Tembe ya kutoa mimba dhidi ya utoaji mimba kwa upasuaji: Ni ipi sahihi kwangu?

Katika jedwali hili, tunalinganisha uzuri na ubaya wa utoaji wa mimba kwa kutumia tembe na utoaji mimba kwa njia ya kunyonya au kufyonza.

safe2choose inasisitiza njia hizi mbili salama ndani ya wiki 11 za kwanza za uja uzito, na ni kwa wanawake kuamua ni ipi bora kwao kulingana na bajeti yao, upatikanaji, umri wa mimba, na chaguo la kibinafsi.

Kuchagua njia bora ya kutoa mimba

Utoaji wa Mimba wa kimatibabu (MA) au Utoaji mimba na tembe
Je! kutoa mimba kwa kutumia tembe ni nini? ( utoaji wa mimba wa kimatibabu)
Ufafanuzi Utoaji wa mimba kwa matibabu (wakati mwingine huitwa utoaji wa mimba kwa tembe) ni njia salama sana ya kutoa mimba ambayo mwanamke hutumia tembe nyumbani kumaliza ujauzito usiohitajika.
Kuna aina mbili salama za kutoa mimba kwa matibabu: kutumia Mifepristone pamoja na Misoprostol, au kutumia Misoprostol peke yako. safe2choose inakubali njia zote hizi za utoaji mimba kwa kimatibabu kwa ujauzito wenye wiki kumi na moja [1], na maelezo yanaweza kupatikana hapa.

Kutoa mimba kwa upasuaji au kwa njia ya kunyonya au kufyonza (MVA)
Je! njia ya kunyonya au kufyonza ni nini? ( kutoa mimba kwa upasuaji)
Ufafanuzi Njia ya kunyonya au kufyonza (MVA) ni njia salama sana ya kutoa mimba kwa ujauzito katika trimester ya kwanza, na / au mapema trimester ya pili hadi wiki kumi na nne ya ujauzito. Kikomo cha umri wa mimba kwa MVA mara nyingi hutegemea kliniki, na vile vile mtoaji wa huduma ya afya anayefanya utaratibu. [3]
MVA inafanywa kwenye kliniki na mhudumu wa afya aliyefundishwa. Unaweza kupata maelezo zaidi juu ya utaratibu hapa.

Utoaji wa Mimba wa kimatibabu (MA) au Utoaji mimba na tembe
Ubaya na uzuri wa utoaji wa mimba na tembe (utoaji mimba wa kimatibabu) [1], [2]
UfanisiAsilimia 95 yenye ufanisi
UsalamaSalama sana
Kupima ujauzitoJaribio la mawimbi sauti haihitajiki
Kikomo cha umri wa mimbaInaweza kutumika hadi wiki kumi na moja ya ujauzito
Ili kujua juu ya umri wako wa mimba yako, tembelea ukurasa wetu ambao una Uthibitisho wa Mimba na kikokotoo.
MahaliInafanyika katika faragha ya nyumba au mahali popote mwanamke anahisi ako salama
mtekelezajiInaweza kufanywa na mwanamke mwenyewe.
MudaWakati wa kukamilisha mimba na tembe unaweza kuwa siku chache hadi wiki chache.
MadharaDamu yaweza kuwa yatoka na kupotea wakati wa kutokwa na damu kwa wiki mbili au zaidi.
Kukandamizwa kwa tumbo la uzazi kunaweza kuja na kupotea kwa mda wa wiki mbili
Shida na hatariUwezekano wa hatari ni pamoja na: kutokwa na damu nyingi, maambukizi, kuendelea kwa ujauzito, na utoaji mimba usio kamili.
GharamaKwa ujumla, MA ni ghali kuliko MVA kwa sababu inajumuisha ununuzi wa tembe.Jaribio la mawimbi sauti, ambalo linaweza kuwa na gharama kubwa, halihitajiki. Gharama halisi ya MA itatofautiana sana kulingana na eneo la jiografia na ikiwa tembe zinapatikana au karibu na duka la dawa, au kwa maagizo tu.
Huduma ya baada ya utoaji wa mimba Kufuatilia katika kliniki wakati mwingine kunapendekezwa kudhibitisha MA iliyofanikiwa.
Wanawake wanapaswa kuwasiliana na kliniki yao ikiwa wanapata: kutokwa na damu nyingi, homa, maumivu makali, dalili za kuambukizwa au kuendelea kwa ujauzito.
Matokeo ya upimaji wa mimba kwa mkojo yatakuwa hasi wiki nne hadi wiki sita-6 baada ya mafanikio ya MA.
Kwa ujumla, wanawake wanaweza kurudi kwenye shughuli zao za kawaida kama inavyostahimiliwa baada ya MA.
Unaweza kupata maelezo zaidi juu huduma ya baada ya utoaji wa mimba hapa.
Utunzaji wa uzazi Njia nyingi za upangaji uzazi zinaweza kuanza mara moja baada ya utoaji wa mimba wa kimatibabu, isipokuwa machache ya kuwa pete ya uke na IUD.
Kupata njia sahihi za upangaji uzazi kwa changuo lako, tembelea www.findmymethod.org

