Nastahili kungoja kipindi kipi ili kujamiiana baada ya kutumia tembe za kutoa mimba?

Hakuna ushahidi kuwa unastahili kungoja kwa kipindi fulani kabla ya kujamiiana baada ya kutumia tembe za kuto mimba. Hata hivyo, ni muhimu kwako kusikiza mwili wako na ari yako. Ikiwa unahisi tayari kurudi kujamiiana unaweza kufanya hivyo.

Ni muhimu pia kujua unaweza kuwa na uja uzito tena mapema hata kwa siku 8 baada ya kutumia tembe za kutoa mimba. Kwa sababu hii, inapendekezwa kutumia kondomu au mbinu yoyote ya kuzuia mimba za usoni zisizohitajika. Tena kumbuka, kondomu ndio njia pekee inayoweza kuzuia dhidi ya maambukizi ya zinaa. [1]

Kujua zaidi kuhusu njia zako za kupanga uzazi tembelea, www.findmymethod.org

[1] Ipas. (2019). Clinical Updates in Reproductive Health. L. Castleman & N. Kapp (Eds.). Chapel Hill, NC: Ipas. Retrieved from: https://ipas.azureedge.net/files/CURHE19-april-ClinicalUpdatesInReproductiveHealth.pdf

TAZAMA MASWALI ZAIDI

*Hakuna kinachotolewa hapa kinapaswa kudhaniwa kuwa ushauri wa kitaalam na hakuna dawa / tembe zinazopaswa kutumiwa bila agizo kutoka kwa mtaalamu aliye na leseni / aliye sajiliwa anayestahili kuagiza dawa hiyo katika mamlaka yako ya karibu.