HUDUMA SALAMA ZA KUAVYA MIMBA KAMA MOJA WAPO YA HAKI ZA KIJINSIA NA UZAZI

HUDUMA SALAMA ZA KUAVYA MIMBA KAMA MOJA WAPO YA HAKI ZA KIJINSIA NA UZAZI

Mwandishi: Miss Lewis

Huduma salama za kuavya mimba ni  changamoto ambalo limewakumba halaiki ya wanawake na wasichana wenye umri mdogo, katika maeneo mengi tofauti ya kijiografia, dhidi ya vile tuwazavyo.

Abdul na Rita walikuwa wapenzi tangu utotoni waliotengwa na masafa marefu. Hatimaye, baada ya miaka na mikaka, walijipata wakiishi katika eneo moja, wote wakiwa washakomaa kiakili na kimwili. Sauti ya mwanashati ilikuwa kina, kionja mchuzi, masharubu na ndevu zimeenea, mabega mapana na kwa hakika macho yake yalikuwa ya kupendeza Zaidi. Kidosho naye alikuwa Mungu wa kike machoni pake Abdul, mmoja ambaye alitamani sana kumkumbatia ili angalau aweze kukishika kile kiuno cha nyigu.

Usiku mmoja maalum, wote wawili walijipata katika jaribu. Joto la wakati huo liliwazidi nguvu kiasi kwamba walisahau kutumia kinga. Haikuwachukua  muda mrefu baadaye kabla ya wao kujipata na kifaa cha kupima ujauzito kilichokuwa na mistari miwili. Wasiwasi na hofu uliwakumba maanake walikuwa wachanga sana kwa jukumu kama hili na pia walikuwa bado hawajawa huru. Waliamua kutafuta msaada wa huduma salama ya kuavya mimba kutoka kwa duka la dawa la nyumbani.

Asili yao, tamaduni, dini, wazazi na kadhalika, vilikuwa vipengele maishani mwao ambavyo vilikuwa vizuizi kwa wapenzi hao wawili kuwa pamoja katika ndoa. Unyanyapaa uliosubiri kuwafuata ungekuwa mzigo mzito mno kwao, ambao hawangeweza kuustahimili na ungesababisha kuzorota kwa afya zao, kwa hali hii, kiakili na kisaikolojia.

LAITI NINGALIKUWA NA UJUMBE SAHIHI WA NINGEKOPATA HUDUMA SALAMA YA KUAVYA MIMBA

Siku mbili za kukosa kulala baadaye, walishauriwa wangepopata usaidizi katika mji jirani. Baada ya mikopo michache, kuuza mali yao kadhaa na kuweka hela zao za chajio, walipata hela za kutosha za kufunga safari na kupata usaidizi. Kwa hisia mchanganyiko walienda kwa duka la dawa walilotumwa. Walisubiri wateja waliokuwa mle ndani wahudumiwe ili mja hata mmoja asije akajua walichokuwa wakikitaka pale. Mda mfupi baada ya kunong’ona hapa na majibu pale, waliulizwa warudi wakati wa kufunga ili halaiki ya watu iwe imepungua, kisa na maana, huduma salama za kuavya mimba huchukua mda mrefu.

Ilibidi wamemudu njaa, uchovu, jasho na unyogovu wakisubiri. Walienda na kuketi kwenye bustani ya umma na kula mkate, kishirikishi chupa ya maji, wakisubiri miadi yao ya jioni. Baada ya kile kilichoonekana kama umilele, walipewa bahasha iliyokuwa na vidonge vichache na kuamuriwa waviingize ndani ya uke wa Rita, kabla ya kula chajio na kulala. Furaha iliwajaa na wakawashukuru wafamasia wale kisha wakarudi nyumbani ili waanze matibabu. 

Rita aliamka ghafla usiku wa manane akiwa na uchungu mkuu wa hedhi ambao hakuweza kuustahimili. Alikuwa amepanda damu hadi kwenye matandikio na kabla kukuche, walikuwa tayari wakitumia godoro, kwani taulo za hedhi hazingeweza kushika damu tena. Hii hali iliwalazimisha wakimbilie hospitali ya umma kwa huduma.  Walipata kuhudumiwa na kupewa maelezo na daktari kuhusu jinsi ya kujitunza baada ya kuavya mimba.  

Ni jambo la kushangaza na kusikitisha kwamba serikali inaruhusu hospitali kutoa huduma za utunzaji wa shida zinazotokana na kuavya mimba ilhali huduma bora na salama za uavyaji mimba ni marufuku.  Ingekuwa jambo la maana kama serikali ingeruhusu wanawake na wasichana kupata huduma bora na salama za uavyaji mimba kwani kukiwepo hizi huduma basi hakutahitajika huduma za utunzaji wa shida zinazotokana na kuavya mimba.

HUDUMA SALAMA ZA KUAVYA MIMBA KATIKA ENZI ZA TEKNOLOJIA

Hii ndio hali ya sasa katika nchi nyingi ambazo zinajumuishwa na changamoto kadha wa kadha katika vita vya utetezi wa haki za kijinsia na uzazi katika kupata huduma salama za kuavya mimba. Miongoni mwa hizi changamoto huwa: unyanyapaa, tamaduni za kuteleza, sera mbaya na sheria zinazokataa watoa huduma wa afya, kuwapa wanawake habari na huduma. Mwishowe hii imesababisha wahudumu bandia kuteka nyara kazi za wahudumu walio na habari sahihi na mafunzo. Matokeo ya haya yote imekuwa kuongezeka kwa vifo vya wasichana na kina wanawake, viwango vya juu vya utegemezi na hatimaye kudhoofika kwa hali ya uchumi ya kijamii. 

Uaviaji mimba kwa njia ya matibabu kwa kawaida hujulikana kama kuavya mimba kwa tembe. Ikiwa utatumia tembe za kuavya mimba utashuhudia uvujaji damu na msokoto. Dalili ni sawa na kipindi chako cha hedhi au kama unapopoteza mimba. Hii njia ni salama na imeidhinishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO). Kwa kufuata maagizo sahihi wanawake wanayo fursa ya kuavya mimba kwa faraja ya nyumbani mwao. Ni njia rahisi inayosaidia kuepuka vikwazo vingi vinavyokumba wengi wanaotaka kuavya mimba kwa njia salama.

Isitoshe, kunayo  mashirika ambayo yamejitolea mhanga katika utetezi wa kuhakikisha kuwa hakuna msichana au mwanamke anayekosa huduma salama za kuavya mimba. safe2choose ni shirika ambalo liko katika mstari wa mbele katika kusambaza habari zinazofafanua mbinu salama za kuavya mimba. Wao hufafanua ujumbe wa jinsi ya kutumia dawa na wakati hizo dawa zinafaa kutumika, kipimo, dalili zinazotarajiwa, athari mbaya, tahadhari na ishara za onyo. Tembelea tovuti yao upate kuongea na mshauri kwa njia ya moja kwa moja au kwenye barua pepe info@safe2choose.org atakaye kuunganisha na mhuduma upate usaidizi.