Nitajuaje safe2choose ni shirika halisi?

Tunaelewa kuwa ni vigumu sana kuamini tovuti, hasa kwa kuwa kuna taarifa nyingi za uongo katika mtandao. Tunataka ujue kuwa safe2choose imejitolea kuongeza nafasi ya kufikia taarifa za kweli ili wanawake kote duniani waweze kuwa na utoaji mimba salama kwa kutumia tembe.

Taarifa zote tunazopitisha katika tovuti yetu na kupitia kwa timu yetu ya ushauri zimejikita kwenye mapendekezo ya wataalamu wa mashirika ya utabibu ya kimataifa katika uavyaji mimba. Inapofaa, utaona mashirika haya yakirejelewa katika tovuti ya safe2choose ili uweze kuelewa asili zetu zenye sifa

Unaweza kuwasiliana nasi wakati wowote ikiwa una maswali. Tunatoa habari kuhusu tembe za kuavya mimba, na tunapatikana kukupa msaada kabla, wakati wa na baada ya kutoa mimba.

Kila mara safe2choose hutajwa katik habari, angalia kitengo hiki ili kujua mengi kutuhusu.

TAZAMA MASWALI ZAIDI

*Hakuna kinachotolewa hapa kinapaswa kudhaniwa kuwa ushauri wa kitaalam na hakuna dawa / tembe zinazopaswa kutumiwa bila agizo kutoka kwa mtaalamu aliye na leseni / aliye sajiliwa anayestahili kuagiza dawa hiyo katika mamlaka yako ya karibu.