Utoaji Mimba nchini Uganda

Uavyaji Mimba nchini Uganda: Sheria, Upatikanaji, na Huduma ya Afya

Nchini Uganda, zaidi ya asilimia hamsini ya mimba hazijapangwa, na takriban theluthi moja ya mimba hizo hutolewa. Utafiti uliofanyika mnamo mwaka Elfu mbili na tatu ulikadiria kuwa takriban mimba hamsini na nne hutolewa kwa kila wanawake elfu moja wanaopata mimba nchini Uganda.

Licha ya matukio mengi ya mimba zisizo tarajiwa, huduma salama ya utoaji mimba imezuiliwa kisheria nchini Uganda. Hii inafanya kuwa vigumu sana kwa wanawake kutoa mimba kwa njia salama, na kusababisha wengi kugeukia njia zisizo salama za utoaji mimba (1). Makala hii itajadili kwa kina kuhusu utoaji mimba nchini Uganda.

Utoaji Mimba nchini Uganda

Kwa bahati mbaya, nchi ya Uganda inazuia kisheria utoaji mimba isipokuwa katika mazingira maalumu. Kwa mfano, kulingana na Mwongozo wa Sera ya Kitaifa wa elfu mbili na sita, utoaji mimba unaruhusiwa tu katika kesi za ubakaji, matatizo ya uzazi, maambukizi ya VVU, au ikiwa ujauzito huo ulipatikana baada ya ndugu wa damu kujamiiana (1). Kando ya hayo, hakuna mtu anayesemekana kuwa na haki ya kutoa mimba isipokuwa kama ameruhusiwa kisheria, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Uganda (1995), Kifungu cha ishirini na mbili (2). Zaidi ya hayo, Sheria ya Kanuni ya Adhabu inaendelea kueleza kwamba mtu yeyote anayetoa zana za kutekeleza utoaji mimba, iwe kwa dawa au kwa njia nyinginezo, anatenda kosa (2).

Sheria hizi zina utata, na hupelekea wanawake wengi na watoa huduma kusitasita linapokuja suala la kutoa mimba (2). Matokeo ya kisheria huleta hofu kwa wanawake na watoa huduma na kuzuia upatikanaji wa huduma salama ya utoaji mimba.

Njia za utoaji mimba nchini Uganda

Inakadiriwa kuwa kwa kila wanawake Kumi na tisa nchini Uganda, mmoja huwa ametoa mimba. Licha ya kuwa utoaji mimba ni jambo la kawaida, vikwazo vya kisheria vinavyozunguka utoaji mimba huzuia watu kupata huduma salama ya utoaji mimba.

Kwa sababu ya tishishio la kisheria, wahudumu wa afya, hata wale walio na uzoefu wa kutoa mimba, hulazimika kufanya zoezi hili kwa siri na kwa gharama kubwa. Hivyo, wanawake katika maeneo ya vijijini au wale wenye kipato duni huwa na uwezekano mdogo wa kutoa mimba kwa kutumia njia salama. Watu kama hao wanaweza kujaribu kutoa mimba wenyewe au kutafuta msaada kwa watu wasio na ujuzi ambao wanaweza kutumia njia zisizo salama. Hii inaweza kuwa hatari sana, na Wizara ya Afya nchini Uganda inaripoti kwamba masuala yanayo husiana na utoaji mimba ni asilimia Ishirini na sita ya vifo vyote vya uzazi nchini Uganda (1). Kwa bahati mbaya, kati ya wanawake wanaopata matatizo ya utoaji mimba, ni asilimia hamsini pekee wanaweza kupata huduma ya matibabu (3).

Pindi utoaji mimba salama ufanyikapo nchini Uganda, hufanywa kwa njia zifuatazo: njia ya ufyonzaji (MVA), vidonge vya kutoa mimba (Misoprostol pekee/Mifepristone na Misoprostol), au njia za upanuaji na ukwanguaji (D&C) (4). Kila moja ya njia hizi imeelezewa kwa kina hapa chini:

 • Njia ya ufyonzaji (MVA). Inapotumika njia ya ufyonzaji , mtoa huduma hutumia sindano maalum ili kufyonza. Kisha vacum (utupu) na bomba nyembamba, huwekwa ndani ya uterasi. Mashine hufyonza ili kuondoa mimba kutoka kwenye mfuko wa uzazi (uterasi) (5).
 • Vidonge vya kutoa mimba. Mariprist na MA-Kare ni pakiti za vidonge vya kutoa mimba ambazo hujumuisha kidonge kimoja cha Mifepristone na vidonge vinne vya Misoprostol. Mifepristone hutoa mimba kwa kuzuia homoni muhimu za ukuaji wa mimba; Misoprostol husababisha mwili kusafisha tumbo la uzazi.
 • Njia za upanuaji na ukwanguaji (D&C). Kwakutumia njia ya upanuaji na ukwanguaji (D&C), mtoa huduma hutanua cervix (shingo ya kizazi) kisha hutumia vifaa maalumu vya upasuaji kutoa tishu za mimba toka kwenye kizazi (6).

