ya safe2choose kwa Hatua Tano:

1

Kuanzisha Mawasiliano:

Mtumiaji hutuma barua pepe au kuanzisha mazungumzo kupitia tovuti. Taarifa zote zinazotolewa huhifadhiwa kwa usiri na faragha kamili.

2

Uchunguzi:

Washauri hufanya uchunguzi wa kina wa mtumiaji.

3

Kutambua Mahitaji:

Washauri hufanya kazi na mtumiaji kubaini mahitaji yake na kumpa msaada, mara nyingi ukiwemo mwongozo kuhusu utoaji mimba salama.

4

Rufaa:

Iwapo inahitajika, washauri humrejelea mtumiaji kwa washirika walioko eneo husika kwa huduma kama vile tembe, huduma ya hospitalini, au msaada mwingine.

5

Huduma na Msaada:

Washirika wa safe2choose humkaribisha mtumiaji aliyepelekwa kwa huruma, kuhakikisha anapata taarifa muhimu, na kumpatia huduma ya hali ya juu.

Kile ambacho safe2choose inatoa kwa Watoa Huduma wa Utoaji Mimba:

Faida kuu za kujiunga na mtandao wetu:

Ufikiaji wa Kimataifa:

Kuwa sehemu ya mtandao wetu wa rufaa unaoaminika, ukijiunga na maelfu ya watu wanaotafuta huduma za afya ya kijinsia na uzazi kupitia rufaa za moja kwa moja.

Kushiriki Maarifa:

Jiunge na mtandao unaokua wa watoa huduma za utoaji mimba duniani kote ili kubadilishana mawazo, kushiriki mbinu bora, na kushiriki fursa za kujenga uwezo.

Upatikanaji wa Mafunzo:

Pata mafunzo ya mtandaoni bure yanayolenga kufundisha mbinu salama za utoaji mimba na ujuzi wa ushauri.

Rasilimali:

Pokea nyenzo za Habari, Elimu na Mawasiliano bila malipo ili kusaidia vifaa vyako.

Ushirikiano wa Utetezi:

Shiriki katika juhudi za kimataifa za kupambana na unyanyapaa na kupunguza vizuizi kwa huduma za afya ya uzazi.

Mafunzo ya Mtandaoni ya Utoaji Mimba

Ushuhuda wa Ushirikiano wa Maana na Athari Chanya

"Kuna uhitaji wa wazi wa taarifa zinazosaidia watu katika maamuzi yao ya afya ya uzazi – na takwimu kutoka MSI na safe2choose zinaonyesha kuwa mtandao unarahisisha hilo – hivyo tunashirikiana kuhakikisha kwamba wanaotumia safe2choose wanaweza kuelekezwa kwenye huduma bora za utoaji mimba salama na huduma baada ya utoaji mimba kupitia MSI, pale inapowezekana."

Soma makala kamili

"Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2021, ushirikiano wa safe2choose na IPPF umeandikisha watoa huduma 300 kutoka Mashirika Wanachama wa IPPF katika nchi saba barani Afrika na Asia. Katika miaka miwili ya kwanza, safe2choose ilielekeza zaidi ya wateja 3,600 kwenye vituo vya IPPF, ambako walipokea huduma bora za utoaji mimba. Ushirikiano huu umeimarisha kwa kiasi kikubwa mfumo wa huduma za utoaji mimba, na kuhakikisha huduma kamilifu na isiyo na shaka kwa wanawake."

Soma makala kamili

"Women on Web na safe2choose wameungana kuelimisha jamii kuhusu jinsi ya kupata taarifa sahihi na salama mtandaoni kuhusu utoaji mimba kupitia kampeni ya "Kaa na Afya, Kaa na Taarifa Unapotumia Tembe za Utoaji Mimba." Mpango huu unatoa vifaa kamili, ushauri, na rasilimali kuhusu kulinda usalama na faragha yako unapovinjari mtandaoni, mwongozo wa jinsi ya kupata tembe za utoaji mimba, pamoja na mbinu za kuepuka matapeli wanaouza tembe zisizo salama. Mwaka 2022, mashirika haya mawili yalizindua ukurasa maalum wa kukusanya maoni kutoka kwa watumiaji kuhusu watoa huduma au wauzaji wa vidonge bandia vya utoaji mimba."

Angalia video

Uko Tayari Kufanya Mabadiliko?

Jiunge na mtandao wetu wa rufaa leo ili kushirikiana katika kujenga dunia ambayo kila mtu anaweza kupata huduma za utoaji mimba zilizo salama, zenye heshima, na zinazotegemea ushahidi wa kisayansi.

Three diverse women connected around a globe; one holds a phone, another wears a lab coat holding a tablet, and the third holds a beaker, symbolizing global collaboration.