Nunua tembe za kuavya mimba

Jinsi ya kununua tembe za kuavya mimba katika eneo lako

Kunaweza kua na njia kadhaa za kupata tembe za kuavya mimba kutegemea na nchi unayoishi. Ukituambia nchi unayoishi, tutakufahamisha njia ulizo nazo za kupata tembe za kuavya mimba na jinsi ya kuavya mimba salama. Wasiliana nasi ili tukueleze jinsi ya kupata uaviaji mimba kwa njia salama.

Iwapo unapanga kununua tembe za kuavya mimba katika eneo lako, kuna mambo machache muhimu ambayo tungependa kushiriki nawe.

Wakati mwingine kununua tembe katika eneo lako kunaweza kuwa vigumu kwani huwezi kuwa na hakika ya ubora wake au kama ni halisi au la. Pia, huwa ghali sana. Hapo chini kuna vigezo fulani unavyostahili kufikiri unaponunua tembe za kuavya mimba.

Kununua Mifepristone eneo lako

Iwapo unajaribu kununua Mifepristone katika eneo lako, unaweza kuwa na ugumu kuipata.Kimsingi Mifepristone hutumika kwa uaviaji mimba au kupoteza mimba na haijasajiliwa katika nchi nyingi, hasa ambapo uaviaji mimba salama umebanwa kisheria. Hivyo inaweza kuwa vigumu kuipata, hata katika duka za dawa. [1]

Hii inamaanisha kuwa wakati mwingi unapopata Mifepristone katika soko isiyo rasmi, inaweza kuwa si halisi.

Hakuna njia yetu sisi wala yako ya kutambua kama tembe ni halisi kwa kuitazama tu. Hii ni kwa sababu kuna aina tofauti na hivyo maumbo tofauti, ukubwa na rangi. Njia pekee ya kujua kwa hakika ni kama Mifepristone bado iko katika mfuko wake halisi. Iwapo ni hivyo, angalia siku ya kuharibika. [2]

Iwapo utapata Mifepristone, kumbuka ya kwamba kwa ujumla imeamriwa na mtaalamu wa matibabu na kwamba utahitaji tembe moja tu ya 200mg ili kukamilisha uavyaji mimba kwa ufanisi. [3]

Wakati mwingine kipimo (mg) cha tembe utapata ni tofauti, hivyo utahitaji kufanya hesabu tena ya idadi ya tembe. Kwa mfano, kama utaweza kupata tembe za kipimo hiki:

– 10mg, utahitaji tembe 20 ili kufika kipimo sahihi cha 200mg.

– 50mg, utahitaji tembe 4 ili kufika kipimo sahihi cha 200mg.

– 100mg, utahitaji tembe 2 ili kufika kipimo sahihi cha 200mg na kadhalika.

Kunua Misoprostol eneo lako

Ni rahisi kupata Misoprostol katika eneo lako kwa sababu imesajiliwa katika nchi nyingi kutumika kwa vidonda vya tumbo, kuchochea uchungu wa uzazi, au kutibu tatizo la uvujaji damu baada ya kujifungua. Katika baadhi ya nchi unaweza kuipata katika duka za dawa bila maelekezo ya jinsi ya kuitumia. [4]

Misoprostol ina majina tofauti. Wakati mwingine utapata dawa hii chini ya majina yafuatayo. Cytotec, Cyprostol, Misotrol, Prostokos, Vagiprost, Misotac, Mizoprotol, Misofar, Isovent, Kontrac, Cytopan, Noprostol, Gastrul, Chromalux, Asotec, Cyrux, Cytil, Misoprolen, Mibetec, Cytomis, Miclofenac, Misoclo, Misofen, Misogon, Alsoben, Misel, Sintec, Gastrotec, Cystol, Gastec, Cirotec, Gistol, Misoplus, Zitotec, Prestakind, Misoprost, Cytolog, GMisoprostol, Mirolut, Gymiso

Pia unaweza kuamrishwa kutumia tembe inayounganisha Misoprostol na Diclofenac, muradi kipimo cha Misoprostol ni 200mcg. Dawa hii huja kwa majina kama Oxaprost, Oxaprost 75 na Arthrotec. Kwa maelezo zaidi jinsi ya kutumia tembe hii, angalia kitengo cha FAQs, na wasiliana nasi unapohitaji.

