Ushuhuda Meksiko, umri wa miaka 23

Kwanza ningependa kushukuru tovuti hii kwa sababu ilinisaidia wakati ambapo hakuna yeyote aliyenisaidia. Ilinipa taarifa na ilikuwa salama na ya faragha. Ninakiri kwamba mwanzoni nilikuwa na shaka nyingi. Mwishoni ilinisaidia sana kwa sababu kabla ya kupata safe2choose tovuti zingine hazikunisaidia na zilinipa taarifa zisizotosha.

Nilikuwa na mimba ya wiki 8 nilipoamua kutoa mimba. Nilikuwa na wakati mgumu sana lakini niliitimiza kwa sababu nilikuwa ninaamini, na bado ninaamini kwamba lilikuwa chaguo bora kwangu – kwa hali yangu ya kifedha, familia na elimu. Nilimeza jumla ya vidonge 12. Nilitapika baada ya dozi ya kwanza, niliendesha na nilikuwa na maumivu makali chini ya kitovu mwanzoni. Saa 5 baadaye nilianza kuvuja damu na siku 3 baada ya kumeza vidonge niliweza kuona kiinitete. Sikuhisi vibaya sana jinsi nilivyodhani, ilikuwa kama hedhi ya muda mrefu kwa sababu nilivuja damu kwa wiki 6 au chache. Sikuhitaji kuenda hospitalini, lakini nilichunguzwa na mwanajinakolojia wangu. Mpenzi wangu alinisaidia wakati wa mchakato wote na nadhani kwamba ni muhimu kuwa na mtu hapo.

Kila kitu kilikuwa salama na ya faragha. Kwangu, mchakato wa kutoa mimba uliniathiri sana kihisia kuliko kimwili – Huwa ninaiwaza na ninajua kwamba haikuwa wakati bora kwangu wa kuwa na watoto, lakini siku moja nitakuwa nao. Ikiwa una uhakika kwamba unataka kutoa mimba uko salama na safe2choose, na ninazungumza kutokana na niliyoshuhudia. Miezi 4 imepita na niko salama.

  • Share your story!

    Share your testimonial with safe2choose! It'll take only a few minutes of your time.

  • Share your story: Upload your story in any of the following format (video, photo, voice recording):

  • safe2choose will not publish stories that are offensive in any way, nor that contradict the safe2choose medical abortion protocols which are based off international medical organizations and our medical team.

  • Sehemu hii ni kwa madhumuni ya uthibitishaji na inapaswa kuachwa bila kubadilishwa.