Je! ni nini Tofauti kati ya utoaji mimba kwa njia ya kufyonza na upanuaji na Kuondoa D&E?

Kuna aina chache za utoaji mimba ambazo hufanywa katika kliniki au hospitali; njia ya kunyonya au kufyonza inaweza kufanywa hadi ujauzito wa wiki 15 (kulingana na upendeleo wa mhuduma wa afya) na Njia ya upanuaji na ukwanguaji (D&E) unaweza kufanywa zaidi ya ujauzito wa wiki 15.

Aina ya utoaji mimba ambayo unaweza kuwa nayo inategemea karibu kabisa juu ya umbali wako katika ujauzito wako. Ikiwa uko katika trimester yako ya kwanza, labda utatumia njia ya kunyonya au kufyonza. Ikiwa uko katika trimester yako ya pili (ikimaanisha kuwa imekuwa zaidi ya wiki 14 tangu kipindi chako cha mwisho cha hedhi), labda utatumia njia ya D&E. Ikiwa uko mbali zaidi katika ujauzito, unaweza kuhitaji utoaji mimba.

Aina zote mbili za utoaji mimba ya upasuaji zinahitaji matumizi ya dawa kuandaa uterasi na kizazi; vyombo tofauti pia hutumiwa kuondoa ujauzito kutoka kwa uterasi [1].


Vyanzo

[1] “Utoaji mimba kwa njia salama: mwongozo wa kiufundi na sera kwa mifumo ya afya.” Shirika la Afya Ulimwenguni, toleo la pili, 2012, www.who.int/reproductivehealth/publications/unsafe_abortion/9789241548434/en/. Ilifikia Novemba 2020.

*Hakuna kinachotolewa hapa kinapaswa kudhaniwa kuwa ushauri wa kitaalam na hakuna dawa / tembe zinazopaswa kutumiwa bila agizo kutoka kwa mtaalamu aliye na leseni / aliye sajiliwa anayestahili kuagiza dawa hiyo katika mamlaka yako ya karibu.