Gharama za utoaji Mimba nchini Uganda

Kwasababu ya usiri unao ambatana na utoaji mimba nchini Uganda, watoa huduma za afya wanaotoa huduma ya utoaji mimba huwa na gharama kubwa. Takwimu za mwaka 2003, zinaonesha kuwa gharama inakadiriwa kuwa kati ya Dola Ishirini na tano ( $25) mpaka Dola Themanini na nane ( $88) endapo zoezi litafanywa na daktari, ikiwa litafanywa na mkunga au muuguzi basi gharama huwa kati ya Dola kumi na nne ( $14) hadi Dola Thelathini na moja ( $31) na endapo litafanywa na mganga wa kienyeji basi litagharimu Dola Kumi na mbili ($12) mpaka Dola Thelathini na nne ( $34). Endapo mtu atatoa mimba mwenyewe, gharama zinakadiriwa kuwa kati ya Dola Nne ($4) hadi Dola Kumi na nne ( $14).

Ni muhimu kutambua kwamba kuna gharama za ziada zinazohusiana na matibabu baada ya utoaji mimba, hususa ni zile zinazotokea kutokana na utoaji mimba usio kamili. Madhara mengine makubwa yanaweza kutokea hasa wakati utoaji mimba unapofanywa kwa njia isiyo salama. Madhara hayo ni kama vile maambukizi katika via vya uzazi (sepsis), michubuko, vitobo na mshtuko. Hii huongeza mzigo wa ziada wa kifedha na kiafya kwa mtu binafsi.

Huduma baada ya kutoa mimba pia huleta mzigo mkubwa kwa nchi ya Uganda, takriban dola milioni kumi na nne (14) za Kimarekani hutumika kila mwaka katika huduma hizi(1).

Kliniki zinazo patikana

Kuna kliniki chache zinazojulikana hadharani nchini Uganda zinazoweza kusaidia katika suala la uzazi wa mpango, afya ya uzazi, na huduma za utoaji mimba. Mfano wa kliniki hizo ni Marie Stopes UG. Marie Stopes UG inatoa huduma za uzazi wa mpango, upimaji na matibabu ya magonjwa ya zinaa, huduma za uzazi, na matibabu baada ya kutoa mimba.

Ikiwa unatafuta huduma za utoaji mimba au matibabu baada ya kutoa mimba nchini Uganda, wasiliana na safe2choose ili kuunganishwa.

Mambo ya kuzingatia

Sheria kali zinazohusu utoaji mimba nchini Uganda, licha ya hitaji kubwa la huduma hiyo miongoni mwa wanawake wa Uganda, zimeendeleza matukio ya utoaji mimba katika hatari kubwa. Hivyo basi, huduma salama za utoaji mimba lazima zipatikane kwa wanawake wote ili kupunguza hatari ya madhara na vifo vinavyotokana na utoaji mimba usio salama.

Ikiwa unaishi Uganda na unatafuta huduma za utoaji mimba, wasiliana na washauri wetu kwa safe2choose ili kuunganishwa na nyenzo unazohitaji.

 1. “Abortion in Uganda.” Guttmacher Institute, 2013, www.guttmacher.org/sites/default/files/pdfs/pubs/FB-Abortion-in-Uganda.pdf. Accessed November 2023.
 2. “Uganda’s Abortion Provisions.” Center for Reproductive Rights, reproductiverights.org/maps/provision/ugandas-abortion-provisions/. Accessed November 2023.
 3. Mulumba, M., et al. “Access to safe abortion in Uganda: Leveraging opportunities through the harm reduction model.” National Library of Medicine, 2017, hpubmed.ncbi.nlm.nih.gov/28455836/. Accessed November 2023.
 4. Kagaha, A. & Manderson, L. “Medical technologies and abortion care in Eastern Uganda.” ScienceDirect, 2020,
  www.sciencedirect.com/science/article/pii/S0277953620300320. Accessed November 2023.
 5. “Vacuum Aspiration for Miscarriage: Care Instructions.” MyHealth Alberta,  myhealth.alberta.ca/Health/aftercareinformation/pages/conditions.aspx?hwid=abs1230#:~:text=With%20manual%20vacuum%2C%20the%20doctor,suction%20to%20remove%20the%20tissue. Accessed November 2023.
 6. “Dilation and curettage (D&C) .” Mayo Clinic, www.mayoclinic.org/tests-procedures/dilation-and-curettage/about/pac-20384910. Accessed November 2023.