Nikiwasiliana nanyi kupitia kwa mazungumzo ya moja kwa moja au barua pepe, ni nani atajibu?

Mawasiliano yetu hushughulikiwa na timu yetu ya kike iliyopewa mafunzo ya kusaidia na kuheshimu uamuzi wa wanawake na watu wasiozingatia jinsia katika hali ya mimba isiyohitajika. Wamepewa mafunzo ya kina kuhusu uavyaji mimba wa kimatibabu, na hupewa mafunzo tena baada ya kipindi fulani kuhakikisha kuwa wana taarifa za hivi-punde kukuelekeza. Ikiwa unahitaji ushauri wa kipekee kwa sababu yoyote, washauri wanaweza kushauri timu yetu ya utabibu ili kukupa msaada kwa njia bora zaidi iwezekanavyo.

TAZAMA MASWALI ZAIDI

*Hakuna kinachotolewa hapa kinapaswa kudhaniwa kuwa ushauri wa kitaalam na hakuna dawa / tembe zinazopaswa kutumiwa bila agizo kutoka kwa mtaalamu aliye na leseni / aliye sajiliwa anayestahili kuagiza dawa hiyo katika mamlaka yako ya karibu.