Kutoa mimba kwa upasuaji au kwa njia ya kunyonya au kufyonza (MVA)
Ubaya na uzuri wa utoaji mimba kwa njia ya kunyonya au kufyoza (MVA au kutoa mimba kwa upasuaji) [3], [4]
UfanisiAsilimia 99 yenye ufanisi
UsalamaSalama sana
Kupima ujauzitoJaribio la mawimbi sauti inahitajika ili kujua tarehe ya ujauzito
Kikomo cha umri wa mimbaInaweza kutumika hadi ujauzito wa wiki kumi hadi kumi na nne ( Kikomo cha umri wa ujauzito kwa MVA mara nyingi hutegemea kliniki, na vile vile mhuduma wa afya anayefanya utaratibu)
Ili kujua juu ya umri wako wa mimba yako, tembelea ukurasa wetu ambao una Uthibitisho wa Mimba na kikokotoo.
MahaliInafanyika katika kliniki au hospitali.
mtekelezajiInahitaji daktari aliyefundishwa kutekeleza utaratibu.
MudaWakati wa kukamilisha MVA ni madakika.
MadharaKawaida ina muda mfupi wa kutokwa na damu kuliko MA kwani huchukua mda wa wiki moja hadi mbili.
Kawaida ina muda mfupi wa kukandamiza kuliko MA, lakini inaweza kuja na kupotea kwa mda wa wiki moja hadi mbili.
Shida na hatariUwezekano wa hatari ni pamoja na: kutokwa na damu nyingi, maambukizi, kujeruhiwa kwa mfuko wa uzazi na miundo iliyo karibu, utoaji mimba usio kamilika, kuendelea kwa ujauzito, na kifo.
GharamaKawaida, MVA itakuwa ghali zaidi kuliko MA kwa sababu MVA inahitaji upimaji fulani (yaani Jaribio la mawimbi sauti) na mtaalamu mwenye ujuzi wa kufanya utaratibu. Gharama halisi ya MVA itatofautiana sana kulingana na eneo la jiografia na sheria husika zinazohusiana na utoaji mimba.
Huduma ya baada ya utoaji wa mimba Kufuatilia katika kliniki wakati mwingine hutolewa baada ya utoaji mimba wa upasuaji, lakini hauhitajiki.
Wanawake wanapaswa kuwasiliana na kliniki yao ikiwa wanapata: kutokwa na damu nyingi, homa, maumivu makali, dalili za kuambukizwa au kuendelea kwa ujauzito.
Matokeo ya upimaji wa mimba kwa mkojo yatakuwa hasi baada ya wiki mbili au tatu baada ya utaratibu.
Kwa ujumla, wanawake wanaweza kurudi kwenye shughuli zao za kawaida kama inavyostahimiliwa baada ya utoaji mimba kwa upasuaji.
Unaweza kupata maelezo zaidi juu ya huduma ya baada ya utoaji wa mimba baada ya njia ya kunyonya au kufyonza hapa.
Utunzaji wa uzazi Njia zote za upangaji uzazi zinaweza kuanza mara baada ya utaratibu wa MVA.
Kupata njia sahihi za upangaji uzazi kwa changuo lako, tembelea www.findmymethod.org

Waandishi:

timu ya safe2choose na wataalam wanaounga mkono carafem, kwa kuzingatia mapendekezo ya 2020 na shirika la Kitaifa aa Utoaji wa Mimba (NAF), mapendekezo ya mwaka wa 2019 na Ipas, na mapendekezo ya mwaka wa 2012 yaliyotolewa na shirika la Afya Ulimwenguni.

Shirikisho la Kuavya mimba ni chama cha wataalamu wa wahudumu wa afya Amerika Kaskazini.

carafem hutoa huduma bora na ya kitaalam ya utoaji wa mimba na upangaji wa uzazi ili watu waweze kudhibiti idadi na nafasi za watoto wao.

Ipas ndio shirika la pekee la kimataifa ambalo limedhamiria tu katika kupanua ufikiaji wa kutoa mimba kwa njia salama na utunzaji wa uzazi.

Shirika la Afya Ulimwengini ni chombo maalum cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na afya ya umma ya kimataifa.


Vyanzo

[1] National Abortion Federation (NAF). Clinical Policy Guidelines for Abortion Care. 2020. Retrieved from: https://5aa1b2xfmfh2e2mk03kk8rsx-wpengine.netdna-ssl.com/wp-content/uploads/2020_cpgs_final.pdf

[2] Gynuity. Providing medical abortion in low-resource settings An Introductory Guidebook. Second Edition. 2009. Retrieved from: https://gynuity.org/assets/resources/clinguide_maguide2nd_edition_en.pdf

[3] World Health Organization (WHO). Safe abortion: technical and policy guidance for health systems, second edition. 2012. Retrieved from: https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/70914/9789241548434_eng.pdf;jsessionid=F77B761669FC579124C1E9CA2CC3CFDB?sequence=1

[4] Ipas. Clinical Updates in Reproductive Health. 2019. Retrieved from: https://ipas.azureedge.net/files/CURHE19-april-ClinicalUpdatesInReproductiveHealth.pdf

ilisasishwa mwisho 05/08/2020

Tuko hapa kukuunga mkono Kwa chaguo lako la kuavya mimba wakati wa COVID-19

Tunafuatilia Kwa makini ueneaji wa virusi vya Corona kimataifa na tutaendelea kusasisha habari na huduma zetu.

Tunawashauri wasomaji wetu:

  1. Kusoma chapisho letu la hivi karibuni la blogi juu ya uavyaji wa mimba na COVID-19
  2. Kufuata miongozo ya usalama wa Shirika la Afya Duniani kuhusu COVID-19
  3. Kuwasiliana na washauri wetu