Sisi ni nani na kwa nini tunatetea kutoa mimba kwa usalama?

safe2choose ni biashara ya kijamii ambayo ni sehemu ya watetezi wa kimataifa wa haki ya uzazi na ufikiaji wa utoaji mimba ulio salama. Kazi yetu ni kusaidia wanawake kote ulimwenguni kufikia taarifa sahihi na vidonge bora na nafuu vya kutoa mimba ili waweze kutoa mimba kwa usalama pahali, wakati na wakiwa na watu wawatakao bila wasiwasi.

Timu yetu inajumuisha washauri wanaozungumza lugha nyingi, madaktari na wataalamu katika ulingo wa afya ya umma na maendeleo ya kimataifa wanaofanya kazi pamoja kukupa taarifa sahihi kuhusu kutoa mimba kwa usalama. Tunawasaidia na kuwapa wanawake uhuru wa kufanya maamuzi yao wenyewe kuhusu miili yao na afya yao ya uzazi.

Je, mbona vidonge vya kutoa mimba?

safe2choose inaamini kwamba wanawake wenye mimba isiyotarajiwa wana haki ya kufanya maamuzi kuhusu miili yao na siku zao za usoni chini ya hali salama. Tunaelewa kwamba katika nchi ambazo kutoa mimba hakuruhusiwi wanawake wengi hulazimika kutoa mimba kwa njia hatari na kuhatarisha maisha yao. Vidonge vya kutoa mimba ni chaguo salama kwa wanawake kote ulimwenguni na pia ni sehemu muhimu katika kupigania haki za uzazi.

Je, ulijua kwamba:

Takriban milioni 85 (41%) ya mimba zinazopatikana kila mwaka ni zisizokusudiwa (Taasisi ya Guttmacher).

Kila mwaka wanawake milioni 6 ulimwenguni hutoa mimba kwa njia hatari.

Milioni 18.5 za mimba zilizotolewa kwa njia hatari hutendeka katika nchi zinazoendelea.

Takriban wanawake 47.000 hufa kila mwaka kwa sababu ya matatizo yatokanayo na utoaji mimba hatari (WHO).

Kazi yetu:

Ni kukuza kutoa mimba kwa usalama kwa kuwezesha ufikiaji wa vidonge vya kutoa mimba.

Wajibu wetu

safe2choose:

  • -Huwa inatoa taarifa kwa kuzingatia ushahidi wa kisayansi uliosasishwa kabisa kuhusu kutoa mimba.
  • -Huwa inatoa huduma za kutoa mimba zilizo salama, siri, fanisi na nafuu bila hukumu na unyanyapaa.
  • -Huwezesha ufikiaji wa vidonge bora vya kutoa mimba vilivyopitishwa kimataifa kwa bei nafuu zaidi iwezekanayo na agizo la kimatibabu.
  • -Inafikika kwa urahisi, ina uhusiano mzuri na watu na husaidia sana.
  • -Huwa inaheshimu haki yako ya kufanya maamuzi yako mwenyewe.