Kuavyamimba kwa tembe

Uaviaji mimba kwa njia ya matibabu [1] kwa kawaida hujulikana kama kuavya mimba kwa tembe. Watu wengine pia huita njia hii kama uaviaji mimba wa kujisababishia, uavyaji mimbautekelezwao-kibinafsi [2] au kuavyamimba kwa kufanya-mwenyewe.

Ikiwa utatumia tembe za kuavya mimba utashuhudia uvujaji damu na msokoto. Dalili ni sawa na kipindi chako cha hedhi au kama unapopoteza mimba. (uaviaji mimba kwa njia ya asili).

Kuna njia mbili za kuwa na uaviaji mimba kwa tembe: kutumiaMifepristone na Misoprostolau kutumiaMisoprostol tu.

Mifepristone

– Mifepristone ni dawa inayozuia mtiririko wa progesterone, ambayo ni homoni inayosaidia uja uzito. Bila progesterone uja uzito hauwezi kua. [3]

– Mifepristone pia hulegeza mlango wa tumbo la uzazi (sehemu ya chini ya tumbo la uzazi) ambayo huzidisha athari ya Misoprostol. [4]

– Mifespristone tu haitoshi kusababisha uaviaji mimba, Misoprostol pia inahitajika. [5]

– Kimsingi Mifepristone hutumika kuavya mimba au kupoteza mimba, hivyo kutegemea na sheria and vikwazo, wakati mwingine inaweza kuwa vigumu kuipata. [6]

Misoprostol

– Misoprostol ni dawa ambayo husababisha tumbo la uzazi kusonga (au kujikunja), na hii inasaidia katika kuondoa mimba pamoja na uvujaji wa damu na msokoto.

– Unaweza kutumia Misoprostol bila Mifepristone, lakini ni bora zaidi kutumia dawa zote pamoja.

– Misoprostol ina matumizi mengine ya kiafya mbali na kuavya mimba, hivyo kwa kawaida inapatikana sana. [7]

Mifepristone na Misoprostol zimeorodheshwa kama dawa muhimu kulingana na Shirika la Afya Duniani na zina kusudiwa kutumiwa kwa uaviaji mimba salama. [8]

Ili kujua jinsi ya kuavya mimba kwa njia salama na yenye ufanisi kwa kutumia Misoprostol na Mifepristone bonyeza hapa. Ikiwa unatumia Misoprostol tu bonyeza hapa.

Usalama wa tembe za uaviaji mimba na dalili kinzani

Kuavya mimba kwa njia ya matibabu ni salama kwa wanawake wengi. Kunatuhali chache za kiafya zenye dalili kinzani kwa kutumia tembe za kuavya mimba. [9]

Mifepristone haipendekezwi ikiwa :

– Umekuwa ukitumia steroidi ya muda mrefu (kama vile Prednisone au Dexamethasone) Lakini unaweza kuavya mimba kwa Misoprostol tu.

Uaviaji mimba kwa kutumia tembe za Mifepristone na Misoprostol haupendekezwi [10]:

– Ukitumia tembe za kuzuia kushikana kwa damu (viyeyusha damu) kama vile Heparin na Warfarin,

– Ikiwa una kasoro ya kuvuja damu kama vile Porphyria,

– Ikiwa unaathiriwa na Mifepristone, Misoprostol au prostaglandini, uaviaji mimba kwa tembe haukupendekezwi kwako. Njia pekee ya kujua kama una unaathiriwa ni ikiwa umetumia tembe hizi awali na ukaathirika. Haiwezekani kujua kama utaathirika au hautaathirika kabla ya kutumia tembe hizi.

– Ikiwa una uja uzito nje ya tumbo la uzazi (nje ya tumbo la uzazi) tembe za kuavya mimba haziwezi kukudhuru, lakini hazitatamatisha uja uzito. Ikiwa unajua una uja uzito nje ya tumbo la uzazi, unahitaji kutafuta msaada wa kiafya mara moja ili kukabili uja uzito nje ya tumbo la uzazi kwa njia salama.

Ikiwa una IUD (kifaa kati-uterasi) si dalili kinzani kwa kutumia tembe za kuavya mimba, lakini inahitaji umakinifu. Hatari ya kuwa na uja uzito nje ya tumbo la uzazi (uja uzito usio ndani ya uterasi) unaongezeka unapokuwa na IUD. Kila mara inapowezekana, pendekezo salama ni kutolewa IUD kabla ya kutumia tembe za kuavya mimba. [11]

Ikiwa huna hakika kama tembe za kuavya mimba ni salama kwako, wasiliana nasi! Tunaweza kukusaidia kujua kama njia hii inakufaa.

Kumbuka safe2choose ina mafunzo tu kusaidia wanawake ambao watatumia tembe za kuavya mimba katika wiki kumi na moja za kwanza za uja uzito. Ikiwa mimba yako imekua zaidi, tutafanya kila tuwezalo kukuelekeza kwa shirika lililojiandaa zaidi kukusaidia. [12]

Cha kutarajia unapoavya mimba kwa tembe

Baada ya kutumia tembe za kuavya mimba utakuwa na dalili zinazofanana na za hedhi au kupoteza mimba. Ikiwa unatumia Mifepristone, hii dawa kwa kawaida haisababishi dalili zozote. Dalili nyingi zitatokea tu baada ya kutumia Misoprostol.

Dalili zinazotarajiwa kutokea zinajumuisha: msokoto, kuvuja damu na pengine kupitisha damu iliyokolea. Kwa kawaida uvujaji damu zaidi na msokoto utatokea katika saa arubaini na nane za kwanza baada ya kutumia Misoprostol, lakini unaweza kushuhudia kuvuja au kutovuja damu kwa siku kadhaa au majuma. [13]

Misoprostol inaweza sababisha madhara ya muda kama vile joto, kibaridi, kuhara, kichefuchefu, kutapika, na kuumwa kichwa. Iwapo hautashuhudia ni kawaida kabisa. Iwapo utashuhudia, zitatoweka baada ya saa arubaini na nane zijazo au chini. [13]

Wasiliana nasi ili kujua namna ya kukabiliana na madhara.

Namna ya kujua ikiwa tembe zilifanya kazi

Ikiwa ulitumia dawa kulingana na maelekezo yaliyopendekezwa, na una uvuja damu nyingi kama unapokuwa na hedhi (au zaidi) kwa saa kadhaa, kuna uwezekano kuwa uaviaji mimba ulifanikiwa. Dalili zako za uja uzito (matiti nyororo, kichefuchefu, uchovu), polepole zinastahili kuimarika na baadaye kutoweka takriban siku tano baada ya kutumia tembe za kuavya mimba. Hii ni dalili nyingine nzuri kuwa tembe zilifanikiwa. [11]

Ingawa si lazima, ikiwa unapendelea kuthibitisha zaidi unaweza kufanya mojawapo ya majaribio haya:

– Jaribio la mkojo (mkojo hcg): Hili ni jaribio rahisi linaloweza kufanywa kwa kuthibitisha, pia linaweza kufanywa faraghani katika nyumba yako. Inapendekezwa kusubiri takriban wiki nne baada ya kutumia tembe za kuavya mimba. Ikiwa mchakato ulifanikiwa, jaribio linastahili kuwa hasi baada ya wiki nne.

– Jaribio la damu (Ujumuishaji hcg): Jaribio hili linahitaji safari ya kimatibabu, na ni bora zaidi ikiwa jaribio la damu hii lilifanywa kabla ya kutumia tembe za kuavya mimba kwa ajili ya kulinganisha viwango vya homoni. Jaribio hili halifanywi kila mara, na hivyobasi kama utapendelea kuthibitisha jaribio la mkojo kama lilivyoelezwa hapo juu hupendekezwa zaidi.

Jaribio la mawimbi sauti: Hii inahitaji safari ya kimatibabu, na inaweza kutumika kubaini mimba inayokua. Kumbuka kuwa kama tembe za kuavya mimba zilifanya kazi, kunaweza kukawa na damu bado na vijinyama vinavyoonekana katika jaribio la mawimbi sauti kwatakriban wiki mbili. Hata kama mimba imetoka, wakati mwingine jaribio la mawimbi sauti hufanywa.

Iwapo saa arubaini na nane zimepita baada ya kutumia kipimo cha mwisho cha Misoprostol na hujavuja damu au kiwango cha uvujaji wako ni chini ya hedhi yako, kuna uwezekano kwamba uaviaji mimba haukufanikiwa. [14]

Katika hali nyingi, inawezekana kujaribu tena kwa tembe za kuavya mimba. Wasiliana nasi iwapo hii ni hali yako ili tukupe msaada.

