Je! kuna tofauti gani kati ya gharama kati ya utoaji mimba kwa njia ya kufyonza na tembe za kutoa mimba?

Kwa ujumla, njia ya kufyonza itakuwa ya gharama kubwa kuliko utoaji mimba na tembe. Hii ni kwa sababu wakati mwingine inahitaji upimaji wa ziada, na inahitaji daktari mwenye ujuzi kutekeleza utaratibu. Kwa hivyo, gharama hutofautiana sana kulingana na eneo lako la kijiografia, upatikanaji wa rasilimali, eneo la utoaji mimba (kliniki au hospitali), umri wa ujauzito, na sheria zinazohusu utoaji mimba.

*Hakuna kinachotolewa hapa kinapaswa kudhaniwa kuwa ushauri wa kitaalam na hakuna dawa / tembe zinazopaswa kutumiwa bila agizo kutoka kwa mtaalamu aliye na leseni / aliye sajiliwa anayestahili kuagiza dawa hiyo katika mamlaka yako ya karibu.