Uthibitishaji wa Uja Uzito na Kikokotoo

Kufanya hesabu ya muda wako wa uja uzito ni muhimu hata kama utaamua kutamatisha au kuendelea na uja uzito.

Ikiwa utaamua kutamatisha uja uzito, wiki za kuwa mja mzito zitakusaidia kubaini ni njia zipi za kuavya mimba ulizo nazo.

Ikiwa utaamua kuendelea na uja uzito, hii itasaidia mkunga wako au daktari kujua kama mimba inakua kawaida. Kumbuka kuwa uja uzito hudumu kati ya wiki thelathini na nane na arubaini na mbili kutoka siku ya mwisho ya hedhi yako. [1]

Njia rahisi ya kufanya hesabu wiki za uja uzito wako ni kwa kuhesabu idadi ya wiki na siku kutoka siku ya kwanza ya kipindi cha hedhi yako ya mwisho.

Ni muhimu kuhesabu kutoka siku yako ya kwanza ya kipindi cha hedhi yako ya hivi punde , hii ni kwa sababu kutoka kwa hii tunaweza kukadiria yai lilipoachiliwa na kupatana na mbegu za kiume. [2]

Kuwa mwangalifu na makosakadhaa ya kawaida ambayo wanawake hufanya. Unapohesabu, usihesabu kwa:

- Kutoka wakati ulipokosa hedhi yako,

- Kutoka siku ya kujamiiana,

- Kutoka siku unayofikiri ulipata mimba.

Iwapo unahitaji msaada wa kuhesabu wiki za uja uzito wako, chagua siku ya kwanza ya hedhi yako ya mwisho hapa.

Iwapo haufuatilii hedhi yako au huwezi kumbuka mara ya mwisho ulipokuwa nayo, kumbuka hapo nyuma ulichokuwa ukifanya ulipokuwa nayo. Ulikuwa wapi? Ulikuwa an nani? Wakati mwingine hili hukufanya ukumbuke siku yako ya mwisho ya hedhi. [3]

Njia zingine za kuthibitisha uja uzito wako ni pamoja na:

1) Jaribio la mkojo: Hili jaribio ni la kawaida, na hugundua uwepo wa homoni ya uja uzito katika mkojo. Ili kujiepusha na "uongo hasi" jaribio hili linastahili kufanywa wiki 2 au zaidi baada ya kujamiiana bila kinga.

- Manufaa: si ghali na inaweza kufanywa faraghani nyumbani.

- Upungufu: Haisaidii kuhesabu umri wa uja uzito.

2) Jaribio la damu: Aina mbili za jaribio hili zipo: kiubora (hugundua homoni ya uja uzito hCG katika damu) na kijumla (hupima kiasi cha homoni).

- Manufaa: Inaweza kubaini uja uzito wa mapema kuliko jaribio la mkojo, na wakati mwingine inasaidia kukadiria umri wa uja uzito (kama ni kiubora)

- Upungufu: Ni ghali zaidi na lazima iamrishwe na mhudumu wa afya.

3) Jaribio la mawimbi sauti: Jaribio hili linaweza kuwa muhimu takriban wiki 4 za uja uzito au zaidi, la sivyo hakuna kitu kitaonekana. Inaweza kuwa muhimu hasa ikiwa haujui kipindi chako cha mwisho cha hedhi.

- Manufaa: Ni ya kweli katika kukadiria umri wa uja uzito, na inaweza kutumika kugundua uja uzito nje ya tumbo la uzazi au mimba zingine zisizodumu.

- Upungufu: Inaweza kuwa ghali zaidi na lazima itekelezwa na mhudumu wa afya. [4]


Sources

[1] World Health Organization. Safe abortion: technical and policy guidance for health systems. Retrieved from: https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/70914/;jsessionid=B7AEEBE4F34809D869F73B1ABA7F6221?sequence=1

[2] Megan Wainwright, Christopher J Colvin, Alison Swartz & Natalie Leon. Self-management of medical abortion: a qualitative evidence synthesis. Retrieved from: https://www.tandfonline.com/doi/pdf/10.1016/j.rhm.2016.06.008?needAccess=true

[3] Healthline. Tests Used to Confirm Pregnancy. Retrieved from: https://www.healthline.com/health/pregnancy/tests

[4] WebMd. Pregnancy Tests. Retrieved from: https://www.webmd.com/baby/guide/pregnancy-tests#1