Ikiwa utaenda kutumia Misoprostol tu ili kuchochea uavyaji mimba, utaamrishwa tembe nane hadi kumi na mbili kwa jumla, kutegemea na umri uliokadiriwa wa uja uzito wako. Inapowezekana, inapendelewa uwe na tembe kumi na mbili.

Ni vyema zaidi kununua tembe katika mifuko yake halisi, lakini iwapo hili haliwezekani, hakikisha unakagua tembe. Ziguse kuhakikisha haziyeyuki na kuwa zote zinafanana. Hakikisha umethibitisha tarehe ya kuharibika kama zipo katika mfuko halisi.

Maelekezo jinsi ya kutumia tembe

Unaponunua tembe kutoka maeneo tofauti, aidha soko isiyo rasmi, kutoka kwa duka la dawa au kwa daktari kwa mfano, utakuwa unapata maelekezo yanayokinzana kuhusu jinsi ya kutumia tembe.

Wauzaji wengi hawajapata mafunzo ya kutosha na hawana taarifa sahihi kuhusu jinsi ya kutumia tembe za kuavya mimba. Wengine wao wanauza tu tembe za kuavya mimba ili kutengeneza pesa, na si kusaidia wanawake. Kabla ya kutumia tembe za kuavya mimba,thibitisha kuwa unafuata maelekezo yanayofaa kwa kuangalia taratibu zetu mtandaoni kuhusu kuavya mimba kwa Mifepristone na Misoprostol au kwa Misoprostol tu au kwa kuwaandikia washauri wetu katika wasiliana nasi.

Duka za dawa na madaktari pia wanaweza kutoa taarifa zisizo za kweli kuhusu namna ya kutumia tembe. Vizuizi vya kuavya mimba na ukweli kwamba kuavya mimba hakujakubalika kijamii katika sehemu nyingi huunda mazingara ya hadithi na habari zisizo za kweli, hata miongoni mwa wahudumu wa afya.

Ni muhimu kufuata maelekezo yanayoaminika na yanayojikita katika tafiti za kisayansi na yaliyokubaliwa na mashirika ya kiafya ya kimataifa. Ikiwa umesoma taarifa nyingi tofauti, wasiliana nasi ili tuondoe shaka zako na kukupa taarifa za kuaminika. [5]

Kumbuka safe2choose iko hapa kukusaidia

Washauri wetu wamefunzwa kitaalamu kwa mtazamo unaozingatia haki za wanawake kukuelekeza na kukuharifu kwa matumizi ya tembe za kuavya mimba pamoja na maelekezo sahihi jinsi ya kuzitumia. Huwa tunafuata maelekezo ya Shirika la Afya Duniani (WHO). Ikiwa ni lazima, pia sisi hufanya kila tuwezalo kukuelekeza kwa mashirika ya kutegemewa ambayo yanaweza kukusaidia kupata tembe za kuavya mimba au kupata habari katika eneo lako kuzihusu. [3]


Sources

[1] Gynuity. Mifepristone approvals. Retrieved from: https://gynuity.org/assets/resources/biblio_ref_lst_mife_en.pdf.

[2] IPPF. Registered Mifepristone brands. Retrieved from: https://www.medab.org/advanced-search-multiple-results?country=all&commodity=100&brand=all#multiple-search-result

[3] World Health Organization. Safe abortion: technical and policy guidance for health systems. Retrieved from: https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/70914/;jsessionid=B7AEEBE4F34809D869F73B1ABA7F6221?sequence=1

[4] WHO. Essential Medicines List Application Mifepristone–Misoprostol for Medical Abortion. Retrieved from: https://www.who.int/selection_medicines/committees/expert/22/applications/s22.1_mifepristone-misoprostol.pdf?ua=1

[5] Ipas. (2019). Clinical Updates in Reproductive Health. L. Castleman & N. Kapp (Eds.). Chapel Hill, NC: Ipas. Retrieved from:https://ipas.azureedge.net/files/CURHE19-april-ClinicalUpdatesInReproductiveHealth.pdf

Tuko hapa kukuunga mkono Kwa chaguo lako la kuavya mimba wakati wa COVID-19

Tunafuatilia Kwa makini ueneaji wa virusi vya Corona kimataifa na tutaendelea kusasisha habari na huduma zetu.

Tunawashauri wasomaji wetu:

  1. Kusoma chapisho letu la hivi karibuni la blogi juu ya uavyaji wa mimba na COVID-19
  2. Kufuata miongozo ya usalama wa Shirika la Afya Duniani kuhusu COVID-19
  3. Kuwasiliana na washauri wetu