Nahitaji jaribio la mawimbi sauti ili kuthibitisha ikiwa tembe za kutoa mimba zilifanikiwa?

Jaribio la mawimbi sauti si lazima baada ya tembe ya kutoa mimba. Ingawa wakati mwingine itasaidia kuthibitisha kama utaratibu ulifanikiwa, inaweza pia wakati mwingine kutumika kubaini mwanamke aliye na ” utoaji mimba usio kamili” ikiwa damu na damu iliyokolea bado inaonekana ndani ya tumbo la uzazi Hii ni kawaida kupatikana kwa jaribio la mawimbi sauti…

Utenda kazi wa tembe za kutoa mimba hupungua zinapotumika mara kwa mara?

Utenda kazi wa tembe ya kutoa mimba haupungui ikiwa ulizitumia [1] katika uja uzito uliopita na una ari ya kufanya hivyo tena katika mimba ya sasa. Kuna uwezekano unaofanana kuwa zitafanya kazi vyema kama zilivyofanya katika matumizi yaliyopita. Sources [1] Women on Web. Is it safe to have an abortion with pills if you’ve already…

Nastahili kungoja kipindi kipi ili kujamiiana baada ya kutumia tembe za kutoa mimba?

Hakuna ushahidi kuwa unastahili kungoja kwa kipindi fulani kabla ya kujamiiana baada ya kutumia tembe za kuto mimba. Hata hivyo, ni muhimu kwako kusikiza mwili wako na ari yako. Ikiwa unahisi tayari kurudi kujamiiana unaweza kufanya hivyo. Ni muhimu pia kujua unaweza kuwa na uja uzito tena mapema hata kwa siku 8 baada ya kutumia…

Naweza kuwa na uwezo wa kupata uja uzito baada ya utoaji mimba?

Uwezo wako wa kuwa na uja uzito unaweza kurudi haraka sana baada ya utoaji mimba, wakati mwingine haraka hata kwa siku 8 [1]. Ikiwa unataka kuwa na uja uzito siku za usoni, utoaji mimba haustahili kuzuia hii. Ikiwa unataka kuzuia mimba kuna njia nyingi za kupanga uzazi Tafadhali tazama www.findmymethod.org kwa maelezo zaidi. Sources [1]…

Nini kitafanyika ikiwa bado nina uja uzito baada ya kutumia tembe za kutoa mimba?

Ikiwa tembe za kutoa mimba hazikutamatisha uja uzito wako, unaweza kujaribu tena au uwe na utoaji mimba kwa upasuaji ikiwa huduma hii inapatikana mahali unapoishi. Ili kutumia tembe za kutoa mimba tena inapendekezwa usubiri saa 72 tangu wakati wa mwisho ulipozitumia. Wasiliana nasi ikiwa una maswali kuhusu jinsi ya kutumia tembe za kuavya mimba.

Nastahili kupumzika siku ngapi baada ya kutumia tembe za kutoa mimba?

Kupumzika baada ya utoaji mimba kwa utabibu si lazima, ingawa inapendekezwa ili wewe ujihisi kuwa sawa zaidi. Ikiwa unatumia Mifepristone kuna uwezekano utaendelea na shughuli zako za siku na kuelekea hadi kabla ya kutumia Misoprostol. Mara tu baada ya kutumia Misoprostol utakuwa na msokoto na kutokwa damu Wanawake wengi wanapendelea kupumzika msokoto na kutokwa damu…

Nawezaje kukabili maumivu yanayohusiana na tembe za kutoa mimba?

Ibuprofen ipo ukitaka kununua katika nchi nyingi, na hii ni dawa iliyopendekezwa kutumia kwa ajili ya maumivu na msokoto. Unaweza kutumia tembe 3-4 (200mg) za ibuprofen kila saa 6-8 kwa maumivu. Tylenol pia inaweza kutumika, tembe 2 (325mg ya tembe) kila saa 4-6 kwa maumivu. Visodo vya kuleta joto au kupapasa sehemu ya chini ya…

Tuko hapa kukuunga mkono Kwa chaguo lako la kuavya mimba wakati wa COVID-19

Tunafuatilia Kwa makini ueneaji wa virusi vya Corona kimataifa na tutaendelea kusasisha habari na huduma zetu.

Tunawashauri wasomaji wetu:

  1. Kusoma chapisho letu la hivi karibuni la blogi juu ya uavyaji wa mimba na COVID-19
  2. Kufuata miongozo ya usalama wa Shirika la Afya Duniani kuhusu COVID-19
  3. Kuwasiliana na washauri wetu