Utunzaji wa kiafya baada ya tembe za kuavya mimba

Iwapo dalili zako ziko zilivyotarajiwa na hauna dalili zozote za kutahadharisha, hauhitaji utunzaji wa kiafya. Si lazima kufanya jaribio la uja uzito au jaribio la mawimbi sauti baadaye, ama kuwa na upasuaji kama vile D&C

Uwezo wa kupata uja uzito na hedhi baada ya kuavya mimba

Baada ya kuavya mimba (kwa upasuaji au matibabu), kipindi cha hedhi yako kitaanza tena, kama kwamba ulikuwa na muda wako wa hedhi. Bado mayai ya kike yataachiliwa tena takriban siku kumi baadaye. Hii inamaanisha kuwa unaweza kuwa na uja uzito tena ikiwa utajamiiana bila kinga. [11] Ikiwa hauko tayari kuwa mjamzito tena, unapaswa kuzingatia njia za kuzuia mimba. Unaweza kupata habari zaidi kwa FindMyMethod.org

Hedhi yako itakayofuata inaweza kurejea baada ya wiki nne au sita baada ya kutumia tembe za kuavya mimba. [15]


Sources

[1] World Health Organization. Safe abortion: technical and policy guidance for health systems. Retrieved from: https://apps.who.int/iris/bitstream/handle/10665/70914/;jsessionid=B7AEEBE4F34809D869F73B1ABA7F6221?sequence=1

[2] Reproductive Health Matters. Self-management of medical abortion: a qualitative evidence synthesis. Retrieved from: https://www.tandfonline.com/doi/pdf/10.1016/j.rhm.2016.06.008?needAccess=true

[3] Children by Choice. Medication abortion. Retrieved from:https://www.childrenbychoice.org.au/foryou/abortion/medicationabortion

[4] S. Hopkins MD, M. Fleseriu MD. Chapter 7 – Medical Treatment of Cushing’s Disease. Retrieved from:https://www.sciencedirect.com/science/article/pii/B9780128043400000073

[5] Thoai D Ngo, Min Hae Park, Haleema Shakur & Caroline Free. Comparative effectiveness, safety and acceptability of medical abortion at home and in a clinic: a systematic review. Retrieved from: https://www.who.int/bulletin/volumes/89/5/10-084046/en/

[6] Brooke Ronald Johnson, Vinod Mishra, Antonella Francheska Lavelanet, Rajat Khosla & Bela Ganatra. A global database of abortion laws, policies, health standards and guidelinesArticle has an altmetric score of 221. Retrieved from: https://www.who.int/bulletin/volumes/95/7/17-197442/en/

[7] Webmd. Misoprostol. Retrieved from: https://www.webmd.com/drugs/2/drug-6111/misoprostol-oral/details

[8] WHO. Access to essential medicines as part of the right to health. Retrieved from: https://www.who.int/medicines/areas/human_rights/en/

[9] Ipas. Medical abortion contraindications and precautions. Retrieved from:https://www.ipas.org/clinical-updates/general/ma-precautions

[10] WHO. Essential Medicines List Application Mifepristone–Misoprostol for Medical Abortion. Retrieved from:https://www.who.int/selection_medicines/committees/expert/22/applications/s22.1_mifepristone-misoprostol.pdf?ua=1

[11] Ipas. (2019). Clinical Updates in Reproductive Health. L. Castleman & N. Kapp (Eds.). Chapel Hill, NC: Ipas. Retrieved from:https://ipas.azureedge.net/files/CURHE19-april-ClinicalUpdatesInReproductiveHealth.pdf

[12] National Abortion Federation. 2020 Clinical Policy Guidelines for Abortion Care. Retrieved from:https://5aa1b2xfmfh2e2mk03kk8rsx-wpengine.netdna-ssl.com/wp-content/uploads/2020_cpgs_final.pdf

[13] Planned Parenthood. How does the abortion pill work? Retrieved from: https://www.plannedparenthood.org/learn/abortion/the-abortion-pill/how-does-the-abortion-pill-work

[14] Gynuity. Abortion with self-administered misoprostol. Retrieved from: https://gynuity.org/assets/resources/polbrf_misoprostol_selfguide_en.pdf

[15] BPAS. Caring for yourself after your abortion. Retrieved from: https://www.bpas.org/abortion-care/abortion-